Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 524
- 829
Siasa za figisu ndani ya Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania, UWT, Mkoa wa Mbeya, zimetajwa kuwa miongoni mwa mambo yanayokwamisha na kuchelewesha utekelezaji wa baadhi ya miradi yenye lengo la kuwainua wanawake kiuchumi kutokana na viongozi wa jumuiya hiyo na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ujumla ndani ya Mkoa huo kulinda maslahi ya mtu mmoja.
Inadaiwa kuwa mwaka 2023, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Mhe. Suma fyandomo, alinunua mashine za kusaga na kukoboa nafaka kwa ajili ya kuwekwa katika kila wilaya za Mkoa wa Mbeya, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi.
Hata hivyo, licha ya mashine hizo kufikishwa wilaya zote zimeshindwa kufungwa na kuanza kutumika kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni figisu ndani ya jumuiya hiyo.
Miongoni mwa mashine hizo ni moja iliyokuwa imepelekwa katika Wilaya ya Chunya na wilaya ya kyela,pia hazikufungwa kama wilaya nyingine na ili ziweze kuanza kutoa huduma kwa wananchi, inadaiwa zilihifadhiwa katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi katika wilaya hizo na mashine ziliteketea kwa moto wakati wa vurugu zilizotokea katika kipindi cha uchaguzi wa 29 october 2025.
Na mashine hizo zilinunuliwa zikiwa na vifaa vyote ili kuwezeshwa kufungwa tu zikifika mahali husika na sasa baadhi ya vifaa wanadai vimepotea ,ikiwemo wilaya ya Rungwe ambapo mbunge huyo alilazimika kununua vifaa vingine ili mashine zifungwe kinguvu na ikazinduliwa na Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa (MNEC ) Bi.Hellen Mbogowe pia kwa vita mana uongozi haukutaka izinduliwe na kiongozi huyo.
Mwenyekiti wa UWT Taifa Mh.Marry Chatanda anapaswa kuunda tume maalumu ya kuchunguza mwenendo wa siasa ndani ya UWT mkoa wa Mbeya