Siasa za msikiti Uingereza

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Nimeishi Uingereza kwenye mji mmoja unaitwa Cardiff ambao ni mji mdogo ulioko Wales na kwa kawaida kwa Waingereza watu wa Wales wanadharaulika wanaonekana washamba.

Neil Kinnock alipata kugombea kutaka kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza na yeye ni Mwelshi.

Siku moja kaingia mwalimu wetu mmoja yeye ni kutoka England anaitwa Brown Thomas akamsema kwa ubaya sana Kinnock, ‘’Ati na huyu nae anataka kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza. Nani atampigia kura Mwelish?’’

Kwa sababu hii na dharau hii mimi nilipokwenda kupiga kura nilimpigia Neil Kinnock wa Labour Party lakini hakushinda aliyeshinda alikuwa John Major wa Conservative.

Najua msomaji wangu unashangaa vipi huyu mtu kutoka Kariakoo apige kura Uingereza?

Naam nimepiga kura. Uingereza sheria yao ni kuwa ukiwa ni mlipaji kodi haijaslishi kama ni mwananchi au mgeni unaweza kupiga kura.

Mbunge wangu mgombea alinifata nyumbani kwangu Column Road kwa adabu zote kuomba kura yangu.

Msikiti wa mtaani kwangu ni jengo ambalo hapo zamani lilikuwa kanisa lakini kwa kuwa watu walikuwa hawaendi kuabudu Wakristo wa sehemu ile wakaamua kuliweka gazetini kutangaza kuuza kanisa lao.

Hapo wakatokea Waislam wakalinunua kanisa lile na kuligeuza kuwa msikiti.

Hivi ndivyo ilivyotokea kwa msikiti huu Darul Isra kuwa katikati ya makazi ambayo wengi wa wakazi ni Wakristo.

Kwa muda wote nilioishi eneo lile sikupata kuhisi uadui wowote kutoka kwa hawa Waingereza kuwa walikuwa na chuki na msikiti ule.

Tatizo lilikuwa moja tu.

Barabara ya kuingia msikitini ilikuwa inakataza kuegesha magari kwa sababu ya ufinyu wa barabara.

Siku ya Ijumaa wanafunzi wengi wanakuja msikitini kwa ajili ya sala ya Ijumaa na baadhi yao ni vijana wanafunzi kutoka ncbi za Kiarabu ni wanafunzi lakini wana magari mazuri tu na lazima waje na magari yao na watayaegesha hapa mtaani na trafiki watakuja na kuweka tiketi.

Hawajali fedha wanazo wanalipa faini.

Ikatokea baada ya kurudi Tanzania nilirudi tena Cardiff nikitokea London na nikaenda Darul Isra msikitini kwangu kwa zaamani.

Safari hii nikapewa habari nyingine ya kufurahisha kuwa msikiti ule umenunua kanisa lingine na kuna mpango wa kulikarabati kuligeuza msikiti lakini kwa wakati ule lile kanisa wakilitumia kama bohari ya kuwekea vitu.

Nimekwenda Tilbury Port huu ni mji nje ya London na ni bandari.

Siku za nyuma bandari hii ilikuwa na biashara kubwa lakini wakati wa Magret Thatcher uchumi ulibadilika na bandari hii ikapoteza umuhimu wake.

Wengi wa wakazi wa mji ule mdogo walikuwa wafanyakazi wa bandari na baada ya bandari kukosa biashara na kazi kuwa haba wafanyakazi wengi walipoteza ajira kwa hiyo wakahama mji.

Niliingia Tilbury mchana kwa treni.

Nilipata mshtuko mkubwa sana.

Mji mzima hakuna mtu anaeonekana barabarani wala gari kupita.

Maduka ya mtaa mzima mkubwa wenyewe wanaita ‘’High Street,’’ yamefungwa lakini matangazo yapo yakitangaza biashara tofauti.

Unatembea barabarani unasikia sauti ya kiatu chako kinapogonga lami ya barabara.
Tilbury ni ‘’ghost town,’’ mji uliohamwa na katika masiaha yangu yote sijapatapo kuona kitu kama hiki.

Inabidi wenyeji waliobakia wakuelekeze mahali ambapo unaweza kwenda kula chakula sehemu inaitwa Stella Maris, hii ni mfano wa huku kwetu wa Mission to Seaman sehemu ambayo zimewekwa maalum kwa kuwahudumia mabaharia kwa malazi na chakula.

Eid Kubwa imenikuta katika mji huu na hakuna msikiti lakini nimefahamishwa kuwa Waislam wapo ingawa hawana msikiti.

Wenyeji wakanieleza kuwa katikati ya mji kuna shule ya msingi ambayo hapo ndiyo Sala ya Eid huswaliwa ndani ya darasa.

Hapo ndipo niliposwali Sala ya Eid na wengi wa Waislam walikuwa Wahindi.

Miaka mingi ikapita siku moja nikajikuta niko Maryland, Washington DC Amerika na Ijumaa imefika.
Mwenyeji wangu Dr. Harith Ghassany akanichukua twende kusali.

Haikunipitikia kuwa sehemu ile hakuna msikiti na hivyo ndivyo ilivyokuwa.
Hapakuwa na msikiti.

Dr. Ghassany alinichukua John Hopkins University na tuliswali ndani ya moja ya madarasa ya chuo hicho.

Tanzania nchi ambayo Waislam ni umma mkubwa kuna chuki dhidi ya Uislam kupelekea kuvunjwa misikiti...

Swali la kujiuliza ni nchi yetu nani kaifikisha hapa?
Nini chanzo cha uadui huu?
 
Ina Lillah Waina Illah Rajioun
Ni msiba mkubwa huu
Sent from my SM using Tapatalk
 
Niliwahi kumtembelea rafikiangu ZAF-Lusaka, nilishanga waislamu hakuna lakini muda wa swala ukifika unaswali mle ndani na hakuna anaekubughudhi. Nashanga eti mtaalamu mmoja kaamua kuvunja msikiti eneo lenye maelfu ya waislamu sijui katumwa na nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ina Lillah Waina Illah Rajioun
Ni msiba mkubwa huu
Sent from my SM using Tapatalk
Black Sniper,
Mimi hukaa nikajiuliza ni kitu gani kimepelekea hadi leo nchi ikakumbwa na hii hasama
na uadui ilhali historia yetu huko tulikotoka wazee wetu walisimika misingi imara ya umoja
na udugu?
 
Inafikirisha Sana Mada yako!

Allah akubaarik
Pahamba,
Mimi najiuliza ni kitu gani kimepita kuweza kuwa na nguvu ya kuvunja umoja
uliojengwa na wazee wetu wakati wa kudai uhuru?



Hii ndiyo historia yetu ya mapenzi baina yetu. Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere
yuko katikati ya Waislam waliomkaribisha Dar es Salaam 1952 wakamchagua kuwa
kiongozi wa TAA 1953, 1954 wakaunda TANU Nyerere akiwa rais na 1955 wakamfungia
safari ya UNO. Huu uadui na kuwanyanyapaa na kuwabagua Waislam nini chimbuko lake
na imesababishwa na nini na nani muhusika? Kuna mtu anaeweza kutoa majibu?



Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere akiwa kashikwa mkono na
Mzee Mshume Kiyate kulia na kushoto kashikwa na Mzee Max
Mbwana na Mwinjuma Mwinyikambi. Mwalimu Nyerere kazungukwa
na Waislam. Udugu na mshikamano huu umepoteaje? Je, kulikuwa
na watu waliokuwa hawafurahishwi na umoja huu? Ni nani hawa?
Picha hii ni Uchaguzi Mkuu 1962.



Hawa akina mama wa Kiislam ndiyo walikuwa wanachama wa mwanzo wa TANU
1954. Kulia ni Bi. Tatu bint Mzee akifuatiwa na Bi. Titi Mohamed. Kushoto wa kwanza
ni Bi. Chiku bint Said Kisusa (mke wa Shariff Attas) wakimsindikiza Mwalimu Nyerere
Uwanja wa ndege safari ya kwanza UNO 1955..




Kulia Haruna Taratibu, Saadan Abdu Kandoro, Julius Kambarage Nyerere,
Sheikh Mohamed Ramia na Idd Faiz Mafungo Dodoma 1955. Idd Faizi ndiye
aliaminiwa na kukusanya fedha za safari ya Mwalimu Nyerere UNO.



Idd Faiz huyo hapo aliyevaa kanzu, koti na tarbush kulia kwa Nyerere akinsindikiza
safari ya UNO 1955.

Ndugu zanguni hivi nani katuvurugia historia hii?
Kuna mtu ana majibu ya maswali haya?
 
Black Sniper,
Mimi hukaa nikajiuliza ni kitu gani kimepelekea hadi leo nchi ikakumbwa na hii hasama
na uadui ilhali historia yetu huko tulikotoka wazee wetu walisimika misingi imara ya umoja
na udugu?
Nimeshangaa sana kuhusu hiyo habari ya kuvunjwa msikiti
Haijawahi kutokea chokochoko kama hizi maisha yote
Haya huwa tunayasikia kwa wenzetu tu lakini kama na kwetu yameanza basi tumuombe Mungu sana.

Tumeishi kwa upendo miaka yote lakini sasa naona kuna chuki zimeanza na sijui hatima yake kama sio ubaya

Sent from my SM using Tapatalk
 
Black...
Hatujapata kuishi kwa upendo.
Yaelekea huijui historia ya nchi yetu.oma

Umesoma kitabu cha Abdul Sykes?
 
Kuna Waislamu wanaojitambua na ambao hawajitambui.

Kwa hapa Tz kwenye huo msikiti ulioupoint kulikuwa kuna tatizo ndio maana ukavunjwa
 
Black...
Hatujapata kuishi kwa upendo.
Yaelekea huijui historia ya nchi yetu.oma

Umesoma kitabu cha Abdul Sykes?
Hapana kaka mkubwa sijasoma ila nimefuatilia sana nyuzi zako humu na kuzisoma.
Kuishi kwa upendo najua ina maana kubwa sana
Lakini hatujawahi kupigana au kuuwana kwa udini mzee
Ingawa naona yajayo

Sent from my SM using Tapatalk
 
UDOM. Una swali lingine?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ahaaa sasa ishu ya UDOM. Wanachotaka ni kujenga msikiti ndani ya eneo la chuo.
Uongozi wa chuo ulishawahi kukataa kabisa dini yoyote kujenga nyumba za ibada katika eneo la chuo.

Instead chuo walitenga halls maalum kwa ajili ya waislam kuswalia na dini zingine.
Ndio utaratib ambao umekuwepo kwa muda mrefu sasa.
Na halls za waislam haziguswi au kutumika na dini nyingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania nchi ambayo Waislam ni umma mkubwa kuna chuki dhidi ya Uislam kupelekea kuvunjwa misikiti...

Swali la kujiuliza ni nchi yetu nani kaifikisha hapa?
Nini chanzo cha uadui huu?
Waislamu mna uwezo finyu sana wa kufikiri, Mnalalama kama mtoto wa kambo, Mnaikumbatia tamaduni ya kigeni (Uislamu) Kuliko utu au ubinadamu, Waislamu hamuaminiki, waislamu ni Magaidi, watu ambao hawana utu, Watu ambao huwezi kuwa na amani kuishi nao, watu wanaoonesha ubaguzi wa kidini wazi wazi! "Waislamu", Achana na tukio tu la Dodoma, Kuna haja ya waislamu kubomolewa Misikiti yao yote..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…