Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,186
- 7,492
Ndugu zangu, tatizo la mpira wetu sio makocha. Ndio maana kila mara tunabadili makocha na tunapoteza vile vile. Hata tuchukue Makocha wa timu zote kubwa za ulaya waje kufundisha timu yetu kwa wakati mmoja, kama ni wa kupoteza tunapoteza tu.
Tatizo letu ni wachezaji, na kimsingi wala si wachezaji; ni mfumo wa kuwapata wachezaji.Hebu fikiria kama mchezaji anaokotwa tu mtaani akiwa tayari ashakuwa mtu mzima, anapelekwa kambini siku mbili tatu halafu anaenda kucheza mechi ya kimataifa! Utamlaumu bure tu. Hata kama ana kipaji kikubwa kiasi gani; kipaji kisichoendelezwa hufa.
Sasa tukirudi kwenye mada ya msingi, Hatuna mifumo inayoeleweka ya kuandaa viongozi. Unakuta inapofika karibu na uchaguzi (Mechi) wanaibuka au kuibuliwa wachezaji “From nowhere” ambao hawajawahi kuandaliwa/kujiandaa kuwa viongozi kwa namna yoyote ile na baadae baadhi yao hushika nafasi za uongozi kweli na baadhi yao hubaki.
Baada ya hapo wanaanza kutekeleza majukumu yao vile wanavyotekeleza, tunaanza kushangaa na kulaamu vile wanavyotekeleza. Sisemi tusishangae pale tunapofikiri ni muhimu kushangaa. Tushangae tutakavyoshangaa, tulaumu tutakavyolaumu ila hiyo haiwezi kuwa njia ya kuaminika ya kuboresha hali ya mambo. Njia ya kuaminika ni kufanya kila liwezekanalo kuandaa na kukuza vipaji toka mapema kuliko kufikiria siasa za uchaguzi kila mara. Huo ndio uongozi.
Ni heri ya watu wasio na vipaji wanaoendelezwa au kujiendeleza au vyote, kuliko kipaji kisichoendelezwa maana kipaji kisichoendelezwa hufa au kugeuka kuwa janga.
Niwashawishi vyama vya siasa kuliona hili, lakini pia na sisi wadau mmoja mmoja tulione na tuchuke hatua kulingana na mazingira yetu.