Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Ukifuatilia siasa za upinzani za nchi hii utaona NCCR Mageuzi ilianza kama chama mahiri cha upinzani Tanzania kikapotea katika ramani kisha CUF ikafuatia kama chama kikuu cha upinzani nacho kikapotea katika ramani ikafuatia CHADEMA ambayo imekuwa chama kikuu cha upinzani kwa karibia miaka 15 sasa.
Inavyoonekana ni kwamba endapo CHADEMA itafifia kipindi hiki hakuna chama mbadala cha siasa cha upinzani kwa sasa kuchukua nafasi yake.
Wanachama na wapenzi wake wengi wana machaguo makubwa matatu ambayo ni kubaki CHADEMA kupambania ndani kwa ndani, kwenda CCM au kuachana na siasa kabisa.