Queen Esther
JF-Expert Member
- Apr 5, 2012
- 2,206
- 1,464
Leo nimemuona Askofu fulani anasema hawezi kuhubiri mpaka wanakwaya waimbe, pia kikundi cha sifa na kuabudu kiimbe nyimbo za kutosha na nzuri. Pia, muimbishaji yule mwenye uwezo mkubwa afanye huduma hiyo.
Nimejaribu kuangalia siasa za CCM ambapo nyimbo za wasanii zinaimbwa nyingi zikieleza utekelezaji wa Ilani kabla mgombea hajasimama kumwaga sera akionesha tulipotoka, tulipo na tunapoelekea.
Vilevile kwa vyama vingine wanatumia sana mziki wa CD na miondoko mbalimbali kama Reggae nk. Baada ya hapo ndipo mgombea anaongea anachoongea hata kama hana sera.
Nimejaribu kuoanisha matukio haya mawili nikakumbuka hata kwenye maandiko waliobomoa kuta za Yeriko waliwatanguliza wazee wa mapambio mbele! Hongera Rais Magufuli kwani unabomoa ngome za adui zako kupitia sanaa ya uimbaji. Tangu enzi za Capt. John Komba sanaa ya uimbaji imekuwa ni sanaa ya CCM wakati wa matukio yote zikiwemo kampeni, kama kwa Maaskofu, Mitume na Manabii, Wachungaji, Mashekhe na Kaswida nk Hata mchawi anaanza na kuimba kabla ya kuloga au kuagua!!