Siasa za 'upopo' zinaiua sana Tanzania kiuchumi na kijamii

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Chama cha siasa kinachoongoza nchi kinajiita cha kijamaa wakati chenyewe kinaendesha nchi kibepari.

Kuna watu wanajifanya ni wapinzani lakini kutwa kucha wako bize kuisifia CCM.

Kuna watu ni wasomi lakini matendo yao ni kama hawajasoma kabisa. (Kabudi style)

Kuna watu wanasajili Kampuni (Kalynda) lakini wanasema hawajui ilikuwa inafanya shughuli gani?

Yaani Tanzania huwezi kuujua msimamo wa mtu maana anachokipinga ndicho anachokifanya na anachokifanya ndicho anachokipinga.
 
Tanzania bado haijaingia mfumo wa vyama vingi. Tuna kiinimacho kinachoendelea kujaribu kuaminisha hivyo.
Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa ni mahsusi kwa ajili ya kuhakikisha tuna vyama vya upinzani kwa jina tu
 
Chama cha siasa kinachoongoza nchi kinajiita cha kijamaa wakati chenyewe kinaendesha nchi kibepari.
Sio chama, bali ni nchi, Tanzania ni nchi moja inayofuata siasa ya ujamaa na kujitegemea yenye misingi minne, watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora wa CCM.
Kuna watu wanajifanya ni wapinzani lakini kutwa kucha wako bize kuisifia CCM.
Kazi ya upinzani sio kupinga kila kitu bali kuonyesha utofauti yaani altenative. Japo Kazi ya Upinzani ni Kupinga, Lakini Sio Kupinga Kila Kitu, Kwenye Maslahi Ya Taifa, Tutangulize Utaifa, Tuwe Wamoja, Wakweli na Tusipotoshe.
Kuna watu ni wasomi lakini matendo yao ni kama hawajasoma kabisa. (Kabudi style)
Na kuna watu hawajasoma, lakini hoja zao ni kuwazidi maprofesa, ,(Msukuma, Kibajaji) Livingstone Lusinde, japo ni darasa la saba tuu, ni kichwa mbaya!, ana uwezo mkubwa na pia ana powers fulani!.
P
 
Chanzo cha yote hayo ni njaa, wengi wanaingia kwenye siasa wakiwa hawana miradi yoyote ya kuwaletea maendeleo, matokeo yake wanajikuta wakiwa siasani wanayumba kimsimamo ili kuendana na upepo wa kuwaletea kipato.

Boss akienda kushoto, nao huenda nao, akigeukia kulia, nao hugeuka nae.
 
njaa zinatutesa mwana wane 😅
 
Yaani Tanzania huwezi kuujua msimamo wa mtu maana anachokipinga ndicho anachokifanya na anachokifanya ndicho anachokipinga.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hivi Azimio la Zanzibar si ndio lililofuta siasa ya Kijamaa hapa kwenye Jamhuri?
 
Chanzo cha yote hayo ni njaa, wengi wanaingia kwenye siasa wakiwa hawana miradi yoyote ya kuwaletea maendeleo, matokeo yake wanajikuta wakiwa siasani wanayumba kimsimamo ili kuendana na upepo wa kuwaletea kipato.

Boss akienda kushoto, nao huenda nao, akigeukia kulia, nao hugeuka nae.
Akina Bulembo
 
Back
Top Bottom