Kiongozi Jokakuu, nadhani William Sekule alikuwa ndiye DPP kwa wakati huo. Hv sasa ni jaji mstaafu. Nadhani sijakosea.
..asante.
..William Sekule aliteuliwa kuwa Jaji wa mahakama kuu.
..baadae alikuwa Jaji wa Mahakama ya Mauaji ya kimbari ya Rwanda.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kiongozi Jokakuu, nadhani William Sekule alikuwa ndiye DPP kwa wakati huo. Hv sasa ni jaji mstaafu. Nadhani sijakosea.
Mkuu JokaKuu,
Hao mawakili wa serikali upo sawa kasoro huyo Mbwambo siyo .
Ni Johson Mwanyika ndiye aliyekuwa wakili.
Mbwambo ni mwanahabari.
Ndio ,Mawaziri wakuu wotee ni lazima awe vitengo i mean usalama wa Taifa,au hujui kuhusu hili mbona wengi tu wanalijua.Kumbe Mizengo ni kitengo?
Kwahyo mpaka huyu PM wa sasa ni Mzee wa kitengo?Ndio ,Mawaziri wakuu wotee ni lazima awe vitengo i mean usalama wa Taifa,au hujui kuhusu hili mbona wengi tu wanalijua.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sikujua mkuu.Ndio ,Mawaziri wakuu wotee ni lazima awe vitengo i mean usalama wa Taifa,au hujui kuhusu hili mbona wengi tu wanalijua.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio aisee,,wote lazma wawe vitengo hiyo ni wizara nyeti sanaa lazma uwe usalama wa Taifa.Sikujua mkuu.
Kwaiyo mawaziri wakuu wote ni kitengo?
Mzee pinda nae alikuwa hatariJe, Augustine Mahiga ndiye "Shahidi Y" kwenye kesi maarufu ya uhaini ya mwaka 1983?
Yasemekana alikuwa na kumbukumbu mujarab zilizowezesha kuwasambaratisha washtakiwa.
Kitabu cha Kesi ya Uhaini kilitoka mwaka 1985 kilichokuwa kimeandikwa na Marehemu Mnenge S. Suluja. Mhusika mkuu wa washtakiwa alikuwa Thomas Lugangira au ‘Uncle Tom’. Wenzake walikuwa ni Hatibu Gandi au ‘Hatty Mac Ghee’, Kapteni Mohammed Tamim, Kapteni Mbogoro, Kapteni Christopher Kadege, Luteni Badru Rwechungura Kajaja na Kapteni Mapunda.
Wengine walikuwa ni Banyikwa na mkewe, Christopher Ngaiza, Zacharia Hans Pope, Kapteni Rodrick Rosham Robert, na Eugene Maganga. Kingine kilichokuwa very interesting kwenye kesi ni baadhi ya wana usalama kutumia Alphabet kuji-indetify badala ya majina yao yaani walikuwa Mr. X Kama Mabere Marando, Dr. Hassy Kitine, na Mr Y Dr Augustine Mahiga, nadhani pamoja na Mizengo Pinda nk.
Washtakiwa 9 Kati ya 16 Walihukumiwa kifungo cha maisha. Na Jaji Nassoro Mzava. Mwaka 1993 Walitoka kwa Sababu ya Tanzania kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi hivyo wafugwa wa kisiasa walipaswa kutoka Lakini Hatty MCghee alitoka akiwa mahtuti na akafariki Hospital MCghee aliwahi kutoroka pamoja na Uncle Tom lakini akadakiwa Horohoro Tanga. Mawakili Waliotia Fora ni Hussein Muccadam(RIP) Murtaza Larkha, Jadeja Wote walikuwa wa Asia.
Ameishi ikulu toka enzi za mwl mpaka mwaka 2000 alipogombea ubunge muone hapa hapo ni magogoni hiyo picha ni mwaka 1974Kumbe Mizengo ni kitengo?
Heshima kwako and salute kwakoMkuu Joka Kuu umenikumbusha mbali!
Tulikuwa tunaishi Drive In Estate, mafleti next to Banyikwas, nyumba zimeungana na kutenganushwa na ukuta. Mzee wa Kihangaza, mke Mhangaza, alikuwa na mabinti 4 bomba sana!, Hope, Daines, Betty na Ngola na kaka yao mmoja Mzomu. Hapo ndipo vikao vilipo fanyikia!.
Kesi hiyo ilikuwa na similarities nyingi na Kesi ya Mauaji Mwanza, Mzee wangu, Andrew Mayalla ndio alikuwa RSO wa Mwanza, Jaji alikuwa Nassor Mzavas, DPP alikuwa William Sekule, Mzee wangu alitetewa na wakili Murtaza Lakha, ndie pekee alichomoka, wengine wote walikula mvua nyingi!.
Murtaza Lakha alinifanya nitamani kuwa wakili, by then ukikosa 1st class forget law, ndio nika-opt journalism, he was the best na mpaka sasa bado sijaona wakili yoyote Tanzania aliye vaa viatu vyake!.
P
Nimemuona mkuu.Ameishi ikulu toka enzi za mwl mpaka mwaka 2000 alipogombea ubunge muone hapa hapo ni magogoni hiyo picha ni mwaka 1974View attachment 1442095
Sent using Jamii Forums mobile app
Umenikumbusha mzee peter siyovelwa nilkwenda ofini kwake 2003 akiwa mwenyekiti wa alart nikaongea nae kumbe ndio ilikuwa ya mwisho kuonananaeMzee wangu ni mtu mkimya sana ila kuna siku aliamua kufunguka kuhusu hawa jamaa na mambo waliyoifanyia nchi kuanzia miaka ya 1975-1995 (The Golden Age of Tanzanian Intelligence), kiukweli mwili wangu ulisisimka maana kuna wazee nilikuwa nawafahamu lakini nilikuwa nawachukulia kawaida. Ila kilichonishangaza sana ni kwamba wengi wao kwenye ile orodha walikuwa ni watu wa Njombe na Iringa. Alinisimulia kidogo kuhusu Mzee wetu Comrade Mizengo Peter Pinda na sehemu alizotembelea huko Mashariki ya Kati akiwa na wenzake fulani hivi (Majina Kapuni) siku hizi ni mabalozi wastaafu.
Kuna mambo kafanya Mzee Mahiga ambayo binafsi baada ya kuyafahamu yalinifanya nitokee kumkubali sana yule Mzee wetu.
Japo kuna wengine ambao pia mchango wao ni mkubwa sana japo kutokana na kazi zao hawawezi kufahamika kirahisi, kuna watu kama marehemu wazee wetu wakina Peter Siyovelwa (mbali na ukauzu wake mchango wake ulikuwa mkubwa sana), Mzee Kaduma, Mzee Mayagila na wengine ambao siyo vyema kuwataja maana bado wapo hai.
Nilitamani sana kuandika kitabu kama kumbukizi ya haya matukio, maana kuna baadhi ya wahusika ambao ni rafiki wa mzee wangu walisema kwamba wangenisaidia lakini nikafikiri kwamba sheria zetu za nchi siyo rafiki na naweza kuandika kwa nia njema kabisa halafu nikaishia kuvurugwa tu au kupitiwa na kuandika mambo ambaya sikutakiwa kuyaandika.
Leo niko Iringa mjini na nilitamani sana kwenda Tosamaganga kumzika Mzee wangu Mahiga lakini nimeshindwa kwenda kwasababu kuna mambo hayajakaa sawa kidogo na vikwazo vimekuwa vingi sana. Lakini Mungu amlaze mahali pema sana huyu Mzee wetu na aipe faraja kubwa familia yake. Tanzania imepata pigo kubwa sana kwa kifo chake, yeye ni kati ya wa Tanzania wachache sana ambao ni wajenzi wa sera ya mambo ya nje ya Tanzania (Architects of Tanzania's Foreign Policy) akiwa nyuma ya wanasiasa nguli kama Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mzee Oscar Kambona, Mzee Job Lusinde, Mzee Salim Ahmed Salim, Mzee Abdulrahaman Mohamed Babu, Mzee Mkapa na wazalendo wengine.....
Ambassador MAHIGA was The Man, The Myth and The Legend.........
Duuu hatari sanaaaaaaaInasemekana Baba yako alikuwa mtu mwena na mwenye akili sana na hata mama yako pia naye alikuwa na uwezo mzuri sana kichwani (Hizi ni habari za wambea). Lakini mbona wewe umekuwa ni mtu wa ajabu na hovyo-hovyo kihivi, au vinasaba vya akili vya wazazi wako vimekuruka wewe na kwenda kwa wajukuu ? Man you're a disappointment.....
NO HARD FEELINGS...........
Mzee umebomoka balaaInasemekana Baba yako alikuwa mtu mwena na mwenye akili sana na hata mama yako pia naye alikuwa na uwezo mzuri sana kichwani (Hizi ni habari za wambea). Lakini mbona wewe umekuwa ni mtu wa ajabu na hovyo-hovyo kihivi, au vinasaba vya akili vya wazazi wako vimekuruka wewe na kwenda kwa wajukuu ? Man you're a disappointment.....
NO HARD FEELINGS...........
Mkuu, pia nilishasoma mahali , nadhani ni humuhumu JF kuwa Wakili Lakha alianza kazi kama karani wa mahakama baadaye akajiendeleza na shule ya mambo ya sheria.
Wakuu Chakochangu na Tukundane,Hivi huyu wakili alipotelea wapi? Kwani aliibuka ghafula na kupata umaarufu mkubwa sana katika kesi hiyo na baada ya kesi sidhani kama aliendelea kusikika na kwa wakati ambapo uhuru wa vyombo vya habari haukuwepo, huyu wakili alitisha kweli, mpaka magazeti ya uhuru na mzalendo wakawa hawana jinsi ya kukwepa zaidi ya kuandika makali yake kwa jinsi alivyokuwa anawapelekesha mashahidi wa upande wa jamhuri.