Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
NAIBU WAZIRI VIWANDA - SIDO LWOSAA KUKARABATIWA KWA SHILINGI MILIONI 293.99
Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe (Mb) amesema kuwa zaidi ya Shilingi Milioni 293.99 zinahitajika kwa ajili ya kukarabati na kukamilisha jengo la viwanda vidogo vidogo la Lwosaa.
Mhe. Kigahe ameyasema hayo Mei, 5 2023 Bungeni Dodoma wakati wa kujibu swali la msingi la Mbunge wa Jimbo la Hai, Saashisha Mafuwe (CCM). Mafuwe alitaka kujua ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya kufufua jengo la viwanda vidogo vidogo-Lwosaa.
Akijibu swali hilo, Mhe. Kigahe alisema Serikali imekamilisha tathmini ya jengo hilo na kupata gharama za ukarabati wa kukamilisha ujenzi wa jengo hilo ambazo ni jumla ya
shilingi 293,986,850. Alisema pia SIDO inaendelea kufuatilia suala la umiliki wa eneo hilo ili kuanza ukarabati na kumalizia ujenzi.
Aidha, Mhe. Kigahe alisema Serikali itaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ukarabati na kukamilisha ujenzi wa jengo hilo ili shughuli kusudiwa zianze kufanyika kwa manufaa ya wananchi wa Lwosaa na Taifa kwa ujumla.