Siamini kama Aziz Kii kasajiliwa Wydad kwa ajili ya kombe la dunia la vilabu

Siamini kama Aziz Kii kasajiliwa Wydad kwa ajili ya kombe la dunia la vilabu

Aziz Ki amekuwa mzito na hana tena nguvu za miguu. Hata mashuti yake hayana tena uhatari wala nguvu.

Niliwahi kusema ilitakiwa aende Wydad mapema hata miezi 6 nyuma apate mazoezi ya nguvu ili arudishe utimamu wa mwili kujiandaa kwa CWC.
 
Aziz Ki amekuwa mzito na hana tena nguvu za miguu. Hata mashuti yake hayana tena uhatari wala nguvu.

Niliwahi kusema ilitakiwa aende Wydad mapema hata miezi 6 nyuma apate mazoezi ya nguvu kujiandaa kwa CWC ili arudishe utimamu wa mwili.
Ulisema wewe kama nani?
 
Nyoosheni maelezo, Kimsingi Ki pale Wydad ni Galasa.

Ni hawa Wachambuzi wetu wa mchongo ndo Wanawapaishaga.

Kama Walivyowahi kumpaisha Mzize , wakati Wydad hawana time na mchezaji type ya Mzize.
 
Cha msingi Yanga wao tayari wameshafanya biashara, aliyenunua bidhaa bila kukagua atajua mwenyewe atakapoifungua nyumbani kwake maana hata sisi tunaponunua Simu Kariakoo tunakutana na mengi tu unakuta cover ni Samsung halafu ukiiwasha inaleta image ya Tecno
 
Yule Marasta nani sijui aliyesajiliwa Wydad majuzi ameshawahi kukaa benchi kweli achilia mbali kucheza?
 
Ki bado ni bonge la mchezaji ila hawezi anza mbele ya Rochi na huyu sidhani kama widad watarudi naye Africa Rochi is next level

Ki nimemuona dakk za mwisho kwa sababu ya muunganiko na Timu lkn akicheza 10 anakuwa comfortable sana yaani free role

Atacheza vzr na atawika subiri aingie kwenye mfumo
 
Back
Top Bottom