Sielewagi maana ya R.I.P (REST IN PEACE)

Wafu wapo wapi?
 
Wafu wapo wapi?
 
Eti Yesu atarudi kuhukumu,kwani huko aliko hakuna wa kuhukumu?uongo mwingine wa hovyo sana,naomba nioneshwe kwenye biblia ni wapi Yesu kasema atakuja kuhukumu?
Sisi wakristo wa kikatoliki watu wa dogma tunasema hili ni fumbo la imani.
"Kristu alikufa,
Kristu alifufuka,
Kristu atakuja tena,
Kuwahukumu wazima na wafu"

Kama vile dini fulani wanavyoamini Kitabu chao tukufu kilishushwa na Mungu hakikuandikwa na binadamu.

BTW, maana ya dogma ni:
dogma noun [ C or U ] uk /ˈdɒɡ.mə/ us /ˈdɑːɡ.mə/ disapproving. a fixed, especially religious, belief or set of beliefs that people are expected to accept without any doubts. Ideas, concepts and theories.
 
Naomba kutoa elimu ila sio kufundisha Imani, maana kila mtu yuko huru kuamini anacho amini.

Katika Maandiko Matakatifu sisemi Biblia sio kwa bahati mbaya, kuna kitabu cha pili cha Makabayo sura ya 12 ambapo tunasoma Mungu akimwagiza Yudas Maccabeus akusanye fedha kutoka kwa watu(waamini) ili kutolea sadaka kwajili ya roho za marehemu wanajeshi ambao walikufa vitani.

Huo ndio msingi wa Kanisa Katoliki kuombea marehemu. RIP kwa bahati mbaya sana inatafsiriwa kwa lugha ya Kiingereza lakini kiukweli hicho ni kifupisho cha lugha ya Kilatini RIP = Requiscant In Pacem. Utagundua pia watu hudhani vifupisho kama i.e au etc au e.g ni vya lugha ya Kiingereza la hasha hivyo vyote ni vya lugha ya Kilatini.

Martin Luther mwanzilishi wa Protestantism kwa kuwa alikuwa padre na mwanatheolojia wa Kanisa Katoliki alifahamu maana ya kitabu cha makabayo, hivyo alipoongoza upinzani wake aliondoa vitabu kutoka katika orodha ya vitabu vilivyomo katika Maandiko Matakatifu. Ndio maana, ukiondoa Kanisa Katoliki madhehebu yote mengine hutumia Biblia yenye vitabu 66 badala ya 72(73).

Kwa nini Luther alikiondoa kitabu cha Makabayo? Wakati huo Kanisa Katoliki lilitaka kujenga ukuta kuzungushia Vatican kuepuka wavamizi, likawahamisisha waamini wake kama alivyofanya Yudas Maccabeus watoe fedha na kufanya hivyo roho za marehemu wao zitapata msamaha wa dhambi na kupokelewa mbinguni. Luther alilipinga jambo hilo, Unajua kwamba kanisa Katoliki hukusanya kodi kutoka nchi zote ambazo ukatoliki upo, hii ilimaanisha Ujerumani itachangia uchumi wa Roma.

Je Luther alikuwa sahihi au sio sahihi kuondoa baadhi ya vitabu? Ni kwa wanazuoni kujadili. Je vipi leo akitokea mtu mwingine akaongeza Injili ya tano je atakuwa sahihi? Kila mtu akiwa na uhuru wa kuongeza au kupunguza tutafika wapi?

Requiscant in Pacem ni sala katika Requiem Missae ambapo mkristu mkatoliki baada ya kumaliza safari yake hapa duniani huombewa...je ni baba gani ambaye mwanae akimwomba samaki atampa ng'e? Kanisa sio kazi yake kuhukumu watu, kanisa huombea waamini wake pumziko lenye heri!

Ushauri wangu tukisome hiki kitabu cha Makabayo tujiridhishe wenyewe!!!!!!!
 
Ubarikiwe mkuu
 
ngoja tusubil wapinga maandiko waje
Asante kwa somo
 
It’s a stupid saying by some stupid denomination. They believe by saying that a dead person will be exonarated of his or her sins and be allowed into heaven instead of hell fire
 
Yesu ni mungu wa wapi?mnajiita wasomi lakini ni empty kabisa,rudi kaikague biblia vizuri itakueleza huyo unaemuita mungu ameelezewa vipi
Unajua uzuri wa imani ni moja hakuna anayeweza kuthibitisha. Mwenye kuamini Mungu yupo hawezi kuthibitisha na asiyeamini Mungu yupo hawezi kuthibitisha. Hivyo badala ya ninyi kujifanya mnajua biblia bora mngebaki na imani zenu bola kukosoana.

Nionavyo mimi hata wewe hujaisoma biblia ama umeisoma hujaelewa lugha ya biblia ama ya wayahudi wakati ule. Ungeielewa ungefahamu kuwa hata kakubali kuwa ni Mungu ama mwana wa Mungu
 
Kama mtu akifa hajui neno lolote... maanake ujumbe wa REST IN PEACE haujui pia...
Ni umizimu... na hila za shetani kuwadanganya wanadamu kuwa mfu anasikia... kama alivyodanganyanya pale bustanini kuwa HAKIKA HAMTAKUFA wakati MUNGU alisema HAKIKA MTAKUFA
Sasa hapo kujiuliza kati ya MUNGU MUUMBAJI na Shetani ni nani muongo?
Kama MUNGU ni muongo basi wafu wanasikia
Kama Shetani ni muongo basi wafu hawajui neno lolote na kuwaambia waREST in Peace ni kuungana na shetani.
 
u
Eti Yesu atarudi kuhukumu,kwani huko aliko hakuna wa kuhukumu?uongo mwingine wa hovyo sana,naomba nioneshwe kwenye biblia ni wapi Yesu kasema atakuja kuhukumu?
unaamini atarudi kwa mara ya pili?
tuanzie hgapo kwanza
 
aliwaambia mkila tunda hamtakufa na walipokula kweli hawakufa maana tunda halikua na sumu
 
aliwaambia mkila tunda hamtakufa na walipokula kweli hawakufa maana tunda halikua na sumu
 
aliwaambia mkila tunda hamtakufa na walipokula kweli hawakufa maana tunda halikua na sumu

Mhhhh kwa mantiki hiyo Mungu ni MUONGO!?????

Mwanzo 5:5
Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa.
 
Just to correct you....Yesu..hata rudi kuhukumu mtu sio kazi yake hiyo ni kazi ya Mungu kuhukumu...
Neno alilolitamka Yesu ndilo hilohilo litakalotuhukumu. Mhukumu ni Yesu mkuu, ndiye anayejua ngano na magugu
 
Nadhani ibada ile inafanyikaga kwa ajili ya wale walio hai na siyo kwa ajili ya marehemu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…