Hii sio kweli, Wasukuma sio wachawi, bali wanauchukia mno uchawi mpaka mtu akituhumiwa tuu kwa uchawi, huuliwa. Kesi ya Mauji Mwanza na Shinyanga, ni uthibitisho wa chuki ya Wasukuma dhidi ya vitendo vya uchawi.
Tabia mbaya za Wasukuma, ungesema
1. kupenda wanawake weupe matokeo yake wanapenda zaidi ya mwanamke mmoja.
2. Kuwa na moyo wa upendo kupindukia, matokeo yake mioyo yao inakudondokea, hawaoni, hawasikii.
3. Wana roho nzuri kuvuka mipaka, matokeo yake ni watu wa kutumia, mwaga offa na kuhonga sana, hivyo kupata maendeleo kidogo.
4. Wanapenda sana lile somo kupindukia, matokeo yake, wewe kama ni mwanamke, ameolewa na Msukuma chapa ng'ombe, 'rigwaride rinaweza kumshinda'.
5. Wanawake wa Kisukuma, hawana wivu, hali inaopelekea kuwaachia waume zao kujivinjari watakavyo.
6. Wanapenda kufurahi sana, matokeo yake hupenda sana starehe, kujirusha, na kilaji
7. Hawajali, ni ma don't care, matokeo yake wakilewa lazima waimbe, wakiimba lazima wapige kelele ambazo hugeuka bugudha kwa wenzao.
8. Wakikutana hata wawili tuu kwenye kundi la watu wa makabila mengine, wataongea Kisukuma bila kujali kuwa ofend hao wengine wote.
9. Kule Usukumani mfano wilaya ya Bariadi mkoani Shinyanga, lugha rasmi ni Kisukuma kitupu hadi madukani na maofisini hadi ofisi za serikalini.
10. Ni washamba sana, wana poor dress code!.
Mazuri yao.
Ni kabila linaloongoza kwa watu wenye roho nzuri Tanzania, wanaume wanaaongoza kwa kupenda, wanajua kuoa tuu, kuacha hawajui labda waachwe wao, na wanawake wanaaoongoza kwa uvumilivu, kushindia maji, kulala njaa na huku hawana wivu, Wasukuma wanaongoza!
Pasco