Siasa Mamboleo - Mdomo unapojaribu Kulidanganya Sikio

Siasa Mamboleo - Mdomo unapojaribu Kulidanganya Sikio

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Siasa na Propaganda zimekuwa zikifanyika tangia enzi...; ila imefika wakati watu kujaribu kukwambia kwamba nyeusi ni nyekundu yaani wanadhani wakitamka mara nyingi zaidi hata wao wenyewe mdomo wao utali-convince sikio lao...

Angalizo kwa hawa watu ukiwa ni mtu wa kusifia bila kupinga utaondoa authenticity yako..., hata siku ukiongea la maana watu wanaweza wasikusikilize...; Yaani ni bora uwe na mchele mdogo kila siku..., na sio kuchanganya pumba nyingi hata mchele usionekane.....
 
Pili badala ya kuziba wengine midomo ; kama hao so called wachochezi na waongo badala ya kuwafunga midomo kwanini msiwajibu kule kule kwenye uwanja wao...

Mfano badala ya kufungia Kazi ya Ney wa Mitengo (AMKENI) kwanini msije na kazi zenu zikijibu hoja za Ney kwamba anafanya Uchochezi; Mbona sijawahi sikia nyimbo inafungiwa kwa kuisifia Serikali kwa sifa za Uongo ? (Yaani kupotosha UMMA kwa kuipigia Serikali Propaganda)
Leo hata ukija na wimbo,
Mama ana macho mviringo,
Ana midomo mipana,
Anajua Kila kitu,
Anaweza Kila kitu.
HUTASIKIA NAPE WALA KIDAMPA YEYOTE ANAHOJI ZAIDI YA KUKUSIFIA NA WIMBO WAKO UTATUMIKA KWENYE KAMPENI.
 
Ni nani tunamdanganya ?

Watu wanalipwa Posho ili muonekane kama mmejaza Uwanja; Walipwaji Posho wanajua na waliopo nyumbani wanaelewa kwamba ndio mchezo wenu; Hapo nani anadanganywa ? Na wenye uelewa mnawapa chuki kwa kuona kwamba mnafuja pesa za mlipa Kodi, Mnamyanganya kwenye Ma-Tozo ili mzirudishe kwa posho ya elfu kumi kwa siku moja kwa mwaka.....

Haya Maigizo ambayo kila mtu anajua script mnadangaya huyo mtu au mnajaribu kuji-convince kwamba mnachofanya ni sawa ? Mdomo unajaribu kulidanganya sikio....
 
Back
Top Bottom