Kasheshe
JF-Expert Member
- Jun 29, 2007
- 4,694
- 790
Eti Mrema amepata vijana wa kumrithi? swali amemfundisha nani, kuna mtu yeyote anayeweza kusimama hadharani kwamba amemjenga?
Zaidi ya kuona wenzao wa CHADEMA wameweza!
Mrema kustaafu siasa
na Joseph Senga, Makambako
MWENYEKITI wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema, amesema anaweza kupumzika wakati wowote kujihusisha na masuala ya siasa ndani ya vyama vya upinzani na badala yake kuwa mshauri tu ndani ya vyama hivyo.
Akihutubia katika mkutano wa hadhara wa vyama vinne vya upinzani mjini hapa juzi, Mrema alijigamba kwamba, atafanya hivyo kwa kuwa amepata vijana watakaochukua nafasi yake kisiasa.
Alisema awali baadhi ya wananchi walimshauri kupumzika katika masuala hayo, lakini alishindwa kufanya hivyo kwa kuwa hakukuwa na mtu wa kumwachia kuendeleza mapambano aliyoyaanzisha ndani ya vyama vya upinzani.
Na mimi sasa nitakuwa Kingunge wa vyama vya upinzani, kwa kuwa sasa ninao watu watakaovaa viatu vyangu. Wakati ule wapo walionifuata na kunishauri niachane na siasa eti nimezeeka, ningemwachia nani nchi hii? Ningemwachia nani mikoba yangu? Sasa yupo Zitto na Dk. Slaa, nitawakabidhi mikoba yangu yote waendeleze mapambano, alijigamba Mrema.
Alisema, kwa kuwa CCM wanao viongozi ambao wamezeeka na sasa ni maarufu kama washauri wakuu wa chama hicho, akimtaja Kingunge Ngombare - Mwiru, hivyo na yeye angetamani siku moja kuwa mshauri wa vyama vya upinzani, akijifananisha na kigogo huyo wa CCM.
Mwenyekiti huyo wa TLP ambaye yuko katika ziara ya vyama vinne vya upinzani katika baadhi ya mikoa, alisema wabunge wa upinzani wameonyesha njia ya kufuata nyayo zake na wameonyesha umahili wa kuthubutu kuikemea serikali ya CCM kwa kile alichokiita udhalimu na ufisadi wa viongozi wa chama hicho.
Alisema, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwa kushirikiana na wabunge wengine wa vyama vya upinzani, ndio wanamfanya aone haja ya kukabidhi mikoba yake kwao, ili waendeleze mapambano ya kisiasa nchini.
Ziara za viongozi hao wa vyama vinne vya upinzani ambavyo ni CUF, CHADEMA, TLP na NCCR- Mageuzi, imekuwa ikiacha gumzo na mijadala mbalimbali katika kila mikutano inayofanywa, kutokana na sera zinazoelezwa kuwagusa wananchi wa kila rika.
Moja ya hoja iliyoibuliwa na viongozi hao ni pamoja na kuanzishwa kwa Azimio la Songea, kwa lengo la kuanzishwa uhamasishaji wa wananchi kuunga mkono vuguvugu la ukombozi na kulinda rasilimali.
Hadi sasa viongozi hao wamefanya mikutano katika mikoa saba, wakizunguka kwa kutumia helikopta, ambayo ni Mwanza, Shinyanga, Tabora, Rukwa, Mbeya, Ruvuma na leo wanatarajiwa kukamilisha ziara katika Mkoa wa Iringa kabla ya Mkoa wa Morogoro, Pwani na Dar es Salaam.