Siamini kama kuna mpumbavu anayeinimi Simba inajilinganisha na Yanga

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Ukiona mashabiki wa Simba wakilalamikia timu yao,kama una akili nzuri,utakumbuka jinsi mashabiki hao hao walivyoishangilia timu ikiwa imefungwa ama kutoa sare huku wameonesha soka bora kabisa.

Kwa sasa soka la timu limebadilika,wanacheza mpira wa malengo,na kwa hiyo kuna baadhi ya vitu watu wanavyotarajia kuviona hawataviona.

Ile kasi na pressing ya nguvu imepungua,lakini wanapata matokeo.
Soka wanalocheza Simba ni la kibrazil.Soka hili linahitaji watu wazuri wenye vipaji vikubwa mno.Watu ambao akishuti golini hatakiwi kupiga off target.Ni vigumu sana kuwa na wachezaji wengi wa jinsi hii.

Soka la kisasa ni la kasi,maarifa na nguvu.
Maarifa na nguvu peke yake vitakupa ushindi tu kwa timu unayoizidi maarifa.
Kasi husaidia kuvuruga mfumo wa kujilinda wa adui.

Simba ya sasa inashindanishwa na Simba ya zamani na siyo yanga.Ndio maana sio ajabu kusikia wakisema ile Simba ya akina Luis iliyomfunga El Ahly sasa hivi hatuioni
 
Naomba Tukubaliane kwa pamoja madhaifu ya Simba kama ifuatavyo.

1. Uongozi mbovu MANGUNGU, Salim Abdallah (mo) nk.

2. Body ya wakurugenzi WASIOJUA Mpira (Asha Baraka)

3. Scauting Mbovu

4.Kamati Mbovu ya Usajili. (B12)

5. Wanakocha Mbovu Sana.
(Hakuna KOCHA wa kibrazil ANAYEFANYA Vizuri Dunia nzima)

6. Kusajili wachezaji bila Mipango na Malengo.
MIQUISON, Ngoma.

7. Idadi Kubwa Ya Mawinga 8 Raia wa KIGENI.
Kukosa Mabeki na Viungo WA UKABAJI NO 6.

8. Kuendekeza wachezaji wale wale na waliochoka.
Boko, chama, SHOMARI,

9. Mashabiki WAPUMBAVU wanaozomea KOCHA kwa KUMTOA mchezaji.

10. Mashabiki WAJINGA wanashindwa kuhoji mambo ya maana Uwanja,
KUSHINDWA kuinflienceisajili WA wachezaji Wazuri.
Mashabiki WA ndio Mzee.

PUMBAFU KABISAAAAA.
 
Kuna binadamu wasio na madhaifu?

Kama tunakubaliana kuwa hakuna binadamu asiye na madhaifu,basi ni kweli hata viongozi wa Simba wana madhaifu kama walivyo wa utopolo wanaotumia mbinu za kimafia kupata ubingwa.


Na wewe nadhani ni mmoja kati ya watu sio tu wenye madhaifu bali mapungufu ya akili.

Ni chizi pekee anayeweza kulaumu eti kwa nini Chama anachezeshwa
 
Sio kweli. Usikimbie ukweli. Wengi wenu wanalinganisha na YANGA wanaiona soka la simba ukilinganisha na YANGA bado sana. Wote tuko mitaani humu humu kwani hatusikii na kuona. Hiyo ya soka sijui lini lini hiyo yako,lakini ukweli wazi.

Mnacheza mdundo wa YANGA. Kibaya zaidi hata yule mlopokaji wenu amegeuka kabisa amekuwa msemaji wa YANGA. Msikikize kila sentensi moja neno YANGA atalitupia mara 2,3. Akiumia mchezaji wa mbumbumbu atasema YANGA. Mbumbumbu wakicheza vibaya atasema YANGA.

Lakini wasikilize YANGA wanafanya yao,hawana habari na mbumbumbu fc
 


1. Mimi binafsi sina Madhaifu.

2. Taasisi kama taasisi haipaswi kuwa na madhaifu kwasababu ni collective responsbility

Taasisi inaajiri WATU zaidi ya 20
Hayo madhaifu yanatoka wapi????

3. Sijui Hiyo timu ya UTOPOLO unayo izungumzia
Na FIFA wenye Mpira wao wanakataza mno upangaji WA MATOKEO.
ADHABU yake ni Mbaya sana.

4. Mimi Sina Upungufu WA akili kama unavyodhani otherwise unanionea wivu kwa uwezo wangu Mkubwa niliopewa na Mungu.

5. Hakuna ALIYESEMA chama kuchezeshwa ama kutochezwshwa Mimi nimezungumzia KUTOLEWA uwanjani kama substitution. Mashabiki MAANDAZI kama wewe HAWATAKI chama atolewe.

FIKICHA AKILI USISHINDANE NA WATU WENYE AKILI TIMAMU CHENZI KABISA QMM
 
Mbinu gani za kimafia na Sisi tuige mkuu
 
Mbinu gani za kimafia na Sisi tuige mkuu
Mbinu za kimafia za Yanga anamaanisha bahasha kama Ile ya kuhonga wachezaji na refa Kisha Kuifunga USM Algers kwao mechi ya fainali Shirikisho Africa!

Mbumbumbu fc wamebaki na akili ya 1947! Hawakubali Yanga ya Hersi ni boli inatembea!

Hata Max Nzengeli anavyotembeza boli Hawataki kusifia! Au msako wa Yanga kama Bado hawajakufunga goli nalo pia hawalioni!
 
Nimekuelewa
 
Kasoro namba 6 mengine yote nakuunga mkono.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…