Siasa mbovu za mama kuku katika jaa la taka, ndiyo chanzo cha mwewe kupora vifaranga wake

Siasa mbovu za mama kuku katika jaa la taka, ndiyo chanzo cha mwewe kupora vifaranga wake

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
27,705
Reaction score
65,343
Mama kuku ana vifaranga vingi sana vimezagaa kila sehemu ya jaa la taka vikijitafutia. Vipo vilivyo dhoofu na vipo vyenye afya tele. Vingine vimeanza kuota mbawa, vingine bado.

Lkn kwenye jaa hilo kumeibuka balaa la vifaranga kuporwa mchana kweupe na mwewe. Kinyume na matatajio ya vifaranga, mama kuku amekuwa kimya sana juu ya uonevu huu unaofanywa na mwewe. Ktk hali ya kawaida huyu mama kuku alitarajiwa kuwa mkali sana na mpiga kelele namba moja pale mwewe anapojitokeza kutaka kupora vifaranga vyake.

Mjadala umeibuka miongoni mwa vifaranga na swali lao kubwa ni je, mama kuku kaungana na mwewe? Jaa la taka sasa hali si shwari, baadhi ya vifaranga wameanza kulikimbia.

Vifaranga waliobakia je, wataungana ili kupambana na mwewe? Muungano wa vifaranga utaweweza kupambana na mwewe bila ya mama kuku kuwasaidia?

Ikiwa mama kuku kaungana na mwewe, je, vifaranga wanaweza kumuonndoa mama kuku kwenye jaa? Ni jambo la kusubiri miujiza hii kutokea.

Jambo linalokatisha tamaa ni kwamba vifaranga vyenye mbawa na afya tele havioneshi utayari wa kumkabili mama kuku ama mwewe.
 
Tatizo ni njaa , mimi mwenyewe leo wakiweka ile b 1 niliyowapa ofaa kwenye account naaga chadema na nitawapandisha sukari mpaka mkome
 
Ndio shida ya kumpa KUKU mgeni tena "kishingo", Vifaranga wa "kuchi" ambao "mama" Yao mlikubali achinjwe kwa ajili ya "Wageni"!
Hataona uchungu wowote wa kulea hivyo Vifaranga,ambavyo sio vyake na hafanani nao kwa chochote,kuanzia umbo mpaka tabia!

Matokeo yake Vifaranga wameanza kupata taharuki kuwa Mama Yao mlezi "kishingo" anawatelekeza!
Hawaoni hata akijigusa "mwewe" anaposhuka!

Wakijaribu kujitetea kupambana na "mwewe" wao wenyewe wanakuja "kunguru wa unguja" wakubwa mithili ya "TAI"!
Hao wanameza kabisa Kila kitu hawabakishi hata manyoya Ili angalau Vifaranga wenzako wabaki na kumbukumbu!
Ubaya wa "kunguru wa unguja" anashambulia mpaka ndege wengine hasa akiwa "kasuku"!
Hili jambo limewafanya mpaka "bundi" wastuke!
Kwamba Leo,KUKU ameshindwa kutetea Vifaranga hata kama sio vyake!
Na "kunguru" aliyekuwa imported kutoka "India" kwa minajili ya kusafisha "JIJI" Leo ndio amekuwa "Malkia" wa anga!
Leo hii "TAI" na "KONGONI" wanawaacha "mwewe" na "kunguru" wanatamba!
Uzuri ni kwamba Vifaranga ni vya jamii ya "Kuchi",hawa wanakuwa kwa haraka na kivyovyote hawatamalizwa wote!
Kwa "Kuchi" walivyo,wanaweza kumpiga KUKU mwingine mpaka akamgoshoo!
Mama mlezi KUKU "kishingo" akae mguu sawa,Maana hao Vifaranga "Kuchi" wakikua tu wataanza na yeye!

"Bundi" mwana nuksi na balaa mwenye "usiku" wake anaangalia kwa mbaali!
 
Back
Top Bottom