Gamba la Nyoka
JF-Expert Member
- May 1, 2007
- 7,036
- 9,331
Na : Twahir Kiobya (The Man)
Ni rasmi sasa Lissu anautaka uenyekiti ndani ya CHADEMA. Ametangaza nia yake kupitia vyombo vya habari na umma umesikia.
Azimio hili la Lissu ni uamuzi mzito na ni la kihistoria ktk chama cha CHADEMA. Kama Mwenyekiti wa sasa ndugu Freeman Mbowe atagombea uenyekiti, basi utakuwa ni mchuano mkali mno kuwahi kutokea katika nafasi hiyo ya uenyekiti.
SABABU ZA LISSU KUGOMBEA
1. Amezieleza mwenyewe katika mkutano wa waandishi wa habari, ikiwemo kukipa chama msukumo mpya wa kufanya siasa za kuleta mabadiliko ya kweli ya kisiasa nchini.
2. Hata hivyo naamini kuwa zipo sababu ambazo hakuzitaja wazi ikiwemo kutoridhishwa na aina ya uongozi wa mwenyekiti wa sasa katika kupambana na CCM ktk ulingo wa kisiasa nchini, ambapo ni dhahiri kuna siasa ambazo "si safi", na rafu nyingi za kisiasa chama hicho kimekumbana nazo toka 2015 na hata sasa.
3. Kupewa msukumo, na ushawishi wa wenye mitizamo kama yeye ndani na nje ya chama kuwa kaka unaweza, chukua fomu kaka tumng'oe mwamba.
4. Au inaweza kuwa ni personal understanding kati ya Mbowe na Lissu kuwa Mbowe ameamua kustaafu na anakiacha chama kwa mtu mwenye guts, haiba na uwezo wa kukipigania na kukiongoza vyema ktk changamoto mpya za kisiasa ambapo CCM imeacha kuwa chama cha kisiasa na increasingly imeonekana kutegemea zaidi vyombo vya dola!
ATHARI KWA LISSU KISIASA AKIKOSA UENYEKITI
1. Atakosa portfolio ya kiuongozi ndani ya chama, hatokuwa na cheo chochote ndani ya chama, hatokuwa mwenyekiti, makamu wala katibu mkuu. Hii itampunguzia ushawishi ndani ya chama, hatokuwa sehemu ya maamuzi ya chama, na pia itamuondolea fursa ya kuwa daraja la kisiasa baina ya wananchi na chama. Ikitokea hivi hii itakuwa ni Sherehe kubwa kwa CCM. Lissu asiye na mandate wala portfolio yenye dhamana ya chama ktk nafasi yoyote ya kiuongozi ndani ya chama ni Lissu aliyepunguzwa makali.
2. Lissu Akipigwa kwenye nafasi ya Uenyekiti, hatokuwa na political capital kubwa ya kuwa mgombea Urais kwa niaba ya chama kuliko yule atakayemshinda kwenye nafasi ya uenyekiti wa chama. Hapa pia ni bingo kwa CCM. Kwa sasa ndani ya CHADEMA hakuna mtu mwenye siasa ambazo ni zinaiumiza kichwa CCM kama Lissu. Iwapo Lissu hatokuwa mgombea urais 2025 hiyo nayo itakuwa ni sherehe kubwa sana kwa CCM.
UPI UWEZEKANO WA LISSU KUSHINDA NAFASI YA UENYEKITI?
1. Kama atachuana na Mbowe, basi nafasi ya Lissu kushinda uenyekiti ni ndogo sana. Mwenyekiti ana mizizi mirefu mno ndani ya chama, na chaguzi za nafasi mbalimbali ndani ya chama ambazo zinatoa wajumbe watakaopiga kura nafasi ya mwenyekiti inaonekana Mbowe alifanikiwa kupanga safu ambayo ni ya mrengo wake.
2. Pesa, Pesa, Pesa. Siku hizi hata ndani ya CHADEMA nako pesa imegeuka na kuwa kachumbari nzito ya kupata fursa za uongozi, Lissu hili analijua na CHADEMA nzima inajua. Yaliyotokea ktk uchaguzi wa kanda ya Nyasa hata Lissu alisema kuwa kuna pesa nyingi ajabu imemwagwa ktk uchaguzi huo. Sasa Je ni kipi kitazuia mambo hayohayo kujitokeza ktk uchaguzi wa mwenyekiti?. Ni dhahiri Lissu hana pesa ya kuhonga au kununua watu, na hizo siyo siasa zake, lakini hana ubavu wa kuzuia wengine kutumia mlungula.
3. Sidhani kama mfumo a.k.a System ya nchi inamtaka Lissu ktk nafasi hiyo ya uongozi ndani ya CHADEMA. Na hii ni kwa sababu Lissu siyo "tameable", Aliyopitia ni mazito mno kumhandle inahitaji extra care, Ana ushawishi mkubwa hata nje ya nchi, ni mjanja kupitiliza, huwezi kumtame kirahisi kwa njia za kawaida ambazo wanasiasa wengine wanakuwa easily cornered (za kisheria, kuwekwa selo etc).
ATHARI ZA KISIASA KWA MBOWE KAMA LISSU ATAGOMBEA UENYEKITI
1. Kama Mbowe atagombea uenyekiti na Lissu kisha Mbowe akashinda Itapandisha mtaji wa kisiasa wa Mbowe kwa viwango vikubwa mno. Itawadhibitishia wanachadema na CHADEMA kuwa mwenyekiti anakubalika sana ndiyo maana amelibwaga Jabali jingine la kisiasa ndani ya chama hicho.
2. Mbowe akishinda uchaguzi dhidi ya Lissu italegitimize uenyekiti wake tofauti na kama akigombea na mtu mwingine ambaye hana hadhi wala calibre ya Lissu. Kama Mbowe atagombea na mtu "mdogomdogo", ataendelea kuwa LAME DUCK chairman kama ilivyo sasa maana hawataona kama "kauearn" kwa kuthibitisha ubora wake mbele ya wengine.
3. Kama Mbowe atambwaga Lissu ktk nafasi ya Uenyekiti basi itampa Mtaji mkubwa wa kisiasa wa kuwa Mgombea urais ndani ya chama na sioni ni kwa namna gani mtu aliye na momentum kubwa ya kisiasa baada ya kushinda uenyekiti, akose kuaminiwa na chama chake kuwa mgombea urais. Sasa hapa ni sherehe na shangwe tena kwa CCM. Maana kwa CCM ni bora Mgombea urais awe Mbowe badala ya Lissu.
ATHARI KWA CHAMA.
1. Lissu na Mbowe kugombea Uenyekiti kwa upande mmoja ni jambo chanya kwa chama, linaweka precedence njema kwa watu wazito kuchuana ktk mchakato halali wa kidemokrasia, itakikomaza chama. Lakini Mbowe akishinda ni msala mzito kwa CHADEMA. Mtu ambaye CCM wanamuona ni "Mzee wa busara" huyo hafai tena kuwa mwenyekiti wa chama hicho!
2. Itakienergise chama. Sasa hivi chama kimekuwa paralysed, sababu mojawapo ni faulo nyingi walizochezewa toka 2015, lakini sababu ya pili ni kupungua kwa "chaji" kwa mwenyekiti wake. Mbowe aliyekuwa anaogopwa na CCM sasa hivi ni kipenzi cha CCM. Mbowe aliyetoka Jela huku akiwa na mtaji mkubwa mno wa kisiasa aliuza mtaji wake wa kisiasa kwa kujua au kutokujua kwa kukiingiza chama katika mazungumzo/maridhiano "kanyanga" na CCM. Kwa hiyo chama bado kina mapenzi ya wananchi, ila tu hawakiamini kuwa kina uwezo wa kusimama bila kuyumba kupambana na CCM na kuing'oa madarakani.
JE LISSU KAINGIZWA CHAKA KUGOMBEA UENYEKITI?
1. Naamini, Lissu kama akigombea na mwamba hana chance ya kumbwaga mwamba. Hivyo naamini waliomshauri kugombea uenyekiti KWA SASA wamemuingiza chaka. Na ni theory yangu kuwa baadhi ya waliomshauri wamefanya makusudi ili Kumtoa ktk safu za uongozi wa chama, maana ni tishio kwa CCM akiwa na cheo chochote ndani ya CHADEMA.
2. Kugombea kwa Lissu kunamuinua Mbowe, na hivyo kurahisisha Mbowe kuendelea kushika hatamu za chama hicho. Kitu ambacho ni furaha kwa CCM.
MBOWE NA TECHNIC YA "GRAVITATIONAL SLING SHOT MANEUVER"
Katika kusafirisha vyombo kwenda anga za juu, NASA wakati mwingine hutumia technic inayoitwa gravitational Sling shot, Yaani unatumia gravity ya sayari moja kupata nguvu ya kusukuma chombo chako kwenda kwenye sayari nyingine, hii inakurahisishia mission yako. Technique hii imetumika kurusha chombo kwenda kwenye anga la sayari ya saturn (cassini project), ambapo gravity za sayari za humo katikati zilitumika ili kukpa boost chombo. Mfano huu ni sawa na Mbowe kutumia GRAVITA/STAR power ya Lissu kureclaim nguvu yake ya kisiasa iliyopotea kwa kiwango kikubwa mno.
UPI ULIKUWA NI WAKATI MUAFAKA KWA LISSU KUGOMBEA UENYEKITI?
Naamini wakati mzuri wa Lissu kugombea uenyekiti ni pale ambapo angejihakikishia kuwa Mbowe siyo mgombea. Kwa kuwa Mbowe anahitaji Star power ya Lissu katika mchuano ili kujenga legitimacy yake, basi naamini Lissu asingempa hiyo chance safari hii. Alitakiwa amuache Mbowe apambane na pressure ya kumtaka ang'atuke. Hii pressure ni kubwa sana kwa Mbowe, na ni lazima Mbowe angeyield kwa hii pressure. Hapo ndipo ingelazimisha chama kichukue maamuzi magumu ya kutafuta mbadala wa Mbowe na bila shaka Lissu angefit kabisa na bila kutumia nguvu kubwa.
MWISHO:
Kama Mbowe anakipenda Chadema kwa dhati , inabidi aangalie, akubali kuwa siasa nchini zimebadilika sana. Chadema inahitaji mawazo mapya, nguvu mpya, msukumo mpya. Amejitahidi kukijenga chama mpaka hapa kilipofika, hana kipya zaidi kwenye kudeal na changamoto mpya za kisiasa nchini. NIMFAHAMISHE TU AKILAZIMISHA KUGOMBEA NA LISSU ATASHINDA LAKINI UENYEKITI WAKE UNAINUFAISHA ZAIDI CCM KULIKO CHADEMA.