Nina g.f ambaye tumepanga kuoana muda si mrefu Mungu akijalia. Siku za nyuma nimewai kuwa na mahusiano tofauti na wasicha wengine ila nilikuwa mgumu sana katika kutoa pesa yangu na mapenzi niliona kitu cha kawaida sana, ila kwa huyu binti sijui ni limbwata ama ni nini coz nahisi mapenzi yangu kwake si ya kawaida mfano nikimkosa hewani amani yote inatoweka, kila ninalofanya lazima nimwambie nashtuka baadaye nam2mia pesa mara kwa mara hata asiponiomba, tayari nina mpango kumfungulia biashara asije ajiriwa na serikali, kujali wengine kama ndugu kumepungua sana na sasa naanza kupata mashaka, binti ameshika sana dini na ni msikivu pia mnyenyekevu sana sidhani kama anaweza fanya mambo ya giza, sifikiri kama ni mapenzi ya kawaida na sasa nataka niondoe hii khali ila nashindwa nianze vipi.
Msaada kimawazo tu wakuu.
Msaada kimawazo tu wakuu.