Sielewagi maana ya R.I.P (REST IN PEACE)

Sielewagi maana ya R.I.P (REST IN PEACE)

Yesu ni mungu wa wapi?mnajiita wasomi lakini ni empty kabisa,rudi kaikague biblia vizuri itakueleza huyo unaemuita mungu ameelezewa vipi
Yesu ni Mungu, hakika!! Kama unakubali ni mwana wa Mungu, lazima ukubali pia ni Mungu.

Mtoto wa mwanadamu, ni mwanadamu
Mtoto wa simba ni simba
Mtoto wa nyoka ni nyoka.

Iweje mtoto wa Mungu asiwe Mungu?

Yoh 3:16 "Kwa maana jinsi hii, Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwana wake wa pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele"

Ngoja nikupe na shot yake
Screenshot_20180502-172955.jpg
 
*R.I.P[emoji779]*
*R.I.P[emoji779][emoji779]*
*R.I.P[emoji780][emoji780][emoji780]*
⚰⚰[emoji24]⚰⚰[emoji24]⚰⚰

*"PUMZIKA KWA AMANI" [emoji779]*

JE KUNA AMANI IPI KABURINI[emoji780][emoji15]

*"MUNGU ILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI"*

HUKO MAHALA PEMA NI WAPI[emoji780][emoji15] JE WAPO WASIOLALA MAHALA PEMA HUKO PEPONI?[emoji134]‍♂[emoji779]

*UTANGULIZI*
Limekuwa ni jambo la kawaida kuwaambia ndugu zetu waliolala ( wafu) wapumzike kwa amani ( R.I.P) na wengine wakaenda mbali zaidi kumsihi Mungu azilaze Roho hizo mahali pema!

BIBLIA INASEMA WAFU WAKO WAPI???
Mwanzo 3: 1 *"Kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi"*

»»» NB: WAFU WOTE WAPO MAVUMBINI HAIJALISHI WALITENDA MEMA AU MABAYA WANASUBIRI YESU AJAPO KUTOA HUKUMU.

R.I.P( PUMZIKA KWA AMANI)
JE KUNA AMANI YEYOTE KABURINI MTU ANAPOKUFA???
Muhubir 9:5 *"Lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa"*

NB: WAFU HAWAJUI NENO LOLOTE WALA HAWANA MAWAZO WALA KUMBUKUMBU YA CHOCHOTE NI KAMA MEZA, JIWE NA VIUMBE VYOVYOTE VISIVYO HAI! KWAHIYO KUWAAMBIA WALALE MAHALI PEMA HAKUNA WEMA WALA GHASIA KABURINI. WAFU WOTE HAWAJIELEW!!

*JE TUKIWAOMBEA WAFU WANAWEZA KUFANYA TENA IBADA?* KUTUOMBEA?? AU TUKIWAOMBEA MUNGU ANAWEZA KUWASAMEHE???
»»» Zaburi 115.17
*"Sio wafu wamsifuo BWANA, wala wo wote washukao kwenye kimya"*

»» Zaburi 143:4
*"Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake,Siku hiyo mawazo yake yapotea"*

»» Mhubiri 9:10
*"Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe"*

HITIMISHO
[emoji116][emoji116][emoji116]
O1. R.I.P.( PUMZIKA KWA AMANI)
Huu ni msemo wa kipagani tena unaokinzana na maandiko maana wafu hawajui chochote hivyo hakuna amani yoyote kaburini mfu hajitambui hajielew ni kama kochi au peni hana ufahamu.

O2. MUNGU ILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI
a) Mungu hapangiwi pa kumuweka mfu

b) Mfu akifa anarudi kuwa udongo

O3. MFU HAWEZI KUKUOMBEA WALA KUOMBEWA DHAMBI ZAKE ZIISHE

a) Wafu hawawezi kutuombea sio bikra Mariam mama wa Yesu wala mtakatifu yeyote aliyekwisha kufa anaweza kutuombea Kwa Mungu, Biblia inasema tuombe kwa jina la Yesu pekeee.. (Wafilipi 2:10)

b) Mtu akifa historia yake imefungwa hawezi kuombewa dhambi zikamtoka,

c) Ibada na maombezi ni kwa walio hai tu

IBADA ZA KUOMBEA WAFU NI UPAGANI NA MACHUKIZO KWA BWANA

*WITO:* TUMKIRI YESU NA KUMFUATA TUKIWA HAI ILI HATA TUKIFA TUWE NA TUMAINI KUWA AJAPO MARA YA PILI ATATUPA MIILI YA KUTOKUHARIBIKA NA TUTAISHI NAE MILELE..!!

Nakuachia swali la changamoto:
*Kama ibada ya kumuombea mfu ina maana kuna umuhimu gani wa kumtumikia Mungu ukiwa hai si usubiri tu ukifa uombewe dhambi zitoke? Je, nani atapewa adhabu ya moto na kupotea milele wakati wafu wote huwa wanaombewa?*

TAFAKARI
[emoji106] [emoji106]
 
Back
Top Bottom