Sifa na vigezo vya Kisheria na Kiimani ili uweze kuoa Mke

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
1.Katika Uislamu,

Mtu anayetaka kuoa anapaswa kuwa na sifa kadhaa ili kuhakikisha ndoa inakuwa yenye baraka, imara, na yenye msingi mzuri wa kidini na kijamii. Sifa hizo ni pamoja na:

1. Kuwa na Imani ya Kidini (Ucha Mungu):

Mwanamume au mwanamke anayetarajia kuoa anapaswa kuwa mcha Mungu, mwenye kufuata maamrisho ya Kiislamu na kujiepusha na makatazo.

Mtume Muhammad (SAW) alisema:
"Mwanamke huolewa kwa sababu nne: mali yake, nasaba yake, uzuri wake, na dini yake. Chagua aliye na dini, utafaidika." (Bukhari na Muslim).


2. Uwezo wa Kifedha:

Mwanamume anapaswa kuwa na uwezo wa kugharamia mahitaji ya mkewe na familia yake, ikiwa ni pamoja na mahari (Mahr), makazi, chakula, na mavazi.

Allah amesema:
"Wawezeni wanandoa wasiokuwa na uwezo. Mwenyezi Mungu atawatajirisha kwa fadhila Zake..." (Qur'an 24:32).


3. Uwezo wa Kijinsia na Afya Njema:

Mwanamume anapaswa kuwa na uwezo wa kutimiza haki za ndoa za mke wake, ikiwemo za kijinsia. Pia, afya yake inapaswa kuwa nzuri ili kuepuka matatizo yatakayoweza kuathiri maisha ya ndoa.


4. Ukamilifu wa Kiakili na Kihisia:

Mtu anayetarajia kuoa lazima awe na ukomavu wa kiakili na kihisia ili aweze kushughulikia changamoto za ndoa kwa busara.

5. Hali Nzuri ya Tabia:

Tabia njema ni msingi muhimu katika ndoa. Mtume (SAW) alisema:
"Mwanamume bora zaidi ni yule anayewatendea wake zake kwa wema." (Tirmidhi).

6. Kukubaliana kwa Wali wa Mwanamke (kwa Wanawake):

Katika Uislamu, wali (mlezi wa mwanamke, kwa kawaida baba au ndugu wa kiume) ni sehemu muhimu ya mchakato wa ndoa. Ruhusa yao inahitajika isipokuwa katika hali maalum.

7. Kusudio Safi la Ndoa:

Ndoa ni ibada na njia ya kujitakasa. Mkusudio la kuoa linapaswa kuwa kuendeleza familia ya Kiislamu, kusaidiana katika dini, na kufanikisha amani na utulivu wa maisha.


2. Katika biblia ( Muongozo wa Wakristo)

Kuna vitu vitatu ambavyo biblia inatuagiza kuwa navyo ili tuwe na sifa ya kuoa mke.
Vitu hivyo ni:-

1. Uwezo wa kumhudumia kwa CHAKULA
2. Uwezo wa kumhudumia kwa MAVAZI
3. Uwezo wa kumhudumia kwa UNYUMBA

Soma: KUTOKA 21:10 "Kwamba ajitwalia mke mwingine; CHAKULA chake huyo, na NGUO zake, na NGONO yake, hatampunguzia."

1 WAKORINTHO 7:9 "Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka TAMAA."

Biblia inaainisha mambo ya mhimu matatu hapo mwanzo, ya kumfanyia mke utakaye muoa. Lakini kama hilo la tatu hauwezi,yaani una upungufu wa nguvu za kiume (maana yake jogoo hawiki) basi unapoteza sifa hata kama una V8 Lexus au MAGHOROFA Itakubidi usubiri uendelee kumuomba MUNGU akuondolee kwanza hilo tatizo kabla ya kuamua kuoa. Msingi wa kuoa na kuolewa ni ili kuishinda ZINAA 1 WAKORINTHO 7:2 "Lakini kwasababu ya ZINAA kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.

Kuoa mke wakati bado unatatizo (yaani jogoo hawiki) ni kuongeza matatizo. Ukimuoa ninani atakayempa hitaji hilo la tatu? Maana kama ni chakula na nguo hata WAZAZI au NDUGU zake wanaweza kumpa, kwa ufupi hata yeye mwenyewe anaweza akafanya kazi na kujilisha na kujivisha, hilo la tatu ndiyo linaloleta tofauti na ndiyo msingi na sababu ya ndoa yenyewe wala siyo watoto.

3. Kiserikali (kwanini mpaka uwe na miaka 18)

Umri wa miaka 18 nakuendelea sheria za nchi yetu zinaruhusu kabisa kufanya maamuzi ya busara. Japo wengi hupendekeza angalau miaka 21 kwa kijana na 18 kwa binti ijapokuwa siyo sheria. Katika taifa la Israel kwa mfano vijana wa miaka 14 waliruhusiwa kuoa na mabinti wa miaka 12 hadi 13 waliluhusiwa kuolewa (Google marriage in ancient Israel). Kwanini ilifanyika hivyo, ilikuwa ndiyo muda ambao binti alikuwa anastawi au kupevuka kwa kasi na ili kulinda aibu isitokee akaolewa akiwa hana alama za UBIKIRA; jambo ambalo lingemgharimu kifo.

3.Wazazi kukuzuia kuoa sababu huna pesa ni sahihi kabisa. KWANINI? 👇

Inabidi uwe vyema kifedha ili uweze kujikimu wewe na familia. Kumbuka ya kwamba unapoamua kuoa unaenda kuanza maisha ya kipekee kwani hiyo ndiyo ngazi ya maisha yako ya mwisho mpaka kufa kwako, kumbuka siku utaitwa baba mpaka utakuja itwa babu, kama Mungu atakujalia maisha marefu, hivyo kumbuka utakuwa umekusanya ndugu wa pande mbili zote, sasa usije sema mi naweza nikamlea mke wangu tu! Hapana, kumbuka kuna ndugu wa upande wa mke/mume wako watahitaji msaada je utaweza kumudu? Na maandiko yanasema;
“Lakini mtu yeyote asiyewatunza walio wake, yaani wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini” (1Timotheo 5:8)

Mara nyingine kwa kijana wa kiume unaoa msichana ambaye ni wa kwanza kwao au ni tegemeo kwenye familia yao, na pindi unapoamua kumwoa inamaana tegemeo lote linakuwa ni wewe, sasa sikwambii usimwoe! Hapana, baali hakikisha umejipanga vizuri kukabiliana na majukumu aliyokuwa nayo kwao kwani huwezi kuwatupa ndugu wa upande wake, na siku nyingine watapenda kuja kukutembelea kwako, na wengine watapenda kulala kama ni mbali kidogo, sasa itategemea umejenga nyumba au umepanga nyumba ya namna gani, nasema hivi kwani nimeona pindi tu wanandoa wanapoingia wakiwa hawana hata muda mrefu huwa inaanza misuguano na ukifwatilia utakuta ni ndugu wanajaa nyumbani. Sasa jiandae unaeingia kwenye ndoa kubeba ugeni na kuwajibika kwa hali na mahali.
 
Nikurekebishe israeli ya kale ilikuwa umri wa kuolewa binti ni kuanzia miaka mitatu (3 year old) na mwanaume ni miaka tisa (9 years) , na ili nisionekane napayuka labda nikuwekee aya kutoka moja ya kitabu cha imani yao (MISHNA au Oral torah)

Niddah 5:4

A girl three years and one day old can be betrothed through relations and if a yavam is intimate with her, he has performed an effective yibum. [Note: This is not discussing the advisability of such an act, merely the efficacy.] One can be liable for adultery because of her and she can convey ritual impurity to one who is intimate with her so that the lower mattress on which he sits is ritually impure like the upper mattress. If married to a kohein, she may eat trumah; if an unfit person is intimate with her, he invalidates her from marrying a kohein. If a forbidden relationship is intimate with her, he is executed but she is not. Younger than this age, relations are like putting a finger in the eye (i.e., not halachically effective).

Niddah 5:5

If a boy nine years and one day old is intimate with his yevama, he performs an effective yibum but he is unable to divorce her until he reaches the age of majority. He can be rendered unclean by a niddah so that the lower mattress on which he sits is ritually impure like the upper mattress. He can disqualify (the daughter of a kohein) from eating trumah but he cannot qualify a woman to eat trumah. He renders an animal unfit as a sacrifice (through relations with it) and causes it to be executed by stoning. If he is intimate with a forbidden relationship, she is executed but he is not.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…