Siasa zetu na mpira; Tatizo kocha au wachezaji?

Siasa zetu na mpira; Tatizo kocha au wachezaji?

Azizi Mussa

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2012
Posts
9,186
Reaction score
7,492
thH2UR5A9Z.jpg
Licha ya kubadilisha makocha kila leo, bado tumekuwa tukipoteza mechi karibu zote. Ingawa siwezi kukumbuka majina ya makocha wote tuliobadilisha kwa kuwa sio mfuatiliaji mzuri wa mpira, angalau namkumbuka Maximo. Ki msingi, hata wale wasio wa nazi wa mpira kama mimi, wanaweza kukumbuka vizuri kwamba tumekuwa na makocha wa kutosha lakini bado tunapoteza karibu kila mchezo mkubwa tunaocheza.

Ndugu zangu, tatizo la mpira wetu sio makocha. Ndio maana kila mara tunabadili makocha na tunapoteza vile vile. Hata tuchukue Makocha wa timu zote kubwa za ulaya waje kufundisha timu yetu kwa wakati mmoja, kama ni wa kupoteza tunapoteza tu.

Tatizo letu ni wachezaji, na kimsingi wala si wachezaji; ni mfumo wa kuwapata wachezaji.Hebu fikiria kama mchezaji anaokotwa tu mtaani akiwa tayari ashakuwa mtu mzima, anapelekwa kambini siku mbili tatu halafu anaenda kucheza mechi ya kimataifa! Utamlaumu bure tu. Hata kama ana kipaji kikubwa kiasi gani; kipaji kisichoendelezwa hufa.

Sasa tukirudi kwenye mada ya msingi, Hatuna mifumo inayoeleweka ya kuandaa viongozi. Unakuta inapofika karibu na uchaguzi (Mechi) wanaibuka au kuibuliwa wachezaji “From nowhere” ambao hawajawahi kuandaliwa/kujiandaa kuwa viongozi kwa namna yoyote ile na baadae baadhi yao hushika nafasi za uongozi kweli na baadhi yao hubaki.

Baada ya hapo wanaanza kutekeleza majukumu yao vile wanavyotekeleza, tunaanza kushangaa na kulaamu vile wanavyotekeleza. Sisemi tusishangae pale tunapofikiri ni muhimu kushangaa. Tushangae tutakavyoshangaa, tulaumu tutakavyolaumu ila hiyo haiwezi kuwa njia ya kuaminika ya kuboresha hali ya mambo. Njia ya kuaminika ni kufanya kila liwezekanalo kuandaa na kukuza vipaji toka mapema kuliko kufikiria siasa za uchaguzi kila mara. Huo ndio uongozi.

Ni heri ya watu wasio na vipaji wanaoendelezwa au kujiendeleza au vyote, kuliko kipaji kisichoendelezwa maana kipaji kisichoendelezwa hufa au kugeuka kuwa janga.


Niwashawishi vyama vya siasa kuliona hili, lakini pia na sisi wadau mmoja mmoja tulione na tuchuke hatua kulingana na mazingira yetu.
 
Ila yanga jaman ndio wanatuangusha
Yaan tunawasaidia wanashiriki mashindano ila wanafika nowhere
Sijui tuwasaidiaje sasa!!!!
 
Ikumbukwe, tofauti na kwenye mpira ambapo tunaweza kutumia makocha na wachezaji wa kuazima, kwenye siasa na uongozi, ni lazima kutumia wa nyumbani. Kwa hiyo kama si mimi lazima iwe ni wewe. Kwa hiyo ni muhimu kufikiri jambo hili kwa uzito unaostahili
 
Ila yanga jaman ndio wanatuangusha
Yaan tunawasaidia wanashiriki mashindano ila wanafika nowhere
Sijui tuwasaidiaje sasa!!!!

Mlishindwa kujisaidia wenyewe dhidi ya Ud Songo tena kwenye uwanja wenu wa nyumbani, halafu mpate muda kuisaidia Yanga!

Hiyo Yanga bado inaendelea na kombe la shirikisho, ila kwa upande wenu mnasubiria msimu ujao ufike.
 
Inatupasa tue na sports academy...

Zitakazo zalisha wanamichezo mbali mbali kuanzia level ya utoto mpaka uutuzima...


Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom