Sifa kuu za Biashara zilizojaa Ghiliba na Utapeli nchini

Sifa kuu za Biashara zilizojaa Ghiliba na Utapeli nchini

Truths

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2017
Posts
1,494
Reaction score
1,504
Biashara hizi kutakiwi kujiingiza, kwasababu hata kama huna tamaa. Zinakujengea matumaini na tamaa ya muda mfupi ya Kutajirika.
Zina sifa mbili au zote ya sifa zifuatuatazo;-

1. Idea ya biashara(Business Venture) inakua Rahisi kuianzisha au kuwekeza.

2. Inatoa ahadi ya Faida kubwa kuliko unachoweka. Yaani Utajiri wa Haraka.

3. Ukiwekeza japo ni mara ya Kwanza huangaiki wewe, wapo watu wa kukufanyia wewe. Ili mradi umeweka pesa yako.

4. Wahamasishaji (mentors).
Ukiwasikiliza ni kama wao wanapenda ufanikiwe wewe na sio wao na ndugu zao.
Wahamasishaji wengi ni waganga njaa, wanaaminiwa, waliovalia nguo zao za Mtumba zilizowakaa vizuri. Kutokana na mionekano yao na ujasiri wao wa kujieleza, hupata vibali mbalimbali katika Taasisi za Serikali ili kuwaendea na kuwafikia watu wa calibre tofauti na kuwarubuni ili wajiingize kwenye hizi biasahara wapate kuwatafuna.

5. Hawa mentors, Wanaposhawishi hupendelea zaidi kutolea mifano ya Matajiri waliofanikiwa zaidi Duniani ili ku-ispire. Mfano, Jack Ma, Billy Gates, Carlos Slim, Warren Buffet, Jeff Bezos, Barack Obama, Donald Trump, nk.

6. Kua na chumba kimoja cha ofisi ama Uwepo wa Ofisi zao za mifukoni.

7. Mentors huandaa mikutano yenye Tozo za kiingilio kwa madai kufundisha watu namna ya kufanya biashara fulani. Mikutano hii sometimes hujazwa watu maarufu ili kuleta mvuto. Kiingilio unacholipa ndio posho ya kazi yao kwa siku

8. Mikutano wanayoiandaa, sometimes wanakwenda mbali zaidi kwa kuandaa vyeti visivyo tambulika kwenye organization yoyote inayoheshimika nchini. Ambacho utaikilipia,ada. Wanawatunukuu Vyeti wale wote walioshiriki mafunzo haya kwa siku zote za mikutano hii. Cha msingi Ni Malipo yako tu.

9. Biashara hizi,Nyingi, Faida yake hutegemea na Idadi ya watu uliowashawishi wajiunge na Biashara zaidi. Na sio huduma(Services) ama uzalishaji(production).( Wajinga ndio waliwao)

Duniani kama huja andaa ndoto zako, wako watakaokuja na kukutumia kutengeneza ndoto zao.
Utakua kama daraja.

Whenever the idea sounds too good, think twice
 
8. Tabia ya pesa ni usiri, yeyote anayepata pesa huwa hasemi ukweli kuwa anapata wapi ana anapata pata vipi. Ukiona mtu anakushawishi muende kufanya kitu fulani kuna mapesa mengi ujue ndio unaenda kutapeliwa
 
Na wamekuja kwa kasi ya ajabu sana kipindi hiki,wamezagaa kila kona wanawinda watu wa kuwatapeli
 
Wako wengi sana humu, hata kupiga picha wakiwa kwenye ndege, magari ya kifahari, mijengo, nje ya nchi n..k.
ukiingia KINGI umekwisha, ukiponda biashara na matangazo yao utashambuliwa na wahusika kila kona..
 
Wako wengi sana humu, hata kupiga picha wakiwa kwenye ndege, magari ya kifahari, mijengo, nje ya nchi n..k.
ukiingia KINGI umekwisha, ukiponda biashara na matangazo yao utashambuliwa na wahusika kila kona..
Hata wakati mwingine wanakublock!
 
Mtu namjua kwao ni masikini wa kutupwa anakuja kunihubiria mafanikio huwa nampa jibu moja tu, tafuta ukoo wenu mkitajirika wote mtatuajiri sisi.
 
Back
Top Bottom