sifa za kujiunga jwtz

kaburu mdogo

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2011
Posts
567
Reaction score
400
ni mara nyingi sana nimesikia watu wakizungumza kuhusu kujiunga kwao kwa jwtz,lakini wengi wao huwa hawazungumzii vigezo vyoa zaidi ya afya,je kwa mtu aliemaliza chuo ni sifa zipi za ziada ambazo anatakiwa kuwa nazo kama umri wa kujiunga na mengineyo,nitashukuru kwa kujua hivyo vigezo
 
AFYA ndio kigezo kikubwa! UKIMWI hapana!
 

Kujiunga JWTZ
Uandikishaji
Askari
Mtu yeyote ataandikishwa kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa sifa zifuatazo: -
*. Awe raia wa Tanzania
*. Awe na Elimu ya kidato cha nne nakuendelea na awe amefaulu..
*. Awe hajaoa/hajaolewa
*. Awe na umri kuanzia miaka 18 hadi 25
*. Awe na tabia na mwenendo mzuri
*. Awe na akili timamu na afya nzuri
Masharti ya Utumishi
*. Askari atapewa nambari ya utumishi baada ya kufaulu mafunzo ya awali.
*. Atalitumikia Jeshi kwa kipindi cha mwanzo cha miaka sita, baada ya hapo atafanya kazi kwa mkataba wa miaka miwili miwili kwa kibali cha Mkuu wa Majeshi.
Maafisa
*. Bodi ya Uteuzi wa Maafisa (OfficersSelection Board)
huwafanyia usaili askari wenye elimu ya kidato cha sita na kuendelea toka Vikosini na Shule za askari wapya (Recruitment Schools).
*. Watakaofaulu masailiano hayo hupewa hadhi ya Afisa Mwanafunzi (Officer Cadet), na hupelekwa Chuoni (Tanzania Military Academy) kwa mafunzo yauafisa kwa muda wa mwaka mmoja.
Source:www.tpdf.mil.tz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…