WilsonKaisary
JF-Expert Member
- Apr 4, 2017
- 392
- 949
Siasa za ushabiki, Siasa zisizo za uzalendo.
Hii nchi ni takribani zaidi ya miaka 45 toka ipate Uhuru, ni nchi yenye rasilimali na utajiri wa karibu kila aina. Lakini Cha kushangaza hata uchumi wa Kati hatujafikia.
Na mpaka hatutaki kuvumbua shida nini inayotukwamisha tusifikie hata uchumi wa kati.
Tukisema tufanye takwimu japo ya nusu watanzania, tuhoji ni wangapi wenye uelewa kwa nini mpaka Sasa uchumi wetu unadolola japo kwa utajiri wa asili tulionao?
Naamini wengi watashindwa kuzungumza ukweli, tokana na ushabiki wa kisiasa yani ushabiki vyama vya Siasa.
Ila tunashindwa tambua kuwa aina ya siasa tunazo fanya Ndio kikwazo kikubwa katika taifa hili.
Mifumo ya siasa nchini ni kikwazo kikuu. Kama mwanasiasa hawezi shurutishwa hata kwa kosa la ufisadi au rushwa, halafu yeye ndie mfanya maamuzi ya walio wengi msitegemee maendeleo ya kiuchumi.
Ni Sawa leo tunasema JPM ndie mwanakondoo wa kutupeleka kwenye uchumi wa Kati, Lakini mwanakondoo huyu anaongoza chini ya mifumo ya katiba duni na dhaifu ambayo haitoi ridhaa au mamlaka ya yeye kuhojiwa hata na yeye akikosea.
Mwanakondoo huyu mihimili yote mitatu yupo juu yake, ni nani wa kumhoji au mshurutisha?
Nani wa kupaza sauti katiba ipate badilika? Wapaza sauti wapo chini ya uoga wa kikatiba na Bado nao ni mashabiki wa vyama vya siasa na Bado ujinga umewa tanda kwenye bongo zao.
Wapaza sauti wanashabikia vyama vya Siasa Kama timu za mpira, Yani ifungwe isifungwe mapenzi yake yapo pale pale. Wapaza sauti wanashindwa tambua ushabiki wa siasa si Sawa na ule wa mpira.
Wanashindwa tambua Chama cha Siasa kikiboronga awamu hii, awamu ijayo kitolewe.
Kabla ya nchi Hii kufanya mapinduzi ya kiuchumi kwanza yapaswa fanya mapinduzi haya.
1: Mapinduzi ya fikra, mapinduzi haya yapaswa fanywa ili kufuta ujinga ulio akilini na mioyoni mwa watanzania. Yani ni pamoja na ubadilishwa wa aina ya elimu itolewayo kwenye taasisi zetu za elimu. Watanzania wakipata elimu iliyo Bora Basi watapata kuwa Bora kifikra, kimawazo na kimitazamo.
2: Mapinduzi ya kikatiba na kimifumo ya utawala. Katiba ipate kubadilishwa ili iweze kuweka mihimiri mitatu ya nchi kuwa huru, huku mhimili bunge kuwa ndio mhimili mkuu na mlezi kwa mihimiri miwili Yani serikali na mahakama.
>>Taasisi za serikali Kama CAG, jeshi la polisi, tume ya uchaguzi, msajirivwa vyama vya siasa n.k kikatiba taasisi hizi zifanywe na kutambulika huru.
>> Uundwaji wa mabunge mawili ya nchi, bunge la sasa lifanywe kuwa bunge dogo aingie hata mtanzania yeyote tu na wa Kisimo chochote, wabunge Hawa wapate kuongoza na kutawala majimbo tu na huku liundwe bunge kuu ambao mipaka yake iwe mkoa na wabunge Hawa wawe ni wabobezi na wasomi wa tasnia mbali mbali.
>> Katiba itambue na ikiri uwepo wa serikali ya umoja wa kitaifa, itayosimikwa kila mwaka mkuu wa uchaguzi. Hii serikali itoe fursa mpaka kwa wapinzani wapate hatamu ya kupewa nyadhifa serikalini.
Bila mapinduzi hayo hata baada ya miaka 300 mbeleni Hii itabaki Kama ilivyo leo. Serikali ya awamu ya Tano, imesimama walau kwa uwepo wa JPM lakini tunasahau, kesho na kesho kutwa JPM atamaliza Muda wake.
Je, serikali zijazo zitatengamaa Kama ya leo? Kwa nini tusibadilishe katiba na mifumo ya serikali, ili serikali iwe na taasisi huru na Bora, kuliko tukawa tunavizia viongozi Bora? Viongozi hupita, mifumo na taasisi hubaki.