PreGE2025 Siasa zetu ziwe na mipaka yake, mwanasiasa anapotamka jambo la uongo, sheria ichukue mkondo wake!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Ungeanza na Makala kuhusu CHADEMA kuleta vurusi vya MPox na Murbug kitu ambacho ni hatari Kwa usalama wa Taifa! Kwamba aitwe na vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi athibitishe kwamba wakati serikali inatumia gharama kubwa ya muda na rasilimali fedha na watu kudhibiti kuenea Kwa ugonjwa huo, CHADEMA wanakusanya hela Kwa ajili ya kuusambaza na tujue je ugonjwa utauliza kadi ya uanachama kabla ya kuingia! Wakati Wasira na Makala wanaeneza propaganda chafu lazima uikumbushe hiyo serikali ya wajinga kuwa impunity na wao! Kiongozi anapofanya mambo ya kijinga ujue hiyo taaaisis na waliomo watafamya mambo ya kijinga
 
::::::::::::::ANGALIZO, ANGALIZO:::::::::::::::
###################
Hoja yangu imelalia katika mwendo tunakwenda nao mbele ya safari, haya yote yaliyotokea hayana mashiko endapo serekali haijatoa tamko rasmi la kukemea mwenendo wa usemaji wa uongo ndiyo maana kila mtu anajisemea vile apendavyo!
Ni hekima baada ya sikukuu ya idd ul fitr, serekali ikatoa tamko rasmi linalokemea lugha za uongo usio na uthibitisho na adhabu zake stahili, huko tuendako upo uwezekano kukachafuka zaidi...
 
Hii nchi Ili uwe mwanasiasa lazima ufuzu taaluma ya uongo.
 
Minyumbu imeumbuka!

Chuki inapopitiliza, huwa inaondoka na akili. Ukweli chadema wanamchukia sana sana huyu Mama. Penye chuki na husda, ni kawaida Mwenyezi Mungu kutia tafrani vichwani mwa wenye husda Ili kuwaumbua......huo ni mwanzo tu.
 
Kwa namna ninavyoijua nchi hii alichosema Heche ni sahihi na wanachokisema serikali sio kweli. Ushahidi ni kuwa Heche hatapelekwa mahakamani. Kwa ninavyowajua watawala hawawezi kukubali wasemwe kwa uongo na ushahidi wanao. Lazima watamburuza mahakamani. Dalili ya kuwa jambo ni la kweli au uongo ni hatua watakayoichukua πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…