Siasa za dunia hii; Tusaidiane kidogo hapa wapendwa

Pejokiss

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2011
Posts
248
Reaction score
187
Habari za wakati huu wapendwa!

Binafsi nashangazwa sana na mambo yanayoendelea ulimwenguni. Tangu utotoni tumefundishwa na dini zetu kuhusu upendo na pia kuonywa juu ya siku za mwisho. Lakini kwa upande mwingine, inaonekana kama watu wenye nguvu, wanasiasa na mataifa makubwa hawaguswi kabisa na mafundisho hayo, wala hawaogopi matokeo yake.

Mwezi Oktoba juzi kulitokea mauaji hapa nchini ambayo yalilalamikiwa na wengi, na baadhi wakataja jumuiya ya kimataifa kama sehemu ya kutafuta haki. Hata hivyo, ukiangalia yanayoendelea katika maeneo kama Gaza, Ukraine na sasa Iran, utaona pia mauaji makubwa yakifanyika huku dunia ikiwa kimya. Maelfu ya watu wanapoteza maisha, lakini inaonekana kama hakuna anayejali. Kwa nini hali iko hivyo?

Kuna watu wanaolaani mauaji yanayotokea hapa nyumbani, lakini wakati huo huo mioyoni mwao wanaunga mkono mataifa kama Marekani na Israel katika vita vinavyoendelea sehemu nyingine. Je, hilo ni sawa? Na hizi dini tulizofundishwa kuhusu upendo tangu utotoni—je, mafundisho yake yanawahusu Waafrika pekee? Kwa sababu hata yanayoendelea Congo na maeneo mengine kama Sudan yanaonyesha kuwa mara nyingi maslahi ya binadamu yanawekwa mbele kuliko thamani ya maisha.

Wengine hata wanatajirika kupitia viwanda vya silaha wanazouza ili watu wengine waendelee kuuana. Kwa kweli mambo haya yanachanganya sana. Hii hali inaelewekaje wadau?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…