Sielewi kwanini Maalim Seif ameenda Chato kuonana na Rais Magufuli

Sielewi kwanini Maalim Seif ameenda Chato kuonana na Rais Magufuli

Status
Not open for further replies.

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
44,629
Reaction score
83,056
Sikupata jibu na niliwaza sana kilichompeleka Maalim Seif Ikulu kukutana na Magufuli ni nini?

Niliwaza sana, nikamlinganisha kitendo hicho na say, Museveni kukutana na Bobi Wine, his main rival au enzi hizo PW Botha kukutana na Mandela kwa faragha. Watu wasingelielewa.

Kumbe usaliti wa Maalim ndio ulikuwa unajengwa. Zitto hakuweza kufikiri mpaka huko au alijua akamezea kwa maslahi ya baadaye and the like!

Kwanini sasa Maalim aliwasubject watu kwenye mateso na vifo wakimfuata yeye na kumfia yeye wakati anajua fika ataungana na Magufuli? Kweli wanasiasa (baadhi) ni Mashetani!

Swali:
Hivi 2025 Maaalim atagombea urais Zanzibar au ataungana na CCM kuiponya nchi?
 
Watanzania ni wepesi kulaumu hata kwa mambo yasiyohitaji lawama. Mlitaka Maalim afanye nini wakati wafuasi wake mwenyewe wanafiki? Mwacheni amalizie uzee wake pazuri kwa kuwa hata umri umeshamtupa mkono na siasa ndo basi tena...
 
Katika Siasa hakuna adui wala rafiki wa kudumu.

Pia shabiki wa siasa hatakiwi kukaza shingo sana... ataumia huku akiacha wanasiasa wakigonga mvinyo!
hewala mzee; wewe umenena ambacho wengine anapenda kumumunya tu!
 
Uungwana ni vitendo.

Maalim Seif ni muungwana. Kakubali yaishe. Ameona mbali.

Zanzibar moja ni muhimu kuliko maslahi yake.

Wenye roho mbaya za kidhalimu ndiyo watamponda huyu mzee.

Hakuna marefu yasiyo na ncha.

Vita sasa basi. Maisha mbele
 
Kama Maalim kwenda Chato ni tatizo basi hata Chadema kupokea pesa za ruzuku za serikali ya CCM pia ni tatizo.

Kama Chadema kupokea pesa za serikali ya CCM sio tatizo basi na Maalim kwenda Chato sio tatizo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom