Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
Zamani wazungu walikuwa wanawabagua wajapani wakiwaita nyani. Lakini baada ya wajapan kuendelea na kuonyesha mambo wanayoweza kufanya kumekuwa na heshima kubwa sana kati yao.
Wajapan wenyewe walikuwa wana wabagua wachina na kuwaita watu wagonjwa wa Asia. Leo mchina ameonyesha uwezo wake duniani na ana heshimika sana. Mi naamini ubaguzi wa rangi unatokana na mtu kuona sifa fulani mbaya kama ujinga na umaskini vimetamalaki kwa watu wa aina fulani na kuamua kuvihusisha na rangi yao. Akiona ujinga upo sana kwa waafrika anaishia kusema waafrika au watu weusi hawana akili. Akiona umaskini umetamalaki afrika anasema kuwa watu weusi hawawezi kutatua shida zao. Hili ndilo linazaa ubaguzi wa rangi.
Hii kitu kwenye saikolojia inaitwa conditioning. Polepole mtu anaanza kuhusianisha vitu ambavyo havihusiani. Hata hapa kuna namna tunahusisha kuwa kabila fulani lina akili au lina hivi na vile. Ukifuatilia vizuri unakuta kuwa katika hilo kabila hakuhusiani chochote na akili. Ndicho ninachoona kwenye ubaguzi wa rangi.
Najua weusi nao tuna ubaguzi wa rangi lakini najiuliza hivi wazungu ndiyo wangekuwa na umaskini, ujinga na maradhi tuliyo nayo waafrika na waafrika tungekuwa na hali waliyo nayo wazungu ubaguzi nao ungegeuka? Yaani mzungu ndiye angekuwa analia kila siku kuwa anabaguliwa? Au pamoja na utajiri wetu, afya bora, kutengeneza ndege na elimu yetu bado mzungu anayeishi maeneo kama Tandale, mwenye afya mbovu na asiye na shule angetubagua?
Mi naamini tunaoita ubaguzi wa rangi hausababishwi na rangi yetu bali hali yetu. Umaskini wetu, ujinga wetu, maradhi yetu, uchafu wetu na mambo mengine ya kuchukiza tuliyo nayo. Naona ili ubaguzi wa rangi uishe na tuheshimike inatubidi tubadili hali za maisha yetu vinginevyo hali zetu zitahusishwa na rangi zetu na ubaguzi utaendelea.