Siasa Michezoni (Simba vs Al Ahly): Azam TV wanapaswa kuonywa, kuadhibiwa au kufungiwa!

Sioni shida yeyote. Huo ni uhuru wa maoni ambao Katiba ya nchi yetu inautambua na kwa mujibu wa United Nations Charter.

Halafu unadhani huo msomamo ni wa ajabu au mgumu kuliko wanaoandamana dunia nzima? Au wanaowaondoa mabalozi w nchi zao kupinga yanayotokeahapo middle east?
 
Una point ila ujue jana waliohusika na video production ni wao wenyewe CAF na wala sio Azam kama mnavyohisi, na ndio mana hata match utaona ilikuwa kwa quality nyingine kabisaaaaa,

Tusiwape lawama azamTv kwa kosa lisilo lao
 
Azam hana kosa.

Ukiwa unafanya live coverage kunakuwa na crew ya watu wengi kuanzia wachukua, muongoza picha, mchanganya picha n.k...

Kila shot inayotolewa kwa mtazamaji ni matokeo ya cordination ya team...

Kwenye live coverage hakuna picha inayorushwa bahati mbaya...

Na ikitokea bahati mbaya mara nyingi huwa ni zile ambazo husababishwa na tabia za characters/objects mathalani wakati shot inapigwa na ipo hewani labda watokee watu waanze kubusiana, au mtu avue nguo na kuonesha maungo n.k
 
Mabango huwa ni sehemu ya kuwakilisha ujumbe michezoni popote pale duniani apo sidhani kama Azam tv wametenda loss

Mbona urusi ilipoivamia Ukraine tuliona mabango kwenye kila viwanja vinavohusika na michezo?
Sidhani kama kitu kilichokatazwa ukikiona mwingine kakifanya ndio kimeruhusiwa.Ata uko nchi zingine hawaishi malaika kwahiyo wafanya makosa aidha kwakujua au kwakutokujua wapo.Jambo la msingi sio kutetea kwa dhana kua mbona fulani kafanya,utetezi unapaswa kujikita kwenye vifungu vya sheria.Kwahiyo ikitakuwa tumtake mtoa mada atulete kifungu cha sheria kinachokataza ili tujiridhishe nasio kusema mbona fulani anafanya.
 
Mbona mabango ya ushoga hamlalamiki? Au ndio ....
 
Ile Mechi Ilikuwa inachukuliwa na FIFA na ndo maana utaona chanel zote zilionyesha Mechi sawa na Video sawa. Kwa mfano nilikuwa Napitia RwandaTv,K24 wote

walionyesha Hiyo Mechi na Wote walionyesha hilo bango nilipata Taarifa kwamba Wachukuaji wa Mechi hiyo ni FIFA na kuwapa wengine Broadcast na ndo maana utakuta channel ya Rwana na K24 wote walikuwa na commentator sawa kutoka FIFA...

KWAHYO AZAM TV HAIHUSIKI KWA MATUKIO YYTE
 
Kwani vyombo vya bbc au cnn au france havioneshi masuala ya palestine na israel?
 
waarabu jana walikamatwa, ndio maana uliona kabisa wamerudi wanalinda goli, na walichezewa nusu uwanja muda mwingi sana, na hata takwimu za kumiliki mpira simba walikuwa juu. kama tukicheze hivihivi misri na mabeki zetu wakawa serious, tunaweza kuwapiga hata kule kwao. ni ngumu lakini hakuna lisilowezekana.
 
Huwa namshangaa sana huyo mzee na udini wake.

Mengi alikua na media lakini hakuwa na udini kama wake.
 
Mambo hayo yapo hata Ulaya, katika vita ya Ukraine na Russia tulionyeshwa baadhi ya nchi za ulaya zikionyesha kuunga mkono Ukraine kupitia matangazo ya Super sport kwenye mechi za ulaya. "Acha undumila kuwili" Dunia ndivyo ilivyo.
 
Mi ni pro-Israel lakini linapokuja suala la Azam Tv kuonyesha bango linalomsupport mpalestina sioni ukakasi wowote. Azam tv ni private enterprise, wanaweza kuonyesha chochote kinachojitokeza uwanjani hali mradi wana haki ya kurusha matangazo ya mpira uwanjani.
 
Kwa kifupi sana kwa sheria za soka za FIFA na CAF lile lilikuwa ni kosa, na kama litashikiwa bango huenda Azam TV na mamlaka za soka hapa Tanzania zikajikuta matatani.
Sio kweli mbona Mabango ya Ukraine yanawekwa live na hadi kwenye jezi sijawahi kuona timu zikifungiwa?
 
Mi ni pro-Israel lakini linapokuja suala la Azam Tv kuonyesha bango linalomsupport mpalestina sioni ukakasi wowote. Azam tv ni private enterprise, wanaweza kuonyesha chochote kinachojitokeza
Kwenye mambo mengine tunaongeza chumvi bila sababu za msingi
 
Hapa wizara husika ya michezo, wizara ya mambo ya nje na TFF wanatakiwa watoe maelezo kuhusu uwepo wa bango hilo, kwa upande wa Azam Tv wao wamejikita kwenye udini kama ilivyo kawaida yao na huenda liliandaliwa Zanzibar.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…