Khan,
Umeandika kwa hasira nyingi sana.
Ndipo ninapouliza hizi chuki nini sababu na chanzo cheke.
Historia ya udugu iliyowekwa na wazee wetu ni nani kaifuta?
WAISLAM WALIKUWA NA MAPENZI MAKUBWA NA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE
Hii ndiyo historia yetu ya mapenzi baina yetu. Baba wa Taifa yuko katikati ya Waislam waliomkaribisha Dar es Salaam 1952 wakamchagua kuwa kiongozi wa TAA 1953, 1954 wakaunda TANU Nyerere akiwa rais na 1955 wakamfungia safari ya UNO. Huu uadui na kuwanyanyapaa na kuwabagua Waislam nini chimbuko lake na imesababishwa na nini na nani muhusika? Kuna mtu anaeweza kutoa majibu?
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere akiwa kashikwa mkono na Mzee Mshume Kiyate kulia na kushoto kashikwa na Mzee Max Mbwana na Mwinjuma Mwinyikambi. Mwalimu Nyerere kazungukwa na Waislam. Udugu na mshikamano huu umepoteaje? Je, kulikuwa na watu waliokuwa hawafurahishwi na umoja huu? Ni nani hawa? Picha hii ni Uchaguzi Mkuu 1962.
Hawa akina mama wa Kiislam ndiyo walikuwa wanachama wa mwanzo wa TANU 1954. Kulia ni Bi. Tatu bint Mzee akifuatiwa na Bi. Titi Mohamed. Kushoto wa kwanza ni Bi. Chiku bint Said Kisusa (mke wa Shariff Attas) wakimsindikiza Mwalimu Nyerere Uwanja wa ndege safari ya kwanza UNO 1955.
Idd Faiz huyo hapo aliyevaa kanzu, koti na tarbush kulia kwa Nyerere akimsindikiza safari ya UNO 1955.
Kushoto Idd Faiz Mafungo, Sheikh Mohamed Ramiya, Saadan Abdu
Kandoro na Haruna Taratibu, Dodoma 1955. Huyu Idd Faiz ndiye
aliyekuwa mkusanyaji fedha za safari ya Mwalimu Nyerere UNO 1955
ni huyo hapo chini kulia kwa Mwalimu Nyerere alyevaa kanzu, koti na
tarbush.
View attachment 997514