Siamini kama duniani kuna ubaguzi wa rangi

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Zamani wazungu walikuwa wanawabagua wajapani wakiwaita nyani. Lakini baada ya wajapan kuendelea na kuonyesha mambo wanayoweza kufanya kumekuwa na heshima kubwa sana kati yao.

Wajapan wenyewe walikuwa wana wabagua wachina na kuwaita watu wagonjwa wa Asia. Leo mchina ameonyesha uwezo wake duniani na ana heshimika sana. Mi naamini ubaguzi wa rangi unatokana na mtu kuona sifa fulani mbaya kama ujinga na umaskini vimetamalaki kwa watu wa aina fulani na kuamua kuvihusisha na rangi yao. Akiona ujinga upo sana kwa waafrika anaishia kusema waafrika au watu weusi hawana akili. Akiona umaskini umetamalaki afrika anasema kuwa watu weusi hawawezi kutatua shida zao. Hili ndilo linazaa ubaguzi wa rangi.

Hii kitu kwenye saikolojia inaitwa conditioning. Polepole mtu anaanza kuhusianisha vitu ambavyo havihusiani. Hata hapa kuna namna tunahusisha kuwa kabila fulani lina akili au lina hivi na vile. Ukifuatilia vizuri unakuta kuwa katika hilo kabila hakuhusiani chochote na akili. Ndicho ninachoona kwenye ubaguzi wa rangi.

Najua weusi nao tuna ubaguzi wa rangi lakini najiuliza hivi wazungu ndiyo wangekuwa na umaskini, ujinga na maradhi tuliyo nayo waafrika na waafrika tungekuwa na hali waliyo nayo wazungu ubaguzi nao ungegeuka? Yaani mzungu ndiye angekuwa analia kila siku kuwa anabaguliwa? Au pamoja na utajiri wetu, afya bora, kutengeneza ndege na elimu yetu bado mzungu anayeishi maeneo kama Tandale, mwenye afya mbovu na asiye na shule angetubagua?

Mi naamini tunaoita ubaguzi wa rangi hausababishwi na rangi yetu bali hali yetu. Umaskini wetu, ujinga wetu, maradhi yetu, uchafu wetu na mambo mengine ya kuchukiza tuliyo nayo. Naona ili ubaguzi wa rangi uishe na tuheshimike inatubidi tubadili hali za maisha yetu vinginevyo hali zetu zitahusishwa na rangi zetu na ubaguzi utaendelea.
 
Waafrika wakiitwa weusi na mzungu, wazungu ndio wanalalamika kwa hiko kitendo
Kwanini lukaku asiite mweusi (black) kwani lukaku mzungu yule!!!!

Hapa kuna mtego hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uko sahihi kwa 100%.

If africa ingekuwa tajiri na bara lilioendelea sawa au zaidi ya china au marekani basi mtu mwenye asili ya africa asingehisi kubaguliwa wala hakuna ambaye angethubu kubagua watu wenye asili ya africa.

Kama ambavyo masikini anavyojihisi kubaguliwa na tajiri ndicho kinachotokea hapa.
Mtu aliyezidiwa siku zote ndio hulalamika na kujiona anabaguliwa au hapendwi.

Ukitaka kujua ubaguzi wa rangi hauhusiani na rangi basi angalia watu weusi waliozungukwa na wazungu like Idris Elba, Denzel Washington, Morgan Freeman, samuel Jackson na labda will smith pia jayz na kanye west ngoja nimuweke na obama.

Ukiangalia kwa makini hao watu hawezi kubaguliwa wala hawajihisi kubaguliwa. Huo ni mfano mdogo tu.
Pia nimetaja hao watu wenye class fulani kwa makusudi.

So if africa ikiweza kusimama na kuonyesha uwezo wake uliojificha basi ubaguzi utaisha kwa watu wenye asili ya africa.

Like utanibagua umenizidi nini kama tuko sawa au nimekuzidi kimaendeleo, kiuchumi, kwenye technology na kielimu.

Sasa hapo naturally mbaguzi wa rangi angejiona yeye ni idiot kabla jamii zote hazitomuona yeye ni idiot.
 
Ukitaka kujua ubaguzi wa rangi hauhusiani na rangi basi angalia watu weusi waliozungukwa na wazungu like Idris Elba, Denzel Washington, Morgan Freeman, samuel Jackson na labda will smith pia jayz na kanye west.

Ukiangalia kwa makini hao watu hawezi kubaguliwa wala hawajihisi kubaguliwa. Huo ni mfano mdogo tu.
Pia nimetaja hao watu wenye class fulani kwa makusudi.

So if africa ikiweza kusimama na kuonyesha uwezo wake uliojificha basi ubaguzi utaisha kwa watu wenye asili ya africa.

Like utanibagua umenizidi nini kama tuko sawa au nimekuzidi kimaendeleo, kiuchumi, kwenye technology na kielimu.

Sasa hapo naturally mbaguzi wa rangi angejiona yeye ni idiot kabla jamii zote hazitomuona yeye ni idiot.
Hapa umemaliza mkuu.
 
Zamani wazungu walikuwa wanawabagua wajapani wakiwaita nyani. Lakini baada ya wajapan kuendelea na kuonyesha mambo wanayoweza kufanya kumekuwa na heshima kubwa sana kati yao.

Wajapan wenyewe walikuwa wana wabagua wachina na kuwaita watu wagonjwa wa Asia. Leo mchina ameonyesha uwezo wake duniani na ana heshimika sana. Mi naamini ubaguzi wa rangi unatokana na mtu kuona sifa fulani mbaya kama ujinga na umaskini vimetamalaki kwa watu wa aina fulani na kuamua kuvihusisha na rangi yao. Akiona ujinga upo sana kwa waafrika anaishia kusema waafrika au watu weusi hawana akili. Akiona umaskini umetamalaki afrika anasema kuwa watu weusi hawawezi kutatua shida zao. Hili ndilo linazaa ubaguzi wa rangi.

Hii kitu kwenye saikolojia inaitwa conditioning. Polepole mtu anaanza kuhusianisha vitu ambavyo havihusiani. Hata hapa kuna namna tunahusisha kuwa kabila fulani lina akili au lina hivi na vile. Ukifuatilia vizuri unakuta kuwa katika hilo kabila hakuhusiani chochote na akili. Ndicho ninachoona kwenye ubaguzi wa rangi.

Najua weusi nao tuna ubaguzi wa rangi lakini najiuliza hivi wazungu ndiyo wangekuwa na umaskini, ujinga na maradhi tuliyo nayo waafrika na waafrika tungekuwa na hali waliyo nayo wazungu ubaguzi nao ungegeuka? Yaani mzungu ndiye angekuwa analia kila siku kuwa anabaguliwa? Au pamoja na utajiri wetu, afya bora, kutengeneza ndege na elimu yetu bado mzungu anayeishi maeneo kama Tandale, mwenye afya mbovu na asiye na shule angetubagua?

Mi naamini tunaoita ubaguzi wa rangi hausababishwi na rangi yetu bali hali yetu. Umaskini wetu, ujinga wetu, maradhi yetu, uchafu wetu na mambo mengine ya kuchukiza tuliyo nayo. Naona ili ubaguzi wa rangi uishe na tuheshimike inatubidi tubadili hali za maisha yetu vinginevyo hali zetu zitahusishwa na rangi zetu na ubaguzi utaendelea.
Uzi bora
Ni kweli umasikini wa akili ndio chanzo cha kubaguliwa maana mtu akiwa maskini wa akili hawezi fanya chochote na mwisho hubakia kulalama kuwa anabaguliwa
 
Uko sahihi kwa 100%.

If africa ingekuwa tajiri na bara lilioendelea sawa au zaidi ya china au marekani basi mtu mwenye asili ya africa asingehisi kubaguliwa wala hakuna ambaye angethubu kubagua watu wenye asili ya africa.

Kama ambavyo masikini anavyojihisi kubaguliwa na tajiri ndicho kinachotokea hapa.
Mtu aliyezidiwa siku zote ndio hulalamika na kujiona anabaguliwa au hapendwi.

Ukitaka kujua ubaguzi wa rangi hauhusiani na rangi basi angalia watu weusi waliozungukwa na wazungu like Idris Elba, Denzel Washington, Morgan Freeman, samuel Jackson na labda will smith pia jayz na kanye west ngoja nimuweke na obama.

Ukiangalia kwa makini hao watu hawezi kubaguliwa wala hawajihisi kubaguliwa. Huo ni mfano mdogo tu.
Pia nimetaja hao watu wenye class fulani kwa makusudi.

So if africa ikiweza kusimama na kuonyesha uwezo wake uliojificha basi ubaguzi utaisha kwa watu wenye asili ya africa.

Like utanibagua umenizidi nini kama tuko sawa au nimekuzidi kimaendeleo, kiuchumi, kwenye technology na kielimu.

Sasa hapo naturally mbaguzi wa rangi angejiona yeye ni idiot kabla jamii zote hazitomuona yeye ni idiot.

A quick google such could tell you otherwise. Watu weusi mashuhuri wengi tu wamekutana na ubaguzi, kwenye link hapa chini Elba mwenyewe kathibitha hilo na watu wengine.

Yeah mara nyingi na sio maisha yao yote.
Pia sijasema hawabaguliwi bali wanaowabagua ni idiots wachache let's say chuki.
Na hao jamaa hata kama wanabaguliwa huwezi kufananisha na ubaguzi wa wamarekani weusi wa kawaida au africans.

Btw siamini kila ninachokiona Google sababu wanaoandika ni watu kama mimi na sio kila kilichopo Google ni sahihi sababu hata mimi ningeandika nilichoandika huko Google then ungeamini.
 
Kuna motion interviews zao online as well.
 
hata waafrika wa ulaya huwa hawabaguliwa bali sisi (tulio afrika)na upuuzi wetu akili zetu ndogo zinawafanya wafananishwe na sisi
 
Rejea kwa Samweli Eto'o mbona alibagulia na waispain na ukiangalia alikua yuko vzuri kiuchumi hata kulisakata bumbu

Me nadhani dhana ya ubaguzi hii ipo kiasili kwa baadhi ya mataifa mf mkiwa imani tofauti mnabaguana,

Ukiangalia hata ombaomba wengi hapa Dar hupendelea kuvaa mavazi ya kiislam kwakuamini hili jiji limejaa waislam hivyo itakua rahisi kusaidiwa na kutobagulia

Huo wangu mtazamo wazee msijenge chuki
 
Zamani wazungu walikuwa wanawabagua wajapani wakiwaita nyani. Lakini baada ya wajapan kuendelea na kuonyesha mambo wanayoweza kufanya kumekuwa na heshima kubwa sana kati yao.

Wajapan wenyewe walikuwa wana wabagua wachina na kuwaita watu wagonjwa wa Asia. Leo mchina ameonyesha uwezo wake duniani na ana heshimika sana. Mi naamini ubaguzi wa rangi unatokana na mtu kuona sifa fulani mbaya kama ujinga na umaskini vimetamalaki kwa watu wa aina fulani na kuamua kuvihusisha na rangi yao. Akiona ujinga upo sana kwa waafrika anaishia kusema waafrika au watu weusi hawana akili. Akiona umaskini umetamalaki afrika anasema kuwa watu weusi hawawezi kutatua shida zao. Hili ndilo linazaa ubaguzi wa rangi.

Hii kitu kwenye saikolojia inaitwa conditioning. Polepole mtu anaanza kuhusianisha vitu ambavyo havihusiani. Hata hapa kuna namna tunahusisha kuwa kabila fulani lina akili au lina hivi na vile. Ukifuatilia vizuri unakuta kuwa katika hilo kabila hakuhusiani chochote na akili. Ndicho ninachoona kwenye ubaguzi wa rangi.

Najua weusi nao tuna ubaguzi wa rangi lakini najiuliza hivi wazungu ndiyo wangekuwa na umaskini, ujinga na maradhi tuliyo nayo waafrika na waafrika tungekuwa na hali waliyo nayo wazungu ubaguzi nao ungegeuka? Yaani mzungu ndiye angekuwa analia kila siku kuwa anabaguliwa? Au pamoja na utajiri wetu, afya bora, kutengeneza ndege na elimu yetu bado mzungu anayeishi maeneo kama Tandale, mwenye afya mbovu na asiye na shule angetubagua?

Mi naamini tunaoita ubaguzi wa rangi hausababishwi na rangi yetu bali hali yetu. Umaskini wetu, ujinga wetu, maradhi yetu, uchafu wetu na mambo mengine ya kuchukiza tuliyo nayo. Naona ili ubaguzi wa rangi uishe na tuheshimike inatubidi tubadili hali za maisha yetu vinginevyo hali zetu zitahusishwa na rangi zetu na ubaguzi utaendelea.

You cannot win with the topic ya ubaguzi wa rangi:

1. Ukisema hakuna ubaguzi, pana grievance industry nzima itakayokushukia. Na wengine wanaweza kukuita majina ya kebehi kama vile "Uncle Tom". Utawaudhi theluthi ya watu kwa wastani.

2. Ukisema kuna ubaguzi, unawaudhi wale wanaosema ubaguzi ulishaisha. Tena sasa hivi imefikia kuwa upendeleo. Mnataka nini tena? Mbona kila kitu mmepewa, na kuzidi. Na wengine wanaweza kukuita majina ya kebehi kama vile "Useful Idiot". Utawaudhi theluthi ya watu kwa wastani.

3. Kundi la tatu lililobaki halijali kuwepo na ubaguzi, au kusiwepo. Lenyewe halitaki kusikia habari za kuwepo au kutokuwepo kwa ubaguzi.

Sera yangu binafsi ni kutozungumzia masuala ya ubaguzi wa rangi. Leo nimekiuka 😉 Exceptions prove the rules!
 
Pole mkuu.

Pole mkuu kwa kudumbukia humu. Kuna principle moja inasema kuwa akili inapenda kuamini inachokitaka. Mfano, unakuta suala liko wazi lakini mshabiki wa Yanga anasema goli na wa Simba anasema siyo goli. Na hapa hii ishu iko hivi hivi lakini ukweli upo.
 
Mzee baba ubaguzi wa mtu mweusi dhidi ya mweusi mwenzake/ukabila(upo umejaa tele) ubaguzi wa mtu mweupe dhidi ya mtu mweusi (ubaguzi wa rangi upo na wala sio wa kuisha leo wala kesho) Afrika kusini,ulaya na amerika ya kusini nimeshuhudia kwa macho yangu sijahadithiwa
Nalog off
 
Back
Top Bottom