maroon7
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 11,311
- 15,640
Si kwamba sikuwa na utaratibu wa kutowa tip, ila nilikuwa sijali na nilikuwa sioni kama inasaidia. Baada ya mimi kuyumba miaka fulani na kulazimika kujiajiri kwenye biashara fulani ambayo ndio ilinisitiri japo kuna siku unatoka kapa.
Ila kitu nilichojifunza kwa mtu kukupa buku au jero tu kama tip ilikua kubwa sana kwasababu kuna siku hata nauli mtu inatokea unakosa na jero uliyopewa inakusitiri, au buku inakuvusha mchana.
Tangu nimerudi kwenye mstari siachi kutoa tip sababu nimeelewa umuhimu na msaada inayompa mtu mradi tu usinihudimie vibaya.