Siasa ni kushindana kwa hoja sio kufokeana wala kupigana wajameni

Siasa ni kushindana kwa hoja sio kufokeana wala kupigana wajameni

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Katika suala ambalo napenda kuwaasa watanzania wenzangu.

Siasa ni mchezo kama michezo mingine.

Tushindane kwa hoja sio kutishana wala kuwekeana maneno ya ugomvi.

Tujibizane kwa hoja ndio siasa.

Mimi ni kijana mdogo tu japo sijafanikiwa kuingia kwenye mfumo wa serikali. Ila natambua siasa sio vita wala kugombana wala kutishana. Bali siasa ni kutumia nguvu ya maneno kumshinda mwenzio wala sio kutishana.

Sisi wengine ni washabiki na tunaipenda sana siasa kama mchezo wa Simba na Yanga.

Tunapenda tukisikia mkijibizana kwa hoja. Maneno yenu yanatujenga na kutufurahisha sana.

Siku nikipata nafasi ya kuingia kwenye mfumo wa serikali hasa siasa nitaendelea kuupenda mchezo wa siasa kama michezo mingine na nitajitahidi kutumia maneno ya kisiasa ili niwe bora zaidi kwenye mchezo.
 
Back
Top Bottom