Bwege2030
Member
- May 10, 2025
- 97
- 197
Tunapozungumzia USALITI WA KIFEDHA (Financial Infidelity) kwenye mahusiano ama ndoa, hatuamanishi kumuibia mwenza wako pesa.
Bali tunazungumxzia hali ya kutokuwa muwazi kwenye masuala ya kifedha kwa mwenza wako hasa juu ya mapato na matumizi yako ya kifedha.
Usaliti wa Kifedha unaozungumzwa hapa ni pamoja na;-
1. Kutoweka Wazi Mapato yako, Mwenza wako anajua una kazi fulani, unalipwa kiasi kadhaa, lakini kumbe kuna mahala unalipwa pesa pia kwa kutoa labda ushauri, mafunzo ama kazi nyingine. Ama kufanya kazi ukidai unalipwa kiasi fulani lakini kumbe unalipwa zaidi ya ulichotaja.
2. Kuwa na Matumizi ya Siri, Ni pale ambapo unajengea wazazi ama walezi wako nyumba ama kununua kiwanja ama kusomesha ndugu zako ama hata kuchangia michango mbalimbali lakini husemi kwa mwenzi wako, inakuwa ni siri yako.
3. Kuwekeza Kwa Siri, Unawekeza kwenye kilimo, hisa, vipande ama hatifungani kwa siri. Unajenga nyumba ya kupangisha kwa siri bila kumjulisha mwenza wako, pia nao huo ni usaliti.
4. Udanganyifu wa Bei, Umenunua gari kwa TZS 50m lakini unasema ni TZS 30m, umenunua nguo ama cheni ama saa ya gharama lakini unataja bei ya chini kwa mwenza wako. Umekata tiketi ya ndege kwenda Kigoma ama Dubai lakini husemi ukweli, unaficha bei halisi kwa mwenzako.
5. Madeni ya Siri, Mara nyingi madeni haya kama ya VICOBA, Kausha Damu, Benki hujulikana pale wadeni wanapokuja nyumbani kutaka kuuza nyumba ama kutaka kuchukua vitu vya ndani hada samani. Tabia ya kuwa na madeni ya siri asilimia kubwa kwasasa ni wanawake wanayo, wanakopa na hawasemi kwa wenza wao.
6. Akaunti ya Benki ya Siri, Kuwa na akaunti binafsi kwenye mahusiano ni muhimu lakini ni vizuri na mwenza wako akajua juu ya akaunti hiyo.
7. Kuanzisha na Kuendesha Biashara Kwa Siri, kuna watu wana biashara za siri, si mume ama mke anajua hivyo hata kinachopatikana huko hubaki siri yake mwenyewe bila mwenza kujua.
Kuna watu wana nguvu kabisa hata ya kuanzisha kwa siri biashara ama uwekezaji na mchepuko (Ex-Boyfried/Girlfriend) na mwenza wake anakuwa hajui na mwisho wa siku huishia kudhulumiwa.
Yapo mambo mengi ambayo hufanya wanandoa ama mahusiano kufa, lakini mojawapo ni hili la usaliti wa kifedha. Madhara ya kufanya haya yote ni pamoja na kupoteza mali endapo itatokea utakufa maana mkeo/mumeo na watoto ambao wana haki ya kurithi hawataweza kurithi kwasababu mali hizo zinakuwa hazijulikani kwao wala popote!