Apollo
JF-Expert Member
- May 26, 2011
- 4,920
- 3,240
Maana nilizozitumia
Ufahamu - Consciousness
Akili - Mind
Ninaposema Akili sina maana ya uwezo wa kufikiri au Intelligence. Ninamaanisha uwezo wa kutambua, kuweka kumbukumbu, kutafakari na ufahamu kwa ujumla. Kwa maana nyingine Akili kwa maana ya MIND. Ninaposema akili ni uwezo wa kutambua sina maana ya utambuzi wa elimu au hekima bali ni kuweza kufahamu hali yoyote au uwezo wowote wa kutambua vitu na hali. Akili na ufahamu vipo pamoja.
Ufahamu ni uwezo wa Utambuzi katika akili. Utambuzi katika ufahamu unafanyika kupitia milango ya ufahamu. Milango ya ufahamu ni viungo ambavyo vinapeleka taarifa katika ufahamu (Consciousness) kwenye akili.
Viungo vya ufahamu na hali zake za ufahamu
Katika ulimwengu wa kifizikia (Mwili), aina hizi za hali za ufahamu/utambuzi zinatumia milango ya ufahamu (Viungo vya mwili) katika utambuzi wa hali mbalimbali za ufahamu
Milango hii ya ufahamu imekutana pamoja kabla ya kufika akilini lakini ilipokutana hapashikiki. Kila unacho kiamini, unacho kikumbuka, unacho kifahamu, unacho kijua kimeingia akilini mwako na katika ufahamu wako kupitia milango ya ufahamu. Unaweza ukawa umekijua kwa kusoma (kuona), kutambua ladha mbalimbali za chakula (kuonja), umekisia kwa mwenzako (kusikia), umekigusa (mfano kugusa kitu cha ncha kali ukajua wembe unakata). Tangu kiumbe kinazaliwa mpaka kinakufa, milango mbalimbali ya ufahamu inatoa taarifa akilini.
Unapotazama kitu na kuweka akili yako hapo, ufahamu wako unaotawala ni ufahamu wa muonekano. Unaposikia sauti ufahamu wako unao tawala unakuwa ni ufahamu wa sauti. Unaponusa harufu, ufahamu unao kuwepo ni ufahamu wa harufu. Unapoonja, ufahamu unaokuwepo ni ufahamu wa ladha. Kutokana na utambuzi wa kupitia milango ya ufahamu, kuna UFAHAMU.
Uwezo wa kuunganisha utambuzi wa kitu, kitu chenyewe na mlango wa ufahamu kwa utambuzi, vyote vinashikilia AKILI.
Akili na Ufahamu vinaweza kufika popote.
Mwili hauwezi kwenda popote kiurahisi kulinganisha na akili. Akili haiitaji VISA kwenda Marekani. Hakuna chombo cha usafiri cha akili. Unaweza kuwaza mambo yaliyopo Marekani hata kama upo Tanzania. Akili ipo kila mahali.
Ufahamu/Akili vinaweza kubadilika kutoka hali moja kwenda hali nyingine kwa haraka na kwa kipaumbele kwenye hali moja Zaidi ya hali nyingine
Ufahamu unaweza kubadilika kutoka aina moja ya ufahamu kwenda aina nyingine ya ufahamu kwa haraka sana. Sekunde moja unaweza kubadilisha unachotafakari. Uwezo wa kubadilika ufahamu wa aina moja kwenda ufahamu wa aina nyingine inatufanya tufikiri kuwa tumeweka ufahamu na akili yetu sehemu zote za kutafakari kumbe akili na ufahamu haviwezi kuwepo kwenye aina Zaidi ya moja kwa pamoja.
Unapokuwa umekaa kwenye kochi, unaangalia TV huku unakula; unaweza ukafikiri akili yako na ufahamu wako vipo katika kusikia, kuona, kunusa harufu ya chakula, kuonja ladha ya chakula na kusikiliza TV kwa pamoja. Sio kweli, ni mazingaombwe ya akili na ufahamu. Akili/ufahamu haviwezi kukaa sehemu Zaidi ya moja na kuwa hali Zaidi ya moja kwa pamoja na kipaumbele sawa.
Kile unachokitazama (perceive) Zaidi au kile unachokipa kipaumbele Zaidi ndicho kinatawala. Kama kipaumbele chako ni kutazama basi hali nyingine za ufahamu zinakuwa chini ya hali ya ufahamu wa kutazama. Sio kwamba hali nyingine za ufahamu hazipo au hazifanyi kazi bali hali nyingine za ufahamu zipo lakini kwenye akili/ufahamu wako hazipewi kipaumbele Zaidi. Lakini pia ufahamu/akili vinaweza kuhama haraka saaana katika muda mchache kuliko speed ya mwanga hivyo inasaidia ufahamu kuwa makini kila wakati. Unaposikia sauti hapohapo akili na ufahamu wako vimehama kwenye hali ya sauti Zaidi ya hali nyingine, na ukitazama hapohapo akili inahamia kwenye hali ya muonekano Zaidi ya hali nyingine. Utaijua ni sauti palepale ulipoisikia, utajua mguso palepale ulipoguswa lakini ufahamu hauwezi kuvipa kipaumbele hali zote za fahamu au hali Zaidi ya moja ya ufahamu.
Akili na ufahamu havina umbo wala hali yoyote ya kifizikia.
Hatuwezi kusema akili/ufahamu ni mweupe, mweusi, mrefu, mduara wala hali yoyote inayoonekana. Bali ni kama energy inayochukua form yoyote kwa haraka sana.
Japokuwa Ufahamu/Akili havina umbo wala havishikiki lakini vinaweza kutumia vitu vya kifizikia
Ufahamu wa muonekano unaanzia kwenye macho, kuona na kinachoonekana, ufahamu wa kusikia unaanzia kwenye sauti, tendo la kusikia na kinachotoa sauti/vibration, ufahamu wa kunusa unaanzia kwenye kinachotoa harufu mpaka kinachonusa, ufahamu wa ladha unaanzia kwenye chochote ambacho kina ladha na kinachoweza kutambua ladha (ndimi) n.k
Ufahamu na akili havina hali ya kifizikia ila vinaweza kutumia vitu vya kifizikia kama vile ubongo, milango ya ufahamu, macho, masikio n.k katika kutenda kazi ila haivitegemei vitu hivyo kuwepo. Mfano ukiwa umeota ndoto, kwenye ndoto hauitaji haya macho kuona, hakuna ngozi kujua mguso, lakini utaota kama vile milango yako ya ufahamu inafanya kazi kumbe haifanyi kazi. Huu mfano wa ndoto unaashiria kuwa kuna uwezekano hata ukifa (mwili pamoja na milango ya ufahamu vikiwa havifanyi kazi) bado ufaham/akili itaendelea kuwepo kwa sababu havitegemei mwili au vitu kuwepo. Ufahamu ni energy, energy haiwezi kufa wala kuharibika kamwe.
Je unaelewa vipi kuhusiana na Akili ni nini na Ufahamu? Karibu katika Topic hii tuelekezane ili sote tuweze kujifunza.

- Aina zote za ufahamu katika muonekano (Sight)
- Aina zote za ufahamu katika sauti (Sound)
- · Aina zote za ufahamu katika ladha (Taste)
- · Aina zote za ufahamu katika harufu (Smell)
- · Aina zote za ufahamu katika mguso (Touch)
- · Aina zote za muonekano ambazo hazitumii milango ya ufahamu wa nje (mfano ukiwa umelala unaweza ukaota na ukawa unaona na kusikia kama vile ni kweli japokuwa macho yamefungwa, aina hii ya ufahamu haitumii milango ya ufahamu lakini inakupa ufahamu pia)
Katika ulimwengu wa kifizikia (Mwili), aina hizi za hali za ufahamu/utambuzi zinatumia milango ya ufahamu (Viungo vya mwili) katika utambuzi wa hali mbalimbali za ufahamu
- · Ufahamu wa muonekano hutambuliwa na macho (seli maalum zenye uwezo wa kutambua mwanga
- · Ufahamu wa mguso hutambuliwa na ngozi (seli maalum zenye uwezo wa kutambua pressure na halijoto au hali baridi)
- · Ufahamu wa sauti unatambuliwa na sikio (seli zenye uwezo wa kutambua mtikisiko hata ukiwa katika mawimbi ya chini)
- · Ufahamu wa ladha unaoweza kutambuliwa na ndimi (seli zenye uwezo wa kutambua chemikali za chakula katika hisia ya uchungu, tamu, chachu nk)
- · Ufahamu wa harufu unaoweza kutambulika na pua (seli zenye uwezo wa kutambua chemikali zenye uwezo wa kuelea hewani)
Milango hii ya ufahamu imekutana pamoja kabla ya kufika akilini lakini ilipokutana hapashikiki. Kila unacho kiamini, unacho kikumbuka, unacho kifahamu, unacho kijua kimeingia akilini mwako na katika ufahamu wako kupitia milango ya ufahamu. Unaweza ukawa umekijua kwa kusoma (kuona), kutambua ladha mbalimbali za chakula (kuonja), umekisia kwa mwenzako (kusikia), umekigusa (mfano kugusa kitu cha ncha kali ukajua wembe unakata). Tangu kiumbe kinazaliwa mpaka kinakufa, milango mbalimbali ya ufahamu inatoa taarifa akilini.
Unapotazama kitu na kuweka akili yako hapo, ufahamu wako unaotawala ni ufahamu wa muonekano. Unaposikia sauti ufahamu wako unao tawala unakuwa ni ufahamu wa sauti. Unaponusa harufu, ufahamu unao kuwepo ni ufahamu wa harufu. Unapoonja, ufahamu unaokuwepo ni ufahamu wa ladha. Kutokana na utambuzi wa kupitia milango ya ufahamu, kuna UFAHAMU.
Uwezo wa kuunganisha utambuzi wa kitu, kitu chenyewe na mlango wa ufahamu kwa utambuzi, vyote vinashikilia AKILI.
SIFA ZA AKILI NA UFAHAMU KWA PAMOJA