Siasa za chuki: Tanzania tunakwama wapi?

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Vumbi la Ndugai lingali kutulia. La Polepole ndiyo hivyo tena.

Kwanini tu wazito mno kuzika tofauti zetu? Kwanini wenzetu hawa, hawana uadui wa kudumu?

IMG_20220107_155807_215.jpg

Kwamba mipira inazagaa golini kwa adui, kipa hayupo:

"Kwa ego tu hatutaki kuisukumia wavuni tuondoke na point 3 muhimu kwa sababu tu adui zetu wameibwaga na kuiacha hapo?"

Tuna nia ya ushindi kweli?

Ama kweli kwenye miti hakuna wajenzi.

Yule bwana si aliimba ya kwamba:

"... Hata kama hunipendi, bora kujidanganya, roho itulie."🎼🎼

________

Ndugai: Ndoto ya Mihimili huru rasmi Imeyeyuka
 
Kumtakia mtu happy birthday ndo kuzika tofauti zao?
Wewe kweli mungiki.
Hao Wana chuki mbaya na damu itakuja kumwagika kenya
 
Kwa hiyo kwetu ambako haya:

IMG_20211225_085219_327.jpg

si sinema wewe unaona damu haimwagiki?

Kweli wewe ni Goodluck kama si wenzake kabisa.
 
Hawa angalau kuna baadhi ya stage walizipitia, Katiba waliyonayo ni bora kuzidi ya kwetu, na mentality ya kiongozi wao inatoa fursa kwa wanasiasa wengine kujitahidi kuondoa tofauti zao, ndio maana aliwahi kutushangaa sisi na siasa zetu za visasi wakati fulani.
 
Kutaka kuleta mabadiliko au hata kuchukua nchi "solo" au "rigidly" tutafika tukiwa tumechoka na hata kudhoofu kweli kweli.
 
2025 unaweza kuwa mwaka mgumu sana kwa Tz ktk uchaguz wa viongoz kulko mwaka wowote ule,

Sababu kuu inaweza kuwa mgawanyiko wa ccm na kuunda timu mbili ndani ya chama kimoja, huku wapinzan nao wakiwa hawaeleweki maana mpka kufika miaka hiyo watakuwa wamevulugwa kabisa na kupoteza ushawishi kwa wananchi, sababu hawakujijengea tabia ya kupambania maono yao, zaid zaid wako bize kujadili hotuba za samia na kumnanga jobu ndugai,

Tutegemee mipasuko zaid,pia tutegemee usariti kuongezeka, na mambo mengi ya hovyo kufichuka.

Siasa ni takataka
 
CCM watajuta kuua upinzani.

Vita ya ndani ni ngumu sana na huwa haiishi. Kuna fukuto kubwa ndani ya CCM. Ni suala la muda tu.

Sisi tusio wanachama wa chama chochote, tuzidi kumwomba Mungu. Nina wasiwasi huenda hata sio wanasiasa watakao chukua utawala 2025
 
2025 unaweza kuwa mwaka mgumu sana kwa Tz ktk uchaguz wa viongoz kulko mwaka wowote ule,

Sababu kuu inaweza kuwa mgawanyiko wa ccm na kuunda timu mbili ndani ya chama kimoja, huku wapinzan nao wakiwa hawaeleweki maana mpka kufika miaka hiyo watakuwa wamevulugwa kabisa na kupoteza ushawishi kwa wananchi, sababu hawakujijengea tabia ya kupambania maono yao, zaid zaid wako bize kujadili hotuba za samia na kumnanga jobu ndugai,

Tutegemee mipasuko zaid,pia tutegemee usariti kuongezeka, na mambo mengi ya hovyo kufichuka.

Siasa ni takataka

Yawezekana tuna elimu duni sana ya uraia.

Matokeo yake ni kuwa hata tunavyovitaka hatujui namna ya kuvipata.

"Ushabiki unakuwaje sehemu ya kutegemewa kwenye kuleta matokeo yenye tija kisiasa?"

Kila sakata huvutia lundo la watazamaji wachekelee yakimkuta au wamzomee mmoja kwenye minyukano:

Sakata la Ndugai: Mashabiki wako mkao wa Kula

Si kwa Mwingira, Shoo, Polepole, Ndugau, au mzee wa upako mwendo ni kila mchuma janga kula na wakwao.

Vyama vya siasa haviwezi kujivua lawama hapa:

CHADEMA: Kujipanga kwa Ukombozi hakuna Ukomo

Pole Tanzania.
 
CCM watajuta kuua upinzani.

Vita ya ndani ni ngumu sana na huwa haiishi.Kuna fukuto kubwa ndani ya CCM.Ni suala la muda tu.
Sisi tusio wanachama wa chama chochote,tuzidi kumwomba Mungu.Nina wasiwasi huenda hata sio wanasiasa watakao chukua utawala 2025

Yawezekana vyama vya upinzani havina strategists mahiri wa kuviongoza kwenye reli ya kutufikisha nyumbani.

Tumeshindwa hata ku rally support Spika kutokufukuzwa. Mwisho rahisi wa yote ulikuwa hapa.

Kumchukia Ndugai kama binadamu ilikuwa na nini cha kufanya kuizuia hii nchi kupata mwanzo mpya?

Ndugai: Ndoto ya Mihimili huru rasmi Imeyeyuka

My goodness!
 
2025 unaweza kuwa mwaka mgumu sana kwa Tz ktk uchaguz wa viongoz kulko mwaka wowote ule,

Sababu kuu inaweza kuwa mgawanyiko wa ccm na kuunda timu mbili ndani ya chama kimoja, huku wapinzan nao wakiwa hawaeleweki maana mpka kufika miaka hiyo watakuwa wamevulugwa kabisa na kupoteza ushawishi kwa wananchi, sababu hawakujijengea tabia ya kupambania maono yao, zaid zaid wako bize kujadili hotuba za samia na kumnanga jobu ndugai,

Tutegemee mipasuko zaid,pia tutegemee usariti kuongezeka, na mambo mengi ya hovyo kufichuka.

Siasa ni takataka
Amini nakwambia mkuu uchaguzi wa 2025 utakuwa mgumu kwa upande wa CCM tu na upinzani unaweza ukawa na nguvu kama uchaguzi wa 2010 mark my word.
Mgawanyiko ndani ya CCM sasa ni dhahiri na unaendelea kukua kadri tunavyoelekea uchaguzi mkuu ujao. Upinzani lazima utashika kasi kipindi hiki kwasababu miaka 6 iliyopita ni ulikuwa umefungiwa kwenye chupa ya chai na sasa wamepata uwanja wa kupractise kwa nguvu.
 
Yawezekana vyama vya upinzani havina strategists mahiri wa kuviongoza kwenye reli ya kutufikisha nyumbani.

Tumeshindwa hata ku rally support Spika kutokufukuzwa. Mwisho rahisi wa yote ulikuwa hapa.

Kumchukia Ndugai kama binadamu ilikuwa na nini cha kufanya kuizuia hii nchi kupata mwanzo mpya?

Ndugai: Ndoto ya Mihimili huru rasmi Imeyeyuka

My goodness!
Mkuu tafadhali usipotoshe. Ndugai hajafukuzwa bali amejiuzulu, kujiuzulu ni utashi wa mtu binafsi iwe amelazimishwa au hajalazimishwa tunachoangalia ni personal assent. Je ulitaka upinzani imlazimishe asijiuzulu wakati ni takwa lake binafsi baada ya kutofautiana na mhimili mwingine?
Kama anajua na anaamini kuwa bunge ni mhimili unaojitegemea na kazi yake ni kutunga sheria na kuisimamia serikali basi angesimamia katika maneno yake yaliyozaa hiyo hali. Katika hili upinzani usiushirikishe
 
Vumbi la Ndugai lingali kutulia. La Polepole ndiyo hivyo tena.

Kwanini tu wazito mno kuzika tofauti zetu? Kwanini wenzetu hawa, hawana uadui wa kudumu?

View attachment 2072123

Kwamba mipira inazagaa golini kwa adui, kipa hayupo:

"Kwa ego tu hatutaki kuisukumia wavuni tuondoke na point 3 muhimu kwa sababu tu adui zetu wameibwaga na kuiacha hapo?"

Tuna nia ya ushindi kweli?

Ama kweli kwenye miti hakuna wajenzi.

Yule bwana si aliimba ya kwamba:

"... Hata kama hunipendi, bora kujidanganya, roho itulie."🎼🎼

________

Ndugai: Ndoto ya Mihimili huru rasmi Imeyeyuka
Ni kwa sababu Wana ajenda za kudumu,
Sasa watz katiba ambayo ingetuungamisha, maccm hawaitaki,. Au wanaogopa kuitaka
 
Mkuu tafadhali usipotoshe. Ndugai hajafukuzwa bali amejiuzulu, kujiuzulu ni utashi wa mtu binafsi iwe amelazimishwa au hajalazimishwa tunachoangalia ni personal assent. Je ulitaka upinzani imlazimishe asijiuzulu wakati ni takwa lake binafsi baada ya kutofautiana na mhimili mwingine?
Kama anajua na anaamini kuwa bunge ni mhimili unaojitegemea na kazi yake ni kutunga sheria na kuisimamia serikali basi angesimamia katika maneno yake yaliyozaa hiyo hali. Katika hili upinzani usiushirikishe

Kwani mwenye macho anaambiwa tazama?

Kujiuzulu kwa Ndugai: Hongereni CHADEMA na NCCR japo haikutosha

Nini nilitaka au nini ningependa?

Sakata la Ndugai: Mashabiki wako mkao wa Kula

Upinzani nisiushirikishe?

Tafadhali heshimu mawazo ya wengine hata kama hupendi kuyasikia.

Ndiyo demokrasia hiyo.
 
Amini nakwambia mkuu uchaguzi wa 2025 utakuwa mgumu kwa upande wa CCM tu na upinzani unaweza ukawa na nguvu kama uchaguzi wa 2010 mark my word.
Mgawanyiko ndani ya CCM sasa ni dhahiri na unaendelea kukua kadri tunavyoelekea uchaguzi mkuu ujao. Upinzani lazima utashika kasi kipindi hiki kwasababu miaka 6 iliyopita ni ulikuwa umefungiwa kwenye chupa ya chai na sasa wamepata uwanja wa kupractise kwa nguvu.

Unamjua Lowasaa na nguvu yake ilivyokuwa ndani ya CCM na CCM ikapenye safely....

Nitajie mtu mmoja mwenye miguvu hata nusu ya Lowassa ambaye sasa yuko ndani ya chama na anaweza kukimegua chama..

CCM wataparuana lakini linapofika kwenye issue ya wao kuongoza dola na kushinda uchaguzi basi watakuwa kitu kimoja kwa namna yeyote washinde..

Upinzani usitegemee kuchukua dola kwa kusubiri CCM ife au isambaratike, wapange mikakati yao kuwin mass support ambayo itakuwa very royal in any case na kuweza kuchukua dola hata kwa kuingia barabarani..
 
Jambo la kheri kama itakuwa hivyo. Bila shaka kama ndivyo, haitakuwa kwa kudra za Mola pekee:

Uanaharakati ndiyo njia pekee ya kuipata katiba ya wananchi

Huo ndiyo ulio ukweli mchungu.
 
Unamjua Lowasaa na nguvu yake ilivyokuwa ndani ya CCM na CCM ikapenye safely....

Nitajie mtu mmoja mwenye miguvu hata nusu ya Lowassa ambaye sasa yuko ndani ya chama na anaweza kukimegua chama..

CCM wataparuana lakini linapofika kwenye issue ya wao kuongoza dola na kushinda uchaguzi basi watakuwa kitu kimoja kwa namna yeyote washinde..

Upinzani usitegemee kuchukua dola kwa kusubiri CCM ife au isambaratike, wapange mikakati yao kuwin mass support ambayo itakuwa very royal in any case na kuweza kuchukua dola hata kwa kuingia barabarani..

Hii ngoma iko wazi:
IMG_20220110_071335_038.jpg

Huo ndiyo ulio ukweli mchungu.
 
NInakazia Kwenye kujitathmini wapo kina Ngongo wengi wakijiaminisha wao ni wao tu.

Disgrace.
 
Back
Top Bottom