Siamini naanza kuacha uhuni, umalaya, ubazazi na ubaradhuli. Huyu mtoto nimemuibua humu humu JamiiForums

Siamini naanza kuacha uhuni, umalaya, ubazazi na ubaradhuli. Huyu mtoto nimemuibua humu humu JamiiForums

Waungwana habari za mchana. poleni na kazi ndugu zanguni. naandika hapa nikiwa nimefurikwa na furaha pomoni. katika harakati zangu za kutafuta mwenzi wa kufanana naye kwa mazuri naanza kuona uelekeo. waswahili wanasema "nyota njema huonekana asubuhi" na nimeamini "mwenda bure si sawa na mkaa bure" nimejipatia kimwana wa haja hasa.

siku nyingi nilikuwa natamani niweze kuibuka humu na mtoto mmoja mzuri classic anipende mimi na mauza uza yangu.awe mzuri wa sura,mwili na tabia isije ikawa story ile ya "uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti"

"jungu kuu halikosi ukoko" nimefanikiwa kumpata mtoto mmoja mzuri sana toka sehemu flani za tanganyika maarufu kwa kutoa mabinti warembo. nimegundua kumbe humu kuna mabinti hujitoa akili tu ila ukiwa nao nje wana akili nzuri zimetulia kabisa.amenishauri kuwa basi nipunguze ubazazi nami kuanzia leo nimeanza kubadilika. nitakuwa goodman kabisa...(ila tu siyo ndo watu wengine waanze kunitibua maana waswahili wanasema "jasiri haachi asili"

nawaambia ndugu zanguni" mgaa gaa na upwa hali wali mkavu" nami sasa nina anza kupata ahueni maana kumbukeni nliwahi kusema "mficha uchi hazai" nami nikaona kwa huyu dada nisifiche hisia zangu.(ingawa sisi wengine tushasahau kutongoza ) basi nikajiuma uma lakini maskini dada wa watu alishajua nia yangu ni nini... basi akanikubalia maana wahenga walisema "heri kenda nenda kuliko kumi nenda rudi" kanipata mkaka wa watu nlishafanya fanya uhuni kidogo nimetuliza majeshi.

nawashauri ndugu zangu.... nanyi mzidi kuwa na tabia njema ,wakweli na wawazi humu ndani watoto wazuri wapo sema ni mpaka uwe unajua kulenga... otherwise utaishia tu kunaniii....bint wa watu hana makuu. ana shughuli zake.ana mvuto na anajiamini sana.si mswahili maana mi nawaogopa sana wanawake wa uswahilini mkigombana mwanamke wa uswahilini anaweza akakusema vibaya mpaka ukafa.huyu hata kwa sauti yake ni ya utulivu haina papara na anajua kuzungumza lugha kuu mbili. english na swahili hivyo hatutakuwa na shida ya mawasiliano. siyo zile type za kunitumia smg... no si hizo.

nami nawaambia "ukuu kuu wa kamba si upya wa mkambaa, japo ni nyembamba na tena imechakaa" mlikuwa mnasema gudume wa nini.. mwenzenu mrembo kila siku alikuwa anasali atanipata lini.
Nipe mbinu mkuu nateseka huku
 
mbinu ni kuwa mtulivu, mkweli na muwazi. kuwa mtulivu na mwenye tabia njema kama mimi.. kuwa mkweli na muwazi utapata mdada ambaye anapenda watu real kabisa siyo fake... usiwe mwanaume wa kichina.

mmmmh kichina
 
mbinu ni kuwa mtulivu, mkweli na muwazi. kuwa mtulivu na mwenye tabia njema kama mimi.. kuwa mkweli na muwazi utapata mdada ambaye anapenda watu real kabisa siyo fake... usiwe mwanaume wa kichina.
Gudume nakupenda kwenye wivu wajinyonge
 
Back
Top Bottom