Sielewi tatizo....

Magoo

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2011
Posts
445
Reaction score
72
Nina g.f ambaye tumepanga kuoana muda si mrefu Mungu akijalia. Siku za nyuma nimewai kuwa na mahusiano tofauti na wasicha wengine ila nilikuwa mgumu sana katika kutoa pesa yangu na mapenzi niliona kitu cha kawaida sana, ila kwa huyu binti sijui ni limbwata ama ni nini coz nahisi mapenzi yangu kwake si ya kawaida mfano nikimkosa hewani amani yote inatoweka, kila ninalofanya lazima nimwambie nashtuka baadaye nam2mia pesa mara kwa mara hata asiponiomba, tayari nina mpango kumfungulia biashara asije ajiriwa na serikali, kujali wengine kama ndugu kumepungua sana na sasa naanza kupata mashaka, binti ameshika sana dini na ni msikivu pia mnyenyekevu sana sidhani kama anaweza fanya mambo ya giza, sifikiri kama ni mapenzi ya kawaida na sasa nataka niondoe hii khali ila nashindwa nianze vipi.
Msaada kimawazo tu wakuu.
 
boy, you in aone real shit ...
 
Hilo ndo limbwata lako sasa! Ungemuambia akuongezee limbwata ili roho yako nayo ipone na nyumba ndogo na ukimwi.
What else do u want? Wenzio wanalalamika kuibiwa, ama una hamu ya kuwa cheated?
binti ameshika sana dini na ni msikivu pia mnyenyekevu sana
 
Mie sioni tatizo mkuu, ni nguvu ya mapenzi tu hayo na wewe umefika sasa kiasi cha kwamba umekuwa insecure mpaka unamwaga pesa hovyo hovyo kwa vile unaogopa wengine wasije kutumia nguvu ya pesa kumchukua.

Jiamini mkuu hata ukimfungulia biashara kama anataka ku-cheat ata cheat tu.

Umefika kimapenzi hapo na wala hakuna nguvu ya giza na acha kuogopa kumpoteza huyu dada wewe chukulia hali ya kawaida usije ukawa unamsumbua kila saa kwa msg kutaka kujua yuko wapi mpaka ukamfukuza.

Usiwatupe ndugu zako kivilee mkuu jaribu ku-balance mambo kidogo.

Kila la kheri, toa hofu.
 
Labda tuanzie hapa kwanza,
Ni kabila gani huyo mdada??
 

Aksant mkuu kwa ushauri wako
 

ee bwana amna cha limbwata wala nini, mmeendana tu,na iyo huwa inatokeaga.
 
Inawezekana hayo mambo anayokufanyia huyo dada ndo mana uko crazy about her, siyo limbwata bro na kama ni limbwata lita expire siku moja ila cha kukushauri sali mwombe mungu kama huyo ndo mke au laah. kama wew ni mkatolik sali novena yan hyo ni special prayer kwa ajil ya kuombea kitu fulani, nenda pale st.joseph kuna novena ya mtakatifu yuda thadei binafsi imenisaidia sana na mpaka sasa naitumia kwenye mambo yangu mengi. na kama ni wa dhehebu nyingine basi sali kwa imani yako mana mke mwema anatoka kwa MUNGU.
 

Yaani kiongozi kwa mujibu wa ushauri uliom'pa mdau-mwenza haufanani na jina lako! Ushauri wako ni ecxelent! Sijui ilikuaje Fergy akakupiga 8 wakati una ma'ushauri mazuri kiivo! Oooh-maaama!
 
Magoo! Soo much whistles it may lead dog to the wron' direction! Also mimi na wasiwasi na hivyo unavyokata mikwanja japokua sikuulizi ni ya urithi ama zako mwenyewe bt above ol try to avoid extravagancy my fellow mdau.
 



Wenger i do tell you hutendi haki kuishia tu sports kule bila kututembelea.....lol... Umeona mambo ambayo hua watubania? The Advice is Great.
 



Magoo hapo Wenger kaongea ya Msingi saana, in short in kwamba you are in love (atleast to my understanding) ila tu nakupongeza pamoja na yoote hayo somewhere in side you waweza reason what is good and not good hasa in relation na the way you feel towards the lady. Hio itakusaidia saana katika maamuzi ya msingi mradi usiwe mwoga....

Best of Luck...
 
eti "kuishi kwingi ni kuona mengi"
mi nimeishi kidogo tu nishanza kuona mengi angalia kama huyu mapenzi yamemdatisha
anasema kibwata mara sio hali ya kawaida .Hilo ni penzi lipo kwenye pick likichuja utajuta

na utaliona halina maana kabisa jitahidi kulimaitain.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…