Siasa imeua ujasiri, wanataaluma wameuchimbia kaburi, tunasubiri wa kuuzika na kufukia

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2023
Posts
1,222
Reaction score
2,912
Miaka ya hivi karibuni wanasiasa wamekuwa na nguvu kubwa pengine kuliko kundi lolote kwenye jamii

Hii ni kwasababu, hata vyombo vya dola karibu vyote dalili nyingi zinaonyesha vinahofu na wanasiasa, vinaongozwa kwa kufuata mwanasiasa anataka wafanye nini

Polisi, mahakama, na vyombo vingine nyeti vya ulinzi na usalama wa nchi ambavyo kwa heshima yake huwa havisemwi semwi kiholela hadharani navyo kuna dalili kubwa viko chini ya siasa za wanasiasa

Hali hii imedumaza watu majasiri waliokuwa na uwezo wa kusema fikra zao hadharani, kukemea uovu, kukosoa na kupendekeza njia nzuri ya kufanya waamue kukaa kimya kwa hofu ya kukosa msaada pindi mdomo wa mwanasiasa utakapochanua kuwameza

Wafanyakazi wa umma hawana ujasiri wa kuwahoji viongozi wao kwasababu ya kuogopa siasa isiwanyang'anye vyeo vyao

Diwani ana nguvu ya kumkoromea Mkurugenzi wa halmashauri na hata kumuondoa ofisini kwa mizengwe tu ya kisiasa

Mzazi anauwezo wa kutishia kibarua cha Mkuu wa shule kwasababu ya kudai mchango wa chakula atakachokula mwanae shuleni ili asome vizuri

Katika wimbi kama hili, ulitarajia kuona wasomi wa vyuo vikuu ambao tunaamini hawafungamani na siasa wakija na mijadala moto moto ya kulitoa taifa hapa lilipofikia;

Hata hivyo; na wao wanaonekana kumezwa na mdomo huo huo wa wanasiasa

Kwa wiki kadhaa sasa tumekuwa tukisoma habari za wahadhiri watatu (wawili wa St.John's na mmoja wa UDOM) wanaosota rumande kwa makosa ambayo inasadikika "ni ya mchongo" kwani walinukuliwa maneno waliyotamka wakiwa wanatimiza majukumu yao ya kujenga bongo za vijana darasani

Haiingii akilini eti muhadhiri haruhusiwi kufundisha darasani kwa kutolea mfano wa ufisadi wa "ESCROW"? wala kuwaambia vijana kwamba "maandamano ni haki ya kikatiba"

Kuwekwa kwao rumande ni kazi ya siasa kuua ujasiri wa kuwa na fikra huru.

Lengo la wanaofanya hivyo ni kudhibiti watu kuwaza, kufikiri wala kutenda kinyume na matakwa ya wanavyotaka wao.

Wanafahamu fika kwamba elimu bora inajenga fikra huru na ujasiri wa kusimamia unachokiamini

Wahadhiri hao kuwekwa kolokoloni kwa kufundisha ujasiri darasani ni jaribio la kufifisha na kuua watu majasiri katika nchi hii.

Wakati ambao wanasiasa wanafanya majaribio hayo ya kuua ujasiri, ungetegemea wanataaluma wa vyuo vikuu waamke na kujibu mashambulizi lakini sasa imekuwa tofauti

Tanzania kuna vyuo vikuu vingi sana, vyenye maelufu ya wahadhari, malaki ya wanavyuo lakini sauti zao hazisikiki zikiwatetea wenzao,

Matendo yao hayaonekani yakiwatetea wenzao, wala mioyo yao haionekani ikiwatetea wenzao wanaolala juu ya sakafu, kujisaidia pasipo na staha, kula kwa ratiba ya gereza. Kwao walioshikiliwa sio shida zao!

Hii ni ishara kwamba wanasiasa wamewazidi nguvu. Ni dalili kwamba baada ya kuua ujasiri sasa wanataaluma wanachimba kaburi la kuuzika ujasiri wa nchi hii

Katika hali ya kawaida, ulitegemea wahadhiri kote nchini waonyeshe dalili ya kukataa huo uonevu, wanavyuo kote nchini wawatetee walimu wao kwa kufanya linalowezekana

Maskini wasomi wetu wako bize! Husikii mgomo wa wahadhiri wala wanafunzi wa chuo chochote, husikii maandamano ya chuo, kitivo au hata wanafunzi waliokuwa darasani siku hiyo.

Wote wameingiwa na ubaridi, wanakigugumizi, hawana kauli wala matendo bali wanasubiri huruma ya mwanasiasa afanye jambo ambalo ataamua yeye.

Hawajui kwamba, mwanasiasa akiamuru waachiliwe itakuwa siraha kali zaidi ya kuwapoteza na kuwatoa kwenye reli

Wapo tu hawajui wafanyeje. Hawajui wawaleeje vijana wa vitivo vyao ili waje kulikomboa Taifa

Haishangazi kuona siku hizi somo linaloeleweka kiwepesi zaidi limekuwa "uchawa".

Wajifunze ujasiri kwa nani sasa wakati walezi wao pia hawana huo ujasiri?

Iko wapi ile migomo ya vyuo vikuu iliyotetemesha nchi? Yako wapi maandamano ya wanavyuo yaliyoketisha baraza la mawaziri na bunge kutafuta suruhu?

Kuwapa limit wahadhari kinyume na miongozo yao ya kitaaluma sio changamoto?

Anayejua kinachotakiwa kufundishwa darasani ni mwanasiasa au ni mkuu wa idara husika?

Anayetakiwa kumshitaki muhadhiri aliyefundisha kinyume na mtaala unavyoelekeza ni TCU au mwanasiasa?


Haya hayatakiwi kuhojiwa na hao wanataaluma wenzao?

Wamekubali kupokea maiti ya ujasiri na wameshika majembe, sururu wanachimba kaburi ili nchi izike ujasiri wa kuikomboa

Yanasubiriwa makundi mawili tu ili kuanua matanga;

kundi la kushusha jeneza la ujasiri na uthubutu kaburini na lile litakalorusha udongo kuufukia na hatimaye Taifa liwe limepotea rasmi maana hakuna Taifa bila wasomi na hakuna wasomi wasiojiamini na kusimamia yale wanayoyaamini
 
Ni kama tunajiandaa kuizika rasmi nchi yetu wenyewe.
 
Ni aibu kwa wasomi heti kesi za Ugaidi hii nchi Naona Kama haina mwenyewe Kama alivyosema Polepole
 
Tanzania ina vyuo vikuu zaidi ya 50 lakini ni nchi iliyojiwekea viwango vya chini sana vya mtu kuwa na sifa za kuwa kiongozi katika nchi hii. Hivi unategemea wasomi wa Tanzania wanaofanya PhD za kidhanifu na kuwafundisha vijana udhanifu walionao kichwani ndo watoke hadharani kupingana na wanasiasa!?
Angalia mifano ya akina Kabudi ambao vijana walidhani wanatema fact za kisayansi wakiwa pale UDSM kumbe wanawalisha wanafunzi udhanifu wao waliochukulia PhD. Ukiwauliza ile mihadhara waliyokuwa wanaitoa ambayo kwa kwa sasa wanaipinga walimaanisha nini watakwambia kijana acha kukosa uzalendo, tunza amani ya nchi.
 
Tufanyeje sasa maana nchi ni yetu sote na kila mwaka tunapeleka watoto wetu vyuo hivyo hivyo vyenye walimu hao hao waliofanya tafiti hizo hizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…