Lituye
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 1,864
- 5,695
Wadau ni kwamba vijana tuchangamke utajiri upo lakini unahitaji mipango. Binamu yangu wiki iliyopita mwezi huu Desemba 2020 ameuza miti yake ya mitiki ambayo aliipanda sio kwa lengo la biashara na sasa anajutia kwa nini hakupanda mitiki mingi zaidi.
Wanunuzi waliifuata mpka kijijini Ndani ndani huko Morogoro kwenda kuinunua mitiki hiyo ambayo anasema haikuzidi 30 kwa bei ya elfu 60000 kila mti japo haikuwa mikubwa sana. Amenambia aliipanda miti hiyo miaka hii ya 2004 lakini sasa ameonja asali anataka kuchonga mzinga.
Jamaa baada ya kuiuza miti ile amepagawa hakujua awali kuwa ile miti ni fedha adhimu. Akaanza kujilaumu kwa nini hakupanda walau hata mitiki 1000 tuu. Hivi sasa tunawasiliana nae kutafuta mashamba kama wendawazimu tukapande miti tuachane na umaskini walau miaka 15 ijayo tufe tukiwa matajiri.
Kumbuka hivi sasa tuna miaka karibia 40yrs lakini tumejiapiza Kama Mungu aishivyo hakika tutapanda miti iwe mvua iwe jua. Aidha tufaidi sisi au wafaidi watoto wetu lakini miti ni utajiri ndugu zangu nimeshudia mwenyewe sasa.
Najua kuna wenda wazimu wengine watasoma hapa na kupuuza hao ni wajinga achana nao.Maisha utakayo kuwa nayo miaka 15 ijayo ni matokeo ya maamuzi utakayo yafanya wakati huu. Shime vijana tupange mipango ya muda mfupi na mrefu. Miti ni dhahabu unayo itengeneza mwenywe.
Maendeleo hayana vyamaa.