Sifa za Mwanaume anayekuchezea

Sifa za Mwanaume anayekuchezea

Ethan Cruz

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2021
Posts
231
Reaction score
331
1. ANAKWEPA MAZUNGUMZO YA NDOA
Haonyeshi Kufurahi Unapoanzisha Mazungumzo Kuhusu Suala La Kufunga Ndoa Na Wala Hapendi Kuzungumzia Hilo. Wakati Mwingine Hata Kukutambulisha Kwa Ndugu Zake Au Rafiki Inakuwa Shida.

2. ANAGHARAMIA ANASA KULIKO MAMBO MUHIMU
Anakuwa Ni Mtu Wa Kukununulia Mapambo Ya Gharama Na Vitu Vyote Vya Anasa, Lakini Hana Mawazo Ya Kuzungumzia Maisha Yenu Ya Baadaye Wala Kukununulia Vitu Ambavyo Vitakuwa Na Manufaa Katika Maisha Ya Mbeleni. Haangalii Masuala Ya Elimu Wala Kukutafutia Mtaji Au Kazi.

3. HAJALI MACHOZI YAKO
Unaweza Kugundua Ni Jinsi Gani Hana Mpango Mzuri Na Maisha Yako, Kwani Hata Anapokuudhi Anakuwa Hajali Wala Haumizwi Na Machozi Yako, Ni Busara Kuwa Makini Kwa Sababu Huyo Atakuwa Ni Mtu Wa Kukupa Maumivu Wakati Wote.

4. HAJITOKEZI HADHARANI
Mwanaume Ambaye Malengo Yake Ni Kukuchezea Huwa Hataki Mapenzi Yenu Yajulikane Hadharani Atakuwa Mtu Wa Kutaka Mambo Yaende Kwa Siri. Hajitambulishi Kwa Rafiki Wala Kwa Ndugu Zako. Hatoi Nafasi Ya Wewe Kumtembelea Nyumbani Kwake Wala Kuwajua Wale Wa Karibu yake na familia yake.

Ukiona hivyo wanasema akili za kuambiwa, changanya na za kwako...
 
Siku hizi hadi mahari tunalipa lakn ndoa utaiskia tu kwa wenzako.
Tuna update mbinu kama iOS vile. Hii ikigundulika tunaibuka na patch mpya ya kuziba mwanya.
 
Haha [emoji23][emoji38] Unaharibu mkuu. Usiwashtue.
 
Hao ni wachezeaji wa zamani...hawa wa siku hizi wanachezea kuanzia binti mpaka na wazazi wake
 
Back
Top Bottom