Siasa ni Kilimo na Kilimo cha Mitiki kinalipa tuache ujinga

Lituye

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
1,864
Reaction score
5,695
Wadau ni kwamba vijana tuchangamke utajiri upo lakini unahitaji mipango. Binamu yangu wiki iliyopita mwezi huu Desemba 2020 ameuza miti yake ya mitiki ambayo aliipanda sio kwa lengo la biashara na sasa anajutia kwa nini hakupanda mitiki mingi zaidi.

Wanunuzi waliifuata mpka kijijini Ndani ndani huko Morogoro kwenda kuinunua mitiki hiyo ambayo anasema haikuzidi 30 kwa bei ya elfu 60000 kila mti japo haikuwa mikubwa sana. Amenambia aliipanda miti hiyo miaka hii ya 2004 lakini sasa ameonja asali anataka kuchonga mzinga.

Jamaa baada ya kuiuza miti ile amepagawa hakujua awali kuwa ile miti ni fedha adhimu. Akaanza kujilaumu kwa nini hakupanda walau hata mitiki 1000 tuu. Hivi sasa tunawasiliana nae kutafuta mashamba kama wendawazimu tukapande miti tuachane na umaskini walau miaka 15 ijayo tufe tukiwa matajiri.

Kumbuka hivi sasa tuna miaka karibia 40yrs lakini tumejiapiza Kama Mungu aishivyo hakika tutapanda miti iwe mvua iwe jua. Aidha tufaidi sisi au wafaidi watoto wetu lakini miti ni utajiri ndugu zangu nimeshudia mwenyewe sasa.

Najua kuna wenda wazimu wengine watasoma hapa na kupuuza hao ni wajinga achana nao.Maisha utakayo kuwa nayo miaka 15 ijayo ni matokeo ya maamuzi utakayo yafanya wakati huu. Shime vijana tupange mipango ya muda mfupi na mrefu. Miti ni dhahabu unayo itengeneza mwenywe.

Maendeleo hayana vyamaa.
 
Safi mkuu ivi mitiki inakubali kwn joto tu au hadi kwene baridi mana pwani pwani nimeiona sana lkn nyanda zajuu sijaiona
 
Safi mkuu ivi mitiki inakubali kwn joto tu au hadi kwene baridi mana pwani pwani nimeiona sana lkn nyanda zajuu sijaiona
Inavyo onekana ni maeneo ya pwani inastawi vizuri zaidi.
 
Kama amepanda tangia mwaka 2004 bado atakuwa Amedhurumiwa maana mpaka kufikia 2020 huo ni mti wa miaka 15 au 16
 
aya 2035 nitakuja kusoma huu uzi tena
Tumechelewa Sana Ndugu Zangu
Tumelaliwa Sana Ndugu Zangu
Tumegongwa Sana Ndugu Zangu
Vyovyote Mtakavyosema Najua Mmenielewa
Ndiyo Ukweli Wenyewe
Nasema Uongo Ndugu Zangu
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
 
Nadhani tumekosa tu international business exposure kwa wengi wetu. Tukitahidi kutoka, kujichanganyanya na kusoma articles(channels) zinazohusu international business

Sent from my SM-G925F using JamiiForums mobile app
 
Acha kudanganya watu sio kabisa kuna mambo mengi ndani yake

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu tupe ukweli wako ili tujue ukweli tuachane na huyu muongo!

kiukweli kabisa mimi ni shuhuda wa jambo hili.
miaka ya 2010 jamaa yangu alishauriwa na mjomba wake akapande miti au alime kwenye shamba lake la urithi,kuliko shamba likikaa wazi bila kulimwa wala kipandwa.
kwasababu ya jamaa kuwa bize kusimamia kilimo hawezi akaamua kupanda miti.
kuna aina flani ya miti mirefu kwenda juu matawi yake ni madogo hupandwa sana kwenye nyumba za mijini sana(jina lake sijalijua).

alivuna mwaka juzi kama milunda(miti myembamba ya kushika zege kwenye ujenzi hasa maghorofa).
walioifata iyo miti shambani kwake walikuwa madalali.
kwa kifupi aliuza ile miti milioni 25,baada ya kuuza aliulizia kwa wenye ujuzi wa iyo miti na idadi yake wakamwambi alipunjwa.


hapo chini ni picha ya aina ya iyo miti.
 
Miashoki na milunda wapi kwa wapi mzee??

Mitiki inalipa ila inahitaji uvumilivu sana. Ni moja ya shughuli kubwa kijijini kwetu.
 
Miashoki na milunda wapi kwa wapi mzee??

Mitiki inalipa ila inahitaji uvumilivu sana. Ni moja ya shughuli kubwa kijijini kwetu.
mimi nilichoeleza ni faida tu ya kupanda miti kibiashara imma iwe ya mbao,mirunda ama iyo mitiki uliyosema.

sikubishii kwasababu kama jamaa yangu alipiga pesa kwenye miti kama iyo miashoki uliyosema inamaana kwenye mitiki kuna faida zaidi.
 
mimi nilichoeleza ni faida tu ya kupanda miti kibiashara imma iwe ya mbao,mirunda ama iyo mitiki uliyosema.

sikubishii kwasababu kama jamaa yangu alipiga pesa kwenye miti kama iyo miashoki uliyosema inamaana kwenye mitiki kuna faida zaidi.
Pamoja sana chief. Huku town tumezoea miashoki ni miti ya urembo. Sikufikiria kmaa inatumika kama milunda
 
Pamoja sana chief. Huku town tumezoea miashoki ni miti ya urembo. Sikufikiria kmaa inatumika kama milunda
hata mimi sikujua,lakini ata uyo jamaa yangu pia ukuwa na fikra izo,kuwa miashock aliyopanda inaweza siku moja kumpa faida.
Ungetoa elimu angalau kidogo kuhusu miti ya mitiki ili twende sawa.jina ili sio geni kwangu ila sijaifahamu hasa hii miti.
 
Mitiki inalipa ila inahitaji uvumilivu wa Hali ya juu wewe fikiria miaka 15...apo kuna kuisafishia na kupunguza.

Badala ya mitiki kuna zao la kokoa/kakao unavuma baada ya miaka 3 tangu kupanda Miche, kilo 1 ya cocoa kavu sh 4000 adi 5000.....kwa bei ya shamba cocoa kavu ni 2500 adi 3000 na mbichi 1800 adi 2500.

Kama kokoa italimwa vzuri na kupesa matunzo mazuri Basi kwa miaka michache (ndani ya miaka 7-8) utakuwa na pesa ndefu Sana....Zaid ya pesa utakayopata Kwenye kupanda hyo miti.
 
Wacha ujinga wewe, hiyo siyo mitiki " teak trees" hiyo ni Ashok!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…