Sielewi Nini kinaendelea kwa huyu mwanamke wiki hii

Sielewi Nini kinaendelea kwa huyu mwanamke wiki hii

Natumai umekutana na manzi Fulani hv,kama ndio huyo basi afadhari Yako wewe Una biashara Yako mie nilikutana naye nikakaa naye siku 3 Ijumaa,jmos na jipi kwenda Job J3 nikapigwa Warning letter Moja nzito Sana.
Sasa sikuwaza kabisa kuwa yeye anahusika..Nimerud tena kwake tokea Alhamis mpaka jmos kwenda kazini J3 nakutana na kikao Cha Boss!!Ninavyoulizwa hata sivielewi nikaambiwa nenda kaandike Utetezi kabla sijapeleka Sec anakuja ananiambia unaitwa tena nafika pale nakutana na Termination letter.

Imefika jioni ananiandikia baby pole na KAZI upo wapi nimekumiss Sana
Dah! Pole san,
Uyo mwanamke ana gundu balaa [emoji26]
Kwaiyo uliendelea nae au ulimtema?

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Wiki 2 zilopita.
Tuligombana, kanuna na kila mtu akabaki kivyake na maisha yake, Sasa tarehe ya rejesho ilivokaribia nikaona Bora nintafute turudiane, kweli jumatano tumerudiana.

Siku ya Ijumaa tumekutana na jumamosi namshkuru Mungu mambo yameenda Safi na mwanga nikaanza kuuona. Ikabd nifanye mpango Jumapili pia tukakutane, ili angalau wiki hii nihakikishe naianza kwa kishindo. Kweli tumekutana na baada ya hapo nmerudi kwangu.

Ila cha kushangaza Kulipokucha jumatatu, siku iliniendea vibaya sana tofauti na miaka yote, nikaona sio kesi, labda ni kwa sababu siku nyng zilipita hatujakutana sababu ya mgogoro, Nikajipa moyo mambo yatakaa sawa tu.

Jumanne pia
Nikajitahidi tumekutana, ila jumatano nayo ikaamka imeenda vibaya sana, mauzo hayaeleweki kabisa. Nikabaki na maswali kibao kichwani ila nikajipa moyo Tena, Huenda sijapata mda wa kutosha wa kukaa nae.

Sasa Jana usiku
Ikabidi nisingizie msiba, nmeenda kwake na nmekesha nae kabisa mpaka alfajiri, Leo nmeamkia kwake nmeunganisha moja kwa moja hadi dukani kwangu.

Ila sahivi mpaka saa 8 hii mchana nnapoandika Uzi huu bado sielewi nini kinaendelea kuhusu huyu mwanamke, yaani bora hata siku 2 hizi zilizopita nilizokua nalaumu.

Kinachoniwazisha zaidi, ni kwamba tarehe ya rejesho nayo iko karibu Sana, Ni jumanne ya wiki ijayo ya tar 7.

Yaani Hapa hadi kichwa kinauma,
Maana nina siku 2 TU (kesho na jumatatu) za kupambania rejesho na bado makusanyo yangu hayafikishi 50% ya rejesho lote nnalodaiwa bank mwezi huu[emoji29].
Hali inaendeleaje huko?? Ngekewa imerudi au??
 
Mwaka unaelekea kukata sasa. Rejesho natumai ulipata
 
Back
Top Bottom