Si sawa hata kidogo kulinganisha umaskini/utajiri wa nyumba A na B kwa mfumo wao wa maisha

Si sawa hata kidogo kulinganisha umaskini/utajiri wa nyumba A na B kwa mfumo wao wa maisha

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,916
Reaction score
6,527
Katika hali halisi ya maisha hatuwezi watu wote kualingana namna tunavyoendesha maisha yetu. Vivyo hivyo hata mataifa hayawezi kufanana kiuchumi. Vigezo vya upimaji wa uchumi si tu namna wanavyoishi bali pia hupimwa kutegemea na rasilimali zilizopo katika nchi husika..

Hakuna asiyejua kuwa Tanzania ni nchi tajiri hivyo wananchi wake wanastahili kuishi kulingana na utajiri wa nchi yao.

Hizo nchi zinazolinganishwa huenda hazina hata ziwa moja,hazina mlima maarufu, hazina madini nk nk..

Ni sawa na kulinganisha maisha ya watoto wa masaki na wanaoishi tandale. Uchumi wao hauwezi kulingana. Eti kwasababu wa tandale wanalala chumba kimoja na kitanda kimoja wa kike na kiume basi na wa masaki vivyo hivyo. Hii si sawa.

Tanzania ni nchi tajiri. Ina rasilimali nyingi kulinganisha na nchi nyingi za Afrika. Vijana wa kitanzania waastahili kufaidi matunda ya nchi yao pasipo kuwasimanga
 
Back
Top Bottom