Siendi Mkoani Ng'ooo!! Dar es salaam is the future! Mikoani ni didimizo la uchumi binafsi


You are a star lara1. You real are! Yaani umekata nyanga za kufa mtu. Ukweli mtupu, mifano hai na hakuna kumung'unya maneno.....This has inspired me a lot.
 
Ni kweli, japo sio kweli sana.
Tatizo lako @lara1 huwa unaandika maneno meeengi kitu kidogo, jaribu kuwa unafupisha utusaidie tunaoingia kwa kuiba dakika chache za kazi
 
Ni kweli, japo sio kweli sana.
Tatizo lako @lara1 huwa unaandika maneno meeengi kitu kidogo, jaribu kuwa unafupisha utusaidie tunaoingia kwa kuiba dakika chache za kazi

Huyu demu aloleta uzi akili anazo sana tu sema na imani kubwa sana hua hafanyii kazi mawazo yake! pengine hana wakumuongoza,. Kama mafanikio maishani yangekua sawa na mitihani ya darasani kuandika kwenye makaratasi basi angesha fankiwa,! Mungu amsaidie aweze kufanya mawazo yake kua katka vtendo!
 
Lara 1 mtizamo wako umeuangalia upande mmoja tu! Yapo matatizo mengi ambayo ukiyafahamu yanaweza kuubadirisha mtizamo wako juu ya Dar Es Salaam.

1. Dar Es Salaam tunalikubali kuwa nini Jiji maarufu sana Tanzania ila kuna mambo mengi yanayolifanya lionekane kuwa si Jiji zuri sana kuishi,moja wapo ya tatizo kubwa kwa Dar ni kuporomoka kwa maadili kitu ambacho kinafanya Jiji hili kuwa siyo sehemu nzuri ya kufanya makazi na kulelea watoto wetu.
Kwa mfano kushamiri kwa biashara ya UKAHABA kwa sehemu kubwa ya Jiji hili inatia kinyaa! Siku moja nilikwenda Dar Live kuangalia Wasanii waliokuwa wana tumbuiza pale, kabla sijafikia Dar Live mwenyeji wangu alikuwa amesimama upande wa pili wa barabara karibu na Bar moja inaitwa MASAKUU BAR sehemu maarufu sana pale Mbagala Zakhiemu,nilipofika pale baada ya kuitwa na mwenyeji wangu niliyoyaona yalinisikitisha sana,niliwakuta mabinti wadogo sawa na watoto wangu wako busy kuuuza miili yao nilishangaa sana kwa sababu mambo kama hayo tulizoea kuyasikia yanafanyika sana Mitaa ya OHIO na sehemu kama KINONDONI na SINZA kumbe hata MBAGALA?
Lakini baada ya kutafakari sana nilikuja kugundua kuwa ugumu wa maisha unaochangiwa na usugu wa mawazo wa watu wengi kuona kuwa Dar ni sehemu tosha ya kupata maisha yao kwa urahisi kama unavyofikiri ndugu yangu Lara 1.

2.Kero ya usafiri asubuhi wakati wa kwenda Mjini au sehemu nyingine yoyote kama Hospitali,Shule na Sokoni na wakati wa kurudi kutoka sehemu hizo pia unachangia kufanya Dar kuwa siyo sehemu nzuri ya kuishi.

3.Dar inaongoza kwa uchafu kuliko Majiji mengine yote ya Tanzania,mifuko ya rambo imezagaa kila kona ya Jiji na Wakazi wa Dar hawaoni kuwa Jiji lao ni chafu.

4.Dar haina mpangilio mzuri wa Makazi kila mtu anajenga anavyotaka tena bila utaratibu,ukitembelea maeneo ya TABATA,VINGUNGUTI,MBURAHATI,KIGOGO,MANZESE,MBAGALA ni shida tupu

5.Mifumo mibovu ya maji taka na maji safi inafanya pia Dar kuwa siyo sehemu nzuri ya kuishi ingawa matatizo yote haya Wakaazi wa Dar wanayafumbia macho na kujifanya hawayaoni kumbe matatizo yapo na kila siku yanazidi kukua.

6.Gharama za maisha kwa Dar ni kubwa mno ukilinganisha na sehemu zingine zote kama Mbeya,Songea,Morogoro na sehemu za mikoa mingine.
Kwa ujumla wake Dar Es Salaam hapafai kuishi kama unataka kuilea familia yako kwa maadili mazuri. Dar kama hauna kipato kuishi ni kama JEHANAMU maaana kila siku utawaona wenzako wanafaidi maisha na wewe hauna kitu hali inayopelekea Dada zetu kujiingiza kwenye biashara ya kuuza miili yao halikadhalika na Vijana wa kiume pia kujiingiza kwenye biashara hiyo! Shime ndugu zangu murudi vijijini kwenu muanzishe miradi ya Kilimo cha mboga mboga mazao mengine ya chakula na ufugaji ambao unaweza kukutoa kwa muda mfupi sana.
 
Uko sahh,kuna baadhi ya mikoa haina fursa na mtu hupat changamoto za kimaisha kabisa..
 
hiyo ndo fact, mi mweneyew nshaendaga ku hustle mkoa kwa muda flani ila nkaona kule akili inakua km imesinzia na chaangamoto hakuna, na watu wanaokuzunguka wanaoana we ndo mkalii wkt we unajiona bado sanaaa
 

Nami siendi mikoani mambo yote hapahapa mwanza
 
Hata me naona hilo,nilikaa Geita napiga mishe nalipwa vizuri kuliko navyolipwa sasa hivi Dar ila niliondokd nipo dar na sitaki tena kurudi mkoani...
 
Watu kama nyie huwa hamkosi, make kunawengine hadi walishajenga bifu na mvua! Ikinyesha mvua tu wanavuta midomo make wanajua ni muda wa wao kuwa samaki kwenye makazi yao lakin bado wanakuambia hawahami ng'o!
Mwingine unakuta hata kupunzika vya kutosha hamna make saa 11 asubuhi kashashika bomba kwenye daladala wakati mie ndo nasubiri saa 12 nisikilize amka na bbc na kisha magazeti, ukimkuta anatembea na kakitambaa anajifutafuta kutwa nzima teh! lakin anakuambia ahami ng'o!
 
Huwezi amini wafanyakazi wengi wa Geita wanaishi dar hasa wa mgodini na mara kibao hufunga safari karibu kila wiki wakipata off tu.Dar kuna utamu wake bhana...

Ni walimbukeni wenzio, 'nang'atuka naenda kuishi butiama' Nyerere.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…