Sifa za wabunge ambao hukaa muda mfupi kwenye nafasi zao

Sifa za wabunge ambao hukaa muda mfupi kwenye nafasi zao

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
339
Reaction score
678
Na Elius Ndabila
0768239284

Kwa wiki hizi kumekuwa na mjadala mzito ambao umechagizwa na maoni ya aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Anna Semamba Makinda aliyesema Ubunge wa viti maalumu ungekuwa na ukomo ili waende kugombea majimboni. Hii inamaanisha kuwa Mh Makinda anatamani Ibara ya 66 ya katiba ya nchi inayotaja aina ya WABUNGE na Ibara ya 71 inazungumza ukomo ifanyiwe amendment. Leo staki kuzunguza sana hili, lakini ninataka nikujuze tu kuwa kwa nini WABUNGE au MADIWANI wengine hushika madaraka kwa muda mrefu na wengine kwa muda mfupi? Majibu ya kitafiti yanaonyesha chanzo ni kati ya sababu zifuatazo:-

Muda wa kukaa majimboni unatajwa kuwa ni bakora tosha kwa wabunge wengi. Tafiti zinaonyesha kuwa wabunge wengine na madiwani wakishachaguliwa si rahisi kuwaona kwenye vituo vyao vya kazi. Wapo ambao kila mwaka anaweza kufika mara moja na akaishia kwenye ofisi yake bila kwenda vijijini.

Tafiti zinaonyesha aina hii ya WABUNGE wanaamini fedha ndiyo silaha ya ushindi na unapofika muda wa uchaguzi kwa wabunge wa majimboni utaanza kuwaona wakija majimboni au kutuma fedha kwa wananchi inapotokea tatizo wakati karibia miaka mingi wanakuwa wamejifungia Dar na Dodoma. Halikadharika kwa wabunge wa UWT nao huanza hekaheka za kutengeneza madaraja na kuomba misamaha kwa wapiga kura. Tafiti zinaonyesha hawa wengi kuanzia miaka ya 2010 wamekuwa wanachapwa na wapiga kura kwa kuwatosa.

Makundi pia ni chanzo kikubwa ambacho kimekuwa kikifanya Wabunge wengine kukaa kipindi kimoja tu madarakani. Wabunge wengi baada ya kuchaguliwa wanashindwa kuwa na silika ya kuwaunganisha wapiga kura. Wengi hutengeneza makundi ambayo mwishoni wa siku yanawamaliza. Ni ukweli ulio wazi kuwa wanasiasa dhaifu wao hupenda kusifiwa kwenye kila jambo. Hawapendi kusikia wanakosolewa. Ukisha mkosoa kwa namna ya kutoka ajisahihishe atakuona wewe hufai na atakaye mpongeza hata kwa unafiki huyo ndiye rafiki. Unapofika wakati wa uchaguzi kwa kuwa alishindwa kupokea ushauri ambao ungemsaidia kumjenga na akapokea unao mubomoa hushindwa kurudi kipindi kingine. Kwa tafsiri sahihi ni kuwa aina hii ya WABUNGE wanakuwa wanawashauri ambao ni outdated thinkers, wanashindwa kucheza na wakati.

Utatuzi wa shida za wananchi nayo ni changamoto. Ieleweke kwamba Mbunge haendi eneo lake la kazi na kumia thinking yake ku endorse matatizo ya jamii ni rahisi kushinda mapema. Aina hii ya WABUNGE tafiti zinaonyesha kuwa ni rahisi kuwapelekea wananchi saruji mahali ambapo mahitaji yao ni maji na ni rahisi kuwapelekea watu Mafriji mahali ambapo shida za watu ni barabara na umeme. Hawezi kufanya kwa usajili kwa kuwa hayupo muda mrefu kwenye eneo la kazi na anategemea kuambiwa kwa simu na yeye hutekeleza kwa simu.

Aina hii ya WABUNGE huwa hawadumu madarakani na huondolewa haraka. Hata hivyo ifahamike kuwa Mbunge haleti maendeleo bali ni mhimili unaounganisha serikali na wananchi na wananchi na taasisi. Hivyo kazi ya Mbunge kubwa ni kuwakilisha wananchi kwa kuchukua matatizo yao anayokuwa anakutana nayo kwenye ziara vijijini. Lakini Mbunge Kama haendi vijijini na kufanya ziara kwa njia ya mobile phone si rahisi kwenda na shida za wananchi bungeni, bali ataenda na mtazamo wake. Huyu ndiye kama unashida ya mkate atakupa jiwe. Tafiti zinaonyesha hawa nao hushika nafasi zao kwa muda mfupi.

Jambo jingine ni kuwa njia walizotumia kupata nafasi hizo zinapofika ukomo. Ifahamike kuwa kila uchaguzi unakuwa na kanuni zake mpya ndani ya vyama na serikali. Wakati mwingine vyama vya siasa nusu sank CCM hutengeneza sheria mpya ambazo zinawaondoa watu kwenye mifumo. Kwa mfano mtu aliyeingia kwa rushwa 2015 akijua fika hakuwa na sifa ya kuwa na nafasi hiyo na ni fedha tu zilimbeba, tafiti zinaonyesha hao ni ngumu kurudi 2020 kwani hawana option kwa mzee wa mafaili ambaye ametega rada kila kona. Hawa mifumo ndiyo inawakomesha. Ninapozungumza rushwa si rushwa tu ya fedha bali hata rushwa zingine katika michakato ya upatikanaji wa wagombea hao.

Ubunge unatakiwa mtu ambaye ni mwanasiasa na brain ipo active muda wote, ubunge si hisani. Tafiti zinaonyesha kuwa unapopata Ubunge Kama hisani anapotokea mtu kupambana na wewe ambaye yeye ni politician by born ni rahisi kumuondoa Mbunge ambaye alipata nafasi hiyo kwa kupewa au kununua. Wapo waliojaribu kununua 2010 wakijua fika si wanasiasa ilipofika 2015 waliondolewa kwa kura na pia wapo watakaondolewa 2020 kwa mifumo ileile.

Tafiti zinaonyesha zipo sababu nyingine nyingi zikiwepo kuhama vyama na zingine zinategemeana na kutofautiana kila Wilaya. Lakini msingi wa hoja zote hizo ni CONTEMPT/DHARAU au CONSPECIES/ MAZOEA. Hivi ni vitu viwili ambayo fika vinachangia kwa kiasi kikubwa kuwaondoa watu madarakani. Mtu akishakuwa kiongozi wengi wanakuwa ni much know na huwa hawashauriki/unadmonitive yaani hata akishaurika basi atashauriwa na wengine na siyo waliompa ngazi ya kupandia. Na wakati mwingine hata hiyo ngazi anapanda nayo ili wengine msije mkaitumia kupandia. Atakapohitaji kwenda kuanza upya kupanda ataishusha ngazi ili tena atafute wa kumshikilia ili apande. Hapo ndipo anakutana na watu dhaifu wa kumsaidia kushikilia ngazi ili apande. Anakuta wale wenye nguvu walishatengeneza ngazi nyingine ambayo wanadhani itawasaidia kupandia.

2020
 
Back
Top Bottom