May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Sio tatizo kumpongeza Mtu alivyovaa na kupendeza, lakini ni vipi unampongeza Mtu kwa kuwa ni Mzuri au umbile lake zuri?...sio tatizo kumpongeza Mtu aliyefanya mazoezi na kutengeneza muonekano wa mwili (body building).
Hivi kwa akili zetu hizi huyo tunayempongeza ana mchango gani kumfanya yeye kuwa na muonekano huo wa sura au umbile?...yeye si amezaliwa tu na kujikuta yupo hivyo?...sasa sifa zinamuhusu nini?.
Sifa hutolewa kwa Mtu aliyejituma na kufanya bidii kufanikisha jambo fulani, iwe kwa kutumia nguvu zake au kwa kufikiri kwa bidii kufanikisha hilo alilolifanikisha.
Na kinyume chake basi pia ni kukosa busara kwa hali ya juu kumbeza, kumdhalilisha au kumkosoa anayeonekana kukosa mvuto wa sura na umbile.
Pia kwa maneno mengine basi ni ukosefu wa busara kwa aliye na mvuto kwa sura nzuri na umbile kujiona bora kuliko aliowazidi.