Siasa Mchezo Mchafu

Kasheshe

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2007
Posts
4,694
Reaction score
790
Eti Mrema amepata vijana wa kumrithi? swali amemfundisha nani, kuna mtu yeyote anayeweza kusimama hadharani kwamba amemjenga?

Zaidi ya kuona wenzao wa CHADEMA wameweza!

Mrema kustaafu siasa

na Joseph Senga, Makambako

MWENYEKITI wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema, amesema anaweza kupumzika wakati wowote kujihusisha na masuala ya siasa ndani ya vyama vya upinzani na badala yake kuwa mshauri tu ndani ya vyama hivyo.

Akihutubia katika mkutano wa hadhara wa vyama vinne vya upinzani mjini hapa juzi, Mrema alijigamba kwamba, atafanya hivyo kwa kuwa amepata vijana watakaochukua nafasi yake kisiasa.

Alisema awali baadhi ya wananchi walimshauri kupumzika katika masuala hayo, lakini alishindwa kufanya hivyo kwa kuwa hakukuwa na mtu wa kumwachia kuendeleza mapambano aliyoyaanzisha ndani ya vyama vya upinzani.

“Na mimi sasa nitakuwa Kingunge wa vyama vya upinzani, kwa kuwa sasa ninao watu watakaovaa viatu vyangu. Wakati ule wapo walionifuata na kunishauri niachane na siasa eti nimezeeka, ningemwachia nani nchi hii? Ningemwachia nani mikoba yangu? Sasa yupo Zitto na Dk. Slaa, nitawakabidhi mikoba yangu yote waendeleze mapambano,” alijigamba Mrema.

Alisema, kwa kuwa CCM wanao viongozi ambao wamezeeka na sasa ni maarufu kama washauri wakuu wa chama hicho, akimtaja Kingunge Ngombare - Mwiru, hivyo na yeye angetamani siku moja kuwa mshauri wa vyama vya upinzani, akijifananisha na kigogo huyo wa CCM.

Mwenyekiti huyo wa TLP ambaye yuko katika ziara ya vyama vinne vya upinzani katika baadhi ya mikoa, alisema wabunge wa upinzani wameonyesha njia ya kufuata nyayo zake na wameonyesha umahili wa kuthubutu kuikemea serikali ya CCM kwa kile alichokiita udhalimu na ufisadi wa viongozi wa chama hicho.

Alisema, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwa kushirikiana na wabunge wengine wa vyama vya upinzani, ndio wanamfanya aone haja ya kukabidhi mikoba yake kwao, ili waendeleze mapambano ya kisiasa nchini.

Ziara za viongozi hao wa vyama vinne vya upinzani ambavyo ni CUF, CHADEMA, TLP na NCCR- Mageuzi, imekuwa ikiacha gumzo na mijadala mbalimbali katika kila mikutano inayofanywa, kutokana na sera zinazoelezwa kuwagusa wananchi wa kila rika.

Moja ya hoja iliyoibuliwa na viongozi hao ni pamoja na kuanzishwa kwa Azimio la Songea, kwa lengo la kuanzishwa uhamasishaji wa wananchi kuunga mkono vuguvugu la ukombozi na kulinda rasilimali.

Hadi sasa viongozi hao wamefanya mikutano katika mikoa saba, wakizunguka kwa kutumia helikopta, ambayo ni Mwanza, Shinyanga, Tabora, Rukwa, Mbeya, Ruvuma na leo wanatarajiwa kukamilisha ziara katika Mkoa wa Iringa kabla ya Mkoa wa Morogoro, Pwani na Dar es Salaam.
 
Kili, siasa sio mchezo mchafu, wachezaji ndo wachafu. Endapo utachezwa na watu wenye hekima na busara na wasio na uroho wa madaraka, siasa ni mchezo msafi sana wenye malengo mazuri tuu.
 
Huwa najiuliza unaweza kweli kuingia kwenye siasa na kubaki msafi? Nyanya nzuri ikiwekwa na zilizo oza si nayo itaoza? Kwa uozo uliopo sasa kwenye siasa kuna uwezekano wa kumpata kiongozi safi? Na hata akipatikana anaweza kubaki msafi? Maana hata waliokuwa wanaitwa "Mr. CLean" wakaja kugeuka na kuwa "Mr. Not So Clean". Kweli politics is a dirty game.
 
Mchezo mbaya...if you're nasty
 
Unaweza kuingia kwenye bwawa la matope na kuli safisha ukiwa ndani?

No, you can't...good analysis.

But, that means you have to get in it too!, and how can you not participate somehow, in it...
 
No, you can't...good analysis.

But, that means you have to get in it too!, and how can you not participate in it...

There is two kinds of participation. 1)from the inside 2)from the outside so which one do you mean? Like as now we are participating in politics without getting our hands "dirty".
 
Last edited:
There is two kinds of participation. 1)from the inside 2)from the outside so which one do you mean? Like as now we are participating into politics without getting our hands "dirty".

Guess, that's the right way to put it...
 
Usicheze mchezo huu wa siasa kama hujaiva vya kutosha, na kutawala hasira na tamaa binafsi
 
Unaweza kuingia kwenye bwawa la matope na kuli safisha ukiwa ndani?

Sasa bwawa utalisafisha ukiwa nje? hata kama utafanikiwa basi hiyo kazi itaku cost hasa. Dawa ni kuingia ndani na kuanza kulisafisha taratibu.

Tatizo la Tanzania sio siasa ni jamii nzima. Jamii karibu yote ni chafu ikiwa na mambo mengi sana dodgy. Bahati nzuri kwao sio rahisi hayo mambo yakajulikana mpaka wanapoingia kwenye siasa.

Mtu ambaye ni msafi na anaamini yale anayoyafanya anaweza kuingia katika nyanja yoyote ile ikiwemo siasa na bado akabaki msafi.

Tunachovuna sasa ni ubinafsi ulioachiwa kwa muda mrefu na sasa umeanza kututafuna hasa.
 
mwanasiasa mzuri ni yule anaeona upepo unavyoenda, TLP kwa sasa ni kama hakuna chama, na mrema sidhani kama yupo kwenye mood ya kuingia chama kingine hivyo anaona bora ajikalie pembeni kungoja kuitwa na kupew kanafasi kwenye chama chochote na sio yeye kuingia kwenye chama kingine,
pumzika mkuu mchango wako kwenye upinzani umeonekana tatizo ulingia wakati muda ulikuwa bado laiti yale ya 1995 yangekuwa leo na uhakika mzee wa kiraracha ungekuwa magogoni unapigwa na shombo la ferry
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…