Sifa za mchezaji bora na tuzo zisizokuwa na vigezo

Ladder 49

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2017
Posts
7,918
Reaction score
20,037
Wakuu habari zenu,moja kwa moja niingie kwenye mada.

Hivi nini sifa za mchezaji kuchaguliwa kuwa mchezaji bora?
Maana kumekuwa na malalamiko kwa mashabiki wampira wa miguu kutokulidhizwa na mchezaji bora anayechaguliwa kwenye ligi mbalimbali iwe bongo Au ulaya kila mtu anakuwa anamtazamo wake.

Kila mtu hakubaliani hata na walio kwenye kinyang’anyilo hicho na kusema hakustahili.

Sasa najiuliza hivi zipi ni sifa za mchezaji kushinda mchezaji bora?

Ni vizuri kukawa na vigezo kabisa

Juzi kati hapa luka modric ameshida mchezaji bora wa dunia wa fifa,kila mtu anasema lake kwenye hizo tuzo na kuwepo na mijadala isiyokuwa natija

Oohh,hakustahili,oohh Messi mbona hakuwepo na halistahili wengine sarah hakustahili kuwepo kwenye tatu bora,wengine varane wapo timu moja na modric halafu varane kachukua pia world cup,

Na mengine mengi kila mtu akidai mchezaji wake anayemuona yeye ndio bora kwa vigezo vyake

Sasa nini vigezo vya mchezaji bora?kuchukua vikombe kwenye ligi ulizoshiliki? Au kufunga magoli mengi kwenye msimu wa ligi? Kama ndio kufunga magoli mengi hivyo tuzo za mchezaji bora iwe wa dunia au wa ligi not for defenders .

Wiki iliyopita messi alishinda tuzo ya player of the week ya uefa alifunga goli 2.

Aliokuwa nao kwenye kinyang’anyilo hicho ni neymar,dyabala,na dzeko wote hao waliondoka na mpira na maanisha walipiga hat trick,

Lakini messi akaibuka mshindi,watu wanasema messi kafunga timu kubwa (spurs)wengine hao wamefunga timu ndogo na wakati huo hiyo ligi ni ya mabigwa ulaya.

Mfano niwakumbushe tu msimu ulioisha uefa champions ligi goli la bicycle kick la ronaldo halikushinda goli bora la wiki ila likaja kushinda goli bora la msimu kwanini?

Kwenye mchezaji au goli la wiki wanaachiwa mashabiki wapige kura anayependwa ndio atakaye pigiwa kura nyingi na kushinda.

Kwa upande wako nini sifa za mchezaji bora?

Ni vizuri kukawa kabisa na vigezo vya sifa za mchezaji bora kitakwimu ilikuondoa malalamiko ya wapenda soka japo kwa kiasi fulani.

Nawasilisha.
 
First to reply..nitakuja kutoa sababu
 
Mchezaji bora atapangwa na FIFA na raisi wa klabu ya Barcelona Josep Maria Bartomeu na Raisi wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez.

Kwenye soka hakuna Organization iliyo corrupt kama FIFA na maamuzi yao sometimes huwa yanaonyesha kabisa dalili za rushwa.

Unadhani kwanini Ronaldo hakuhudhuria tuzo za mwaka huu? Alishajua kabisa jamaa lazima wamwekee mtima nyongo kwasababu ameondoka Madrid.

Haya angalia Top Three ya best players.. Modric + Salah + Ronaldo. Sasa ukija kwenye FIFA Pro XI ambacho ni kikosi cha wachezaji 11 mchezaji wa 3 kwa ubora duniani hayupo [emoji23] [emoji23]

Kipa bora wa mwaka T. Courtois hayupo kwenye kikosi bora cha mwaka. Yani umpe tuzo ya kipa bora wa mwaka alafu team bora ya mwaka kipa awe mwingine.

Anyways michakato ya upatikanaji wa hizo nafasi ni tofauti lakini FIFA wanatakiwa wajiangalie na wajitathmini.

Inabidi ku revise hii michakato ikiwezekana bora mashabiki tupige kura tu kuchagua kama tunavyopigia kura goli bora la mwaka (Puskas Award)
 
Hizi tunzo hazifai kabisa kukuepo mimi binafsi sioni faida yake kabisa.

Ronaldo kanuna kwenda kwenye tunzo na kwa kujua kuwa hatoshinda, na shutuma nyingi kuwa Real Madrid wanainfluence kwenye kuchagua mshindi. sasa yeye ndie wakuleta hizi shutuma? ameshinda tunzo ngapi akiwa na Real ? ni kuenesha wazi tu kama yeye mwenyewe walimfanyia mipango ya ushindi huko nyuma sasa saivi ikiwa ni zamu ya mwenziwe yeye anaumia wapi?

amesahau walipompora tunzo Ribery na akapewa yeye?
 
Tatizo la kwanza kwenye hizi tunzo linakuja kwa Fifa na UEFA. Hivi vyama ni corruption tupu. Wapo kimaslahi zaidi tu. ukiwa Real au Barca una nafanzi nzuri ya kubeba tunzo kuliko sehemu yoyote. Nike, Coca cola, Adidas na wadhamini wengine wana nguvu mpaka kwenye uteuzi watunzo.
Na tatizo la pili linakuja kwa wapiga kura. Unaambiwa captain wa timu ya taifa ya Somalia, Burundi, Tanzania, India, Bangladesh, Vietnam wanapiga kura kuchagua mchezaji bora utegemee nini hapo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…