SIASA

SIASA

lugoda12

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2018
Posts
276
Reaction score
574
DAR ES SALAAM; MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amesema ana sifa na uwezo wa kuongoza nafasi ya uenyekiti kwa weledi.
-
Lissu amesema kutokana na weledi wake kwenye uongozi, ndio maana Chadema ilimuona anafaa kugombea Urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
-
Amesema anashangazwa na maneno ya baadhi ya viongozi na wanachama wa Chadema wanaosema hafai kuongoza nafasi hiyo ya uenyekiti.
-
“Naambiwa na wanachama wangu na viongozi wenzangu kwamba huyu Lissu hafai kabisa, hafai hata kuongoza mtaa. Ila huyu Lissu ambaye hafai kabisa kuwa mwenyekiti alikuwa anafaa kuwa Rais kwenye uchaguzi wa mwaka 2020?” Amehoji.
-
Alisema hatishiki na maneno waliyombatiza baada ya kuingia kwenye mchuano wa kugombea uenyekiti kwa sababu anafahamu maneno hayo ni ya kiuchaguzi tu.
 

Attachments

  • images.jpeg
    images.jpeg
    36.8 KB · Views: 2
Back
Top Bottom