Siasa na Propaganda zimekuwa zikifanyika tangia enzi...; ila imefika wakati watu kujaribu kukwambia kwamba nyeusi ni nyekundu yaani wanadhani wakitamka mara nyingi zaidi hata wao wenyewe mdomo wao utali-convince sikio lao...
Angalizo kwa hawa watu ukiwa ni mtu wa kusifia bila kupinga utaondoa authenticity yako..., hata siku ukiongea la maana watu wanaweza wasikusikilize...; Yaani ni bora uwe na mchele mdogo kila siku..., na sio kuchanganya pumba nyingi hata mchele usionekane.....
Pili badala ya kuziba wengine midomo ; kama hao so called wachochezi na waongo badala ya kuwafunga midomo kwanini msiwajibu kule kule kwenye uwanja wao...
Mfano badala ya kufungia Kazi ya Ney wa Mitengo (AMKENI) kwanini msije na kazi zenu zikijibu hoja za Ney kwamba anafanya Uchochezi; Mbona sijawahi sikia nyimbo inafungiwa kwa kuisifia Serikali kwa sifa za Uongo ? (Yaani kupotosha UMMA kwa kuipigia Serikali Propaganda)